AN-NUUR 
Na.169 Jamadul Akhir 1419, Oktoba 2 - 8, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
 
MAKALA

Unyanyasaji wa kidini mashuleni, vyuoni ukomeshwe 
 

Na Abuu Afahah 

ULIMWENGU sasa unapigia kelele suala zima la aina zote za unyanyasaji na kusisitiza uhuru wa raia, haki za binadamu zikiwemo haki za kusema, kuabudu, kujiunga na vyama na kadhalika. 

Nchi yetu nayo iko mstari wa mbele juu ya kupinga aina zozote za ubaguzi na unyanyasaji. Kwa sababu za kimaumbile mwanamke sasa amekuwa akitetewa sana ili kumkomboa na aina zote za kuonewa. 

Kwa bahati mbaya au kwa makusudi ili watu kulinda imani zao na hutumia kutaka kutimiza nyadhifa zao kukandamiza wengine au kwa kuogopa unyeti wa suala lenyewe, unyanyasaji wa kidini haujapewa nafasi inayostahili. 

Wakati wa ukoloni na mara baada ya uhuru, wakazi wa miji ya Pwani ambao wengi wao ni Waislamu kwa jumla waliogopa kuwapeleka watoto wao shule kwa vile wengi waliokwenda kwenye shule hizo na hasa shule za misheni walilazimishwa kubatizwa, ndio maana leo tunapata watu wengi ambao watoto wao ni Wakristo lakini baba zao Waislamu. 

Wakati ule ilikuwa mtu achague kupata elimu na kuwa Mkristo au abaki na Uislamu wake lakini akose elimu. Hili ndilo wanalolaumiwa Waislamu leo kuwa walibaki nyuma, hawakutaka kupeleka watoto wao shule. Kwa kweli hali inapofikia hivyo kulikuwa hakuna jinsi ila mtu abaki na dini yake. 

Maisha ya katikati baada ya uhuru hali hii ikapungua kidogo hivyo Waislamu wakawapeleka watoto wao kwenye shule za Serikali. 

Kwa bahati mbaya sana hali ile ilianza kubadilika kwa kutumia njia nyingine ambazo mpaka sasa zinaendelea kutumika na njia nyingine zinaendelea kubuniwa. Kilichojitokeza kikubwa ni katika kutekeleza miradi ya kujitegemea. Bila kujali kuwa shule ni za mchanganyiko miradi iliyopewa kipaumbele ni ya ufugaji wa nguruwe ambayo wanafunzi wote walitakiwa kuihudumia wakiwemo Waislamu. 

Kelele nyingi zimepigwa kupinga kitendo hiki, lakini walimu wakuu wengi hawakuzijali kelele hizo halali. Masumbufu mengine wanayoyapata watoto wa Kiislamu ni kukosa mahali pa kusalia. Katika baadhi ya shule hata mtoto kujisalia peke yake chumbani kwake anakatazwa. Tatizo jingine ni wakati wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani baadhi ya shule kwa makusudi ugali wa mchana inakuwa ndiyo futari ya wanafunzi jioni wakati wa kufuturu. 

Sasa kuanzia mwezi Agosti 1995 kumezuka jambo jipya. BAKWATA imeomba serikalini ili watoto wa kike wa Kiislamu watekeleze ibada yao ya kuvaa hijab kama dini yao inavyowataka. Serikali imelikubali ombi hili na imetoa waraka kuwaagiza walimu wakuu na wakuu wa vyuo watekeleze agizo hilo. 

Mpaka leo ni shule na vyuo vichache sana vinavyotekeleza agizo hilo la serikali. Kuna mifano ya shule nyingi ambazo licha ya kukataa kutekeleza agizo hili, watoto waliongia shule hizi wakiwa na hijab zao wanaonekana ni watovu wa nidhamu. Sio hivyo tu bali wananyanyaswa, wanatishiwa kufelishwa, wanaitwa majina mabaya na walimu walezi wao huwatamkia bayana kuwa wanawachukia na kuwauliza wangejisikiaje kama wangeishi katika nyumba ambayo baba yao anawachukia? 

Wizara inalijua hilo, serikali kwa jumla inalijua hilo lakini Wizara haina "uwezo" wa hata kumwelekeza Mwalimu wake mkuu afuate agizo la Wizara. Kama mikoa inajipa uhuru wa kutekeleza au kutotekeleza waraka wa wizara (serikali) basi kuna haja gani hizo waraka kutolewa. 

Taarifa za gazeti hili kama ilivyoelezwa katika matoleo yaliyotangulia ni kwamba kipengere cha hijabu hakiwekwi kwenye "joining instructions" ili kuwajulisha wasichana wa Kiislamu washone sare za hijabu. Huu ni ushahidi wazi kwamba walimu wakuu ambao ni Wakristo wanatumia nyadhifa zao kutekeleza matakwa ya dini zao na kuzikandamiza dini nyingine. 

Sasa iwapo kila mmoja kwa nafasi yake aliyonayo atafanya njama za makusudi kudhalilisha dini za wengine nchi hii tutakuwa tunaielekeza wapi. Hivi ni vitendo vya dhahiri vinavyojenga chuki baina ya waumini wa dini mbalimbali. 

Ifahamike kuwa hawa watoto wanaonyanyaswa leo kwa ajili ya dini zao ndio viongozi wa kesho. Kama tunajijengea misingi ya ubaguzi itabidi nao walipize kisasi watakapopata nyadhifa hizo hizo ambazo leo nyie mnazo. 

Athari haitaonekana haraka, lakini tujue kuwa nchi hii tunaipeleka pabaya. Matatizo tunayoyasikia kwamba nchi za wenzetu hayakuanza jana ni mrundikano wa ukandamizaji wa muda mrefu mpaka kufikia mahali watu wakaona hakuna hata haja au umuhimu wa kuishi. 

Tulio madarakani leo tusiipeleke Tanzania huko. Misingi ya amani ni kuvumiliana na kuheshimiana ndani ya makabila mengi, dini nyingi, mikoa mingi n.k.. 

Kama wizara ya Elimu inaliona hili kuwa ni jambo dogo ijue kuwa inapanda mbegu ya mti mchungu ladha yake watakuja kuionja vizazi vyetu vya baadaye. 

Suala la imani ni suala nyeti. Tusirudi tulikotoka wazazi wanaopenda kutekeleza vilivyo dini zao wakalazimika kuacha watoto wao wasiende shule kwa kuwaogopea hawatavaa hijabu au watoto wa kike walio tayari kuvaa hijabu wasifikishwe mahali wakasema bora kukosa elimu kuliko kumuasi Mwenyezi Mungu kwa kutembea uchi kwa mujibu wa Qur’an. 

Bado hapa anayezungumzwa ni mtoto wa kike ambaye serikali imepania kumkomboa na binti wa Kiislamu naye ni mtoto wa kike. 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 TAHARIRI 
Majeshi ya nje kupelekwa Lesotho: Je, ni sera za Nguvumali? 

Nyumba ya Wakfu yageuzwa  Baa Dar 
Na Mwandishi Wetu 

‘VAT’ yaingia Bakwata Same 
 Na Mwandishi Wetu 

Mchungaji asema hakuna mihadhara ya kashfa 
 Na Muhibu Saidi 

Maoni yetu: Masheikh tupeni Fatwa 

Safari yangu Ufini 
Ustaadh Ka-Batembo 

Unyanyasaji wa kidini mashuleni, vyuoni ukomeshwe 
Na Abuu Afahah 

Wanaume toeni haki za wanawake 
Na Zabibu Iddi Ng’onda Box 78, Mwadui 

MAONI: Yesu ni yule yule Isa 
Na Saleh Ngoi 

Hatuna uwezo wa kuwapinga manabii 
Na Elia Batendi, S.L.P. 538, DSM 

Ukoloni mwingine unaingizwa nchini? 
Sheikh Thabit H. Mbago,S.L.P. 21486,DSM 

Khatamy ni ‘Gorbacheiv’ mwingine? 
Na Athman Rajab 

Tufuate Uislamu kwa vitendo na siyo kwa maneno 
Mwandishi: Maalim Ali Bassaleh 

AN-NUUR  lina chuki na Wakristo 
Na Charles Kamuhabwa, DSA Mtwara 

Msiiparamie ovyo Biblia 
Na Sheikh Bernard P. Nyangasa 

Yaliyosemwa na viongozi wa dini juu ya idadi ya watu 1989 
Na Rajab Rajab 

Uislamu ulivyoingia Zanzibar -2 

Waislamu Moro watakiwa kutoyumba 
Na Rajab Rajab, Morogoro 

Wanawake Masasi wawataka Masheikh kutangaza sheria za Allah 
Na Muhibu Saidi, Masasi 

Ugaidi na Uislamu siyo kitu kimoja – Sheikh Jongo 
Na Bakari Musa 

Sheikh Abbas awataka wananchi Dodoma waepuke upuuzi 
Na Abu Zubair, Dodoma 

Vijana watakiwa kujiepusha na ‘vijiwe’ 
Na Badru Kimwaga 

Mafundisho ya Quran 
Kutoa katika njia ya Allah: Al-Baqarah aya   261-263 

Barua za wasomaji 

Mashairi 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na Lishe 
Magonjwa yanayoathiri lishe 
  

 

 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita