NASAHA
Na. 053 Jumatano Juni 21 - 27, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
MICHEZO

Michuano ya Kombe la Ulaya: 
Uingereza, Ujerumani nje 

UBELGIJI

MZUNGUKO wa kwanza wa kundi D ambalo liliitwa 'kundi la kifo' umemalizika huku vigogo wa soka barani Ulaya timu za Uingereza na mabingwa watetezi Ujeramani kutolewa nje ya mashindano hayo.

Uingereza ilitolewa baada ya kuchapwa mabao 3-2 na timu machachari ya Romania katika mchezo uliofanyika jana usiku. Romania ilikuwa ya kwanza kupata bao lilifungwa na mchezaji Chinvi baada ya kupiga krosi ambayo iligonga mwamba na kuingia wavuni. Bao hilo lilisawazishwa katika dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza kwa penalty iliyopigwa na kapteni wa Uingereza Allan Sheerer. 

Mshambuliaji wa Uingereza Michael Owen alifungia timu yake bao la pili dakika ya tatu baada ya kuanza kipindi cha pili. Romania ilisawazisha bao hilo kwa shuti kali lililofungwa na Monteano kupitia mpira uliopanguliwa na kipa wa Uingereza. Goli la tatu na la ushindi kwa Romania lilipatikana kwa njia ya penati kupitia mchezaji Ganes katika dakika ya 87. 

Hadi tunakwenda mitamboni tulikuwa hatujapata matokeo halisi ya mchezo kati Ureno na Ujerumani. 


Washabiki wamshangaa Mkapa, wambeza Sumaye 

Na Mwandishi Wetu 

WASHABIKI kadhaa wa soka jijini Dar es Salaam wamemshangaa Rais Benjamin Mkapa kwa kuanza kuzungumzia matatizo yanayoikumba sekta ya michezo nchini wakati uchaguzi mkuu unakaribia.

Wamesema, inashangaza Rais wa nchi anakaa kimya kwa kipindi cha miaka minne mfululizo bila kushughulikia matatizo na migogoro iliyo ndani ya michezo hususan soka nchini mpaka inaangamia kiasi hiki. 

Rais Mkapa juzi mjini Mwanza alikaririwa akikemea migogoro ndani ya vilabu na vyama vya michezo nchini wakati akifungua michezo ya Shule za Sekondari nchini (UMISETA). 

Washabiki hao wameonesha wasi wasi kwamba huenda Rais Mkapa ana agenda ya siri na kura za wanamichezo kwa kuwa ameanza kuonesha kukerwa na maendeleo mabovu ya michezo nchini wakati muda wake wa kuyashughulikia hayo wamedai umekwisha. 

Wakizungumzia kauli ya Waziri Mkuu Frederick Sumaye aliyoitoa hivi karibuni jijini ya kuiomba Jamhuri ya Watu wa China kujenga uwanja wa kisasa wa kandanda hapa nchini, washabiki hao wamesema ni kauli ya kujionesha kwa Watanzania kama serikali yake inajali michezo. 

Sumaye alitoa ombi hilo kwa Waziri Mdogo wa Utamaduni wa China ambapo aliwaomba kufanya hivyo kama walivyojenga nchini Uganda, Kenya na Zanzibar. 

"Kwa kweli haya wanayoyazungumza waheshimiwa hawa (Mkapa na Sumaye) ni mambo ya msingi lakini kwanini waanze kuyazungumza wakati huu wa hekaheka za uchaguzi mkuu", amehoji mwanamichezo Joseph Robert. 


BMT waipiga ngwara FAT 

Na Mwandishi Wetu 

BARAZA la Michezo Tanzania (BMT) limetengua maamuzi ya Chama Cha soka Nchini (FAT) yaliyokuwa yameziteremsha timu za Majimaji ya Songea, Reli ya Morogoro, Toto Africa ya Mwanza na Mji Mpwapwa ya Mpwapwa kutoka Ligi Kuu mpaka ligi daraja la kwanza.

Uamuzi huo umekuja kufuatia Majimaji na Reli kukata rufaa barazani kupinga hatua ya FAT kuzishusha daraja timu zao baada ya kushika mkia katika hatua ya awali ya ligi kuu Tanzania Bara iliyozishirikisha timu 16. 

"Baraza" limefikia uamuzi huo baada ya kugundua kwamba Halmashauri Kuu ya FAT yenyewe haikuidhinisha utaratifu wa kuzishusha ligi timu zozote mwaka huu, kwa hiyo katika hili FAT wameshindwa", amesema Said El-Mamry Mwenyekiti wa BMT. 

Juu
 

YALIYOMO
 
 

Tahariri
Uhuru wa kuabudu utiwe katika matendo bila ya ubaguzi

Kauli ya Sumaye yawakera wananchi

Licha ya Katiba ya nchi kutambua uhuru na haki ya kuabudu: Qur’an kizimbani

CCM yapata kiwewe

Wapinzani Waishutumu sheria mpya ya uchaguzi

Mtoto wa Afrika yutaabani

CCM wanatumia pesa za serikali kwa kampeni - Chenyenge

USHAURI NASAHA
Dhuluma haiondoki bila kubadili mfumo

Habari za Mikoani

Kalamu ya Mwandishi
Kweli CUF ni ngangari!

MAKALA
Manabii wa kale na mageuzi

MAKALA
CCM na sera za maendeleo

MAKALA
Wajibu wa wananchi kwenye uchaguzi mkuu

Habari za Kimataifa

Lishe
Kuhifadhi matunda kwenye jokofu

RIWAYA
Dunia ndivyo ilivyo - 3

MASHAIRI

MICHEZO

  • Uingereza, Ujerumani nje
  • Washabiki wamshangaa Mkapa, wambeza Sumaye
  • BMT waipiga ngwara FAT

  • -

       Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita