NASAHA
Na. 053 Jumatano Juni 21 - 27, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
MAKALA

CCM na sera za maendeleo: 
Kutumia vitisho badala ya hoja za kisiasa 

Na Rajab Kanyama 

MWEZI Oktoba mwaka huu wa 2000, kutafanyika uchaguzi mkuu wa pili, tangu mfumo wa vyama vingi vya siasa, urejeshwe nchini mwaka 1992.

Uchaguzi Mkuu, unaofanyika kila baada ya miaka mitano.Kwa mujibu wa sheria, chini ya Ibara namba65(1) ba 65(2) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ndio hitimisho la mfumo wa utawala wa kidemokrasia, unaowawezesha wanasiasa binafsi na pia vyama vya siasa, kuweza kushika madaraka ya kuongoza nchi. 

Hapa,tungependa ieleweke wazi kwamba, kuongoza nchi, na kutawala nchi ni vitu viwili tofauti. 

Wakoloni walitawala nchi, na ndio sababu, wazeewetu walifanya juhudi kubwa na mwisho wakafanikiwa kuwaondoa, maana walikuwa wanatunyonya na kufunyanyasa ndani ya nchi yetu wenyewe. 

Kwa bahati mbaya, hata baada ya kupata uhuru, hali haikubadilika sana tukaondoa watawala Wakoloni, Wazungu Mapagani, na kuwapa madaraka watawala, Wakoloni weusi, ambao kimsingi, walijifunza kazi kutoka kwa Wazungu mapagani na kwa hivyo wakapewa jukumu la kuendeleza ukoloni,siku hizi, unaitwa mambo leo, kwa niaba ya Wazungu mapagani. 

Kazi ya kiongozi wa nchi, ni kubuni na kusimamia shughuli za serikali, kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi, na kujenga mazingira ambayo yatawawezesha kupata mafaniko ya kiuchumi. 

Hii ni pamoja na kukidhi haja za makundi maslahi, hasa kwa vile haiwezekani wananchi wote wakawa na shida zinazofanana, au kundi maslahi, lililokiwezesha chama na mwanasiasa husika, kupata ushindi. 

Hii, ndio sababu ya kuwa na Ilani ya uchaguzi. 

Wananchi wenzangu, ni vema tukaanza sasa kujiuliza, kama ni kweli Chama Cha Mapinduzi(kabla ya hapo, TANU na Afro) ambacho kimekuwepo madarakani kwa zaidi ya miaka 40 hivi leo, kimefanikiwa katika kutatua au angalau kupunguza matatizo ya msingi ya wananchi wa Tanzania. 

Maana,ni kwa kufanya hivyo tu ndipo tutakapo kuwa na uwezo wa kufikia uamuzi sahihi wa chama cha kukipa kura zetu, wakati wa uchaguzi utakapofika. 

Tusiruhusu kufuata maoni, au ushawishi wa baadhi ya vyombo vya habari, na makundi mengine, kama vile BAKWATA, ambayo mara nyingi hutumika ili kuwapotosha wananchi, kwa malengo ya kisiasa. 

Fikiri kwa makini kuhusu matatizo yanayokukabili, ukosefu wa ajira, ugumu wa kupata matibabu, kusomesha watoto, chakula cha kila siku na mengine kadhaa, na utazame kama serikali iliyoko madarakani ina mkakati wowote wa kushughulikia matatizo hayo, ukiachilia mbali kuyaondoa kabisa. 

Mwananchi, unapaswa kuelewa kwamba, jukumu la kwanza kabisa la erikali yoyote ulimwenguni, ni kushughuliki mambo tuliyotaja, na ndio sababu Ibara ya 8 (1)(b) ya Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania inaelekeza wazi kwamba, "Lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi." 

Je ni kweli kuwa serikali yetu inaelekea kutimiza wajibu huo? 

Yapo matatizo kadhaa yanayowakabili wananchi, na 

wao kudhani kwamba ni yao binafsi, sivyo, chanzo chake ni mfumo ya muundo mbovu wa utawala uliopo kwa hivi sasa. 

Uchaguzi, ndio ushahidi wa kweli wa kuonyesha kwamba, madaraka ya kutawala kisiasa yanapatikana kutoka kwa wananchi, na kwamba viongozi wanaochaguliwa, hupewa dhamana tu, na kwa hivyo wanapaswa kusimama na kuendesha mambo, kwa mujibu wa matakwa ya wananchi. 

Hiki, ndio kigezo pekee cha kuwapimia viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, Wabunge na serikali yake. 

Waulizeni, kwa nini hawataki kusikiliza malalamiko yenu, mbali mbali? Waulizeni, ni kweli kwamba mwananchi anaweza akawa mzururaji ndani ya nchi yake mwenyewe? Waulizeni, kwa nini wale polisi waliouwa pale Mwembechai mpaka leo bado hawajafikishwa Mahakamani, na wazee wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyovunjika Je?au Kwa vile wengi wao ni Waislamu ndio maana hawastahili kulipwa haki zao? 

Viongozi wa kuchaguliwa, ni lazima wawajibike kwa wananchi, bila ya kufanya hivyo, tusiwarudishe madarakani. 

Wananchi, wakati wetu umefika,jamaa, wanaanza kuja tena kuomba nafasi ya kula, safari hii tuwashikishe mkaa wa moto, ili iwe ni ovyo kwao wapenda kula kwamba wanapodharau shida zetu na kutufanyia jeuri na kiburi, tutawasubiri wakati muafaka tuondoe kiburi chao. 

Moja ya faida,ya kuwa na vyama vingi vya siasa, ni kudhihirisha na kuthibitisha kwamba wananchi wenye dini, shida, masalahi na mitazamo tofauti kuhusu maisha, wanaweza kuishi pamoja kwa amani na utulivu. 

Wananchi wote wanafahamu kwamba, ili kupatikane maendeleo, ni muhimu kabisa amani na utulivu, vikadumishwa. 

Ni jambo la kusikitisha sana kuona kuwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, na Serikali yake,, siku hizi wamekuwa nambari wani kwa kauli za vitisho za kijumla jumla, kiasi cha kuwafanya wananchi wabaki hoi kwa kuwa na maswali mengi yasiyo na majibu. 

Katika Doria ya matamshi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, iliyofanywa na mwandishi wa makala hii, hapa tutanukuu dondoo kutoka katika gazeti la Chama Cha Mapinduzi, UHURU la tarehe 8 Juni 2000; ili tuweze kubainishani viongozi wa chama kipi, ndio wanaotenda na kutamka maneno, yanayoweza kuvuruga amani na utulivu wa nchi, kwa malengo ya kisiasa. 

Kwa maandishi makubwa katika gazeti hilo sura ya mbele Muhariri anatufahamisha. 

"Mkapa atahadharisha: Zipo njama za kupenyeza mfarakano Bara. 

*Asema baada ya uhasama kuwa umeenezwa Zanzibar. 

* Asema ni njama zifanywazo na wapinzani." 

Je ndugu wananchi kuna ukweli wowote katika madai haya. Wiki ijayo tutachambua kwa kina habari nzima ili tujielimishe, na kuzijua mbinu mpya za kuwalaghai na kuwapotosha wananchi kwa lengo la kuzipata kura zao. 

Tuwe macho, safari hii tuwadhihirishie wapenda kula kwamba sisi ndio tunaowapa ajira. 


MAKALA 

Wajibu wa wananchi kwenye uchaguzi mkuu 

ZIKIWA zimesalia siku miezi michache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ni muhimu kwa kila mwananchi kujua jukumu lake katika kipindi hiki muhimu. Kipindi ambacho kama kutakuwa na maandalizi na mikakati ya kweli nchi itakombolewa kutoka kwa watu wachache wanaofaidi matunda ya uhuru. Mwandishi B.A. MAUA anafafanua zaidi.

NCHI inapokuwa chini ya utawala mzuri kila mtu atafurahia bila kujali kuwa yeye ni tajiri au masikini, mkulima au mfanyakazi, mkereketwa wa chama tawala au la; Matunda ya utawala bora hautajali misingi ya dini wala kabila, watu wote watakuwa sawa na weny efuraha ya uhuru! 

Lakini kinyumechake nchi itakapo kuwa na utawala mbovu; unaoendekeza ubinafsi, ubaguzi, utawala usiofuata na kuheshimu sheria zake zenyewe, utawalausiokuwa namipango ya kiutekelezaji. Serikali inayoshindwa kupambana narushwa,ubadhirifu na uonevu kwa wananchi basi watakaoathirika zaidi ni wananchi wa hali za chini, wanyonge wa sio na kitu. 

Katika utawalambovu walewenye nacho au waliopewa nafasi maalumu ya upendeleo katika utendaji wa serikali hawataathirika. Wao watasikilizwa kwa kila watakacho kitaka. Wanyonge namasikini watubaki kuwa hivyo kwao afya bora ni vitu vya kusikia tu, elimu bora ni ndoto za mchana. Watoto wao ndiyo watakao achashule kwa kukosa ada. Siku zote watasimangwa kuwa si watuwanaopenda elimu na ilihali utawala ndio unaowafanya wawe hivyo. 

Na litakapotokea tatizo lolote kama ukame namagonjw ayamilipukokama kipindupindu wao na watoto wao ndiyo watakao kufa kamanzige. 

Hii ndiyo hali halisi ya maisha ya Watanzania zaidi ya asilimia 80mijini na vijijini. Wanachi wanyonge wanawajibika bila kujali itikadizao za kisiasa, dini, wala kabila kuhakikisha kuwa wanabadilisha hali zao za kimaisha kwa kusaidia kuuwekautawala ulio bora utakao waondolea matatizo waliyonayo. 

Njiakuu ya kuhakikisha kuwa nchi inapata utawala bora ni kwa kushiriki katika kutoa elimu ya demokrasia, kuhamasishajamii kuwa na mwamko wa kisiasa. Ni muhimu wananchi wakaelimishwa nani mbaya wao.Wananchi wanapaswa kuambiwa kuwa inawezekana kabisa utawala uliopo unaweza kuondolewa madarakani kwa njia ya kura. 

Katika kutoa elimu ya Demokrasia si lazima kuandaa mikutano ya hadhara elimu ya demokrasia inaweza kutolewa kwa njia mbali mbali kutegemea na nafasi ya mtu na mazingira yaliyopo. Kwa mfano (1) kuanzisha mijadalakwenye mikusanyiko ya watu, kwenye mabasi, mabaraza yajioni na kadhalika. 

Pili kuhamasisha watu walio karibu nawe, marafiki, ndugu najamaa. Hapa unaweza hata kuwaandikia barua kwa walewaliombali bilakujali chama chao. Wahamasishe nauwaandae kwa uchaguzi wawe tahari kuleta mabadiliko kwa kura. Toa mifano iliyohaiinahogusa halihalisi ya maisha yao. 

Katika familia zetuza Kiafrika, ukoo ni taasisi pana sana, kunaupande wa mama naupande wa baba. Haowote wanahitaji elimu ya uchaguzi u.Ujumbeukiwafikia wote basi utakuwa umefanya kazi yaziada. 

Tatu tunaweza kuanzisha vikundi mbali mbali vya kutoa elimu ya demokrasia. Vikundi hivi vinaweza kutembea sehemu mbali mbali kutoa elimu. Huu si wakati wa kuwaacfhia wanasiasa pekee yao kutembea 

Sehemu zote. Kutokana na vikwazo mbalimbali si rahisi kwao kutembea sehemu zote za nchi. Hata vyombo vya habari navyo havifiki sehemu zote navilevinavyofikasehemu zote kwa namna moja au nyingine vinapigia debeserikali ilioko madarakani. 

Pia huu si wakati wa kusifia tu AhLipumba ni kiboko bwana! Anachambua juchimi ile mbaya! Oh mchungaji Kakobeanawakanyaga CCM kisawa sawa! Hii haitoshi ni lazima nasisi tuchukue nafasi zetu. Wakati kama huu kila mtu ni lazimaawe mchezaji, mfungaji magoli. Kwa sasa haifai mtu kuwa mshangiliaji. Tuwe washangiliaji baada ya uchaguzi kwisha sio leo. Sote ni jukumu letu kuondoa dhulma kwa vinywa na mikono yetu. 

Tusiwaachie walewanaofaidi matunda ya uhurukutoa elimu yauraia peke yao kilainapowezekana tuandae semina, warsha, namakongamanmo yautawala nademokrasia. Wasomi mnaoelewa nini maana ya utawala mbovu msijitenge na jamii. Si kila msomi anaelewa nini maana ya utawala mbovu mfano wa hao niwale wanaoanda na kushiriki mikutanoya kuipongeza serikali kwa kile kinachodaiwa kusamehewa madeni. Hawa ni wasomi wasioelewa kitu wako tayari kuwasaliti wananchi kwa thamani ndogo tu. 

Wanyonge katika kipindi hiki wasichoke kuleta mazungumzo ya kisiasa misikitini, makanisani, mashuleni na hata kupiga simu redioni kuchangia mada mbali mbali zenye mwelekeo wa kisiasa. Wanyonge hawapaswi kuziacha nafasi adimu kama hizi. 

Kwenye siasa hakuna dogo na mshindi hupatikana hata kwa kura moja.Tukumbuke mfano mmoja wa Zanzibar. Salmin anaongoza kwa kura 2000tu! Kwa hiyo kura kama hizo pia zinaweza kuiondoa CCM madarakani. Ni jukumu lako ndugu msomaji kuanza leo kushiriki kuhamasisha na kutoa elimu ya uchaguzi. Siku nilizozitaja hapo juu si nyingi. Anza leo. 

Juu
 

YALIYOMO
 
 

Tahariri
Uhuru wa kuabudu utiwe katika matendo bila ya ubaguzi

Kauli ya Sumaye yawakera wananchi

Licha ya Katiba ya nchi kutambua uhuru na haki ya kuabudu: Qur’an kizimbani

CCM yapata kiwewe

Wapinzani Waishutumu sheria mpya ya uchaguzi

Mtoto wa Afrika yutaabani

CCM wanatumia pesa za serikali kwa kampeni - Chenyenge

USHAURI NASAHA
Dhuluma haiondoki bila kubadili mfumo

Habari za Mikoani

Kalamu ya Mwandishi
Kweli CUF ni ngangari!

MAKALA
Manabii wa kale na mageuzi

MAKALA
CCM na sera za maendeleo

MAKALA
Wajibu wa wananchi kwenye uchaguzi mkuu

Habari za Kimataifa

Lishe
Kuhifadhi matunda kwenye jokofu

RIWAYA
Dunia ndivyo ilivyo - 3

MASHAIRI

MICHEZO

  • Uingereza, Ujerumani nje
  • Washabiki wamshangaa Mkapa, wambeza Sumaye
  • BMT waipiga ngwara FAT

  • -

       Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita