NASAHA
Na. 053 Jumatano Juni 21 - 27, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
TAHARIRI
S.L.P. 72045, Dar es Salaam

Uhuru wa kuabudu utiwe katika matendo bila ya ubaguzi


 


Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeeleza wazi kuwa kila Mtanzania yuko huru kuamini na kuhubiri dini anayoitaka. Aidha imeelezwa katika katiba hiyo ambayo ndiyo sheria mama ya nchi kuwa shughuli hizo za dini zitakuwa nje ya uendeshaji wa mamlaka ya nchi.

Hata hivyo, Waislamu nchini kwa muda mrefu wamekuwa wakidai kuwa uhuru huo uliotolewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hautekelezwi kwa upande wao bali kwa Wakristo tu.

Wakithibitisha madai yao hayo, Waislamu wamekuwa wakitoa mifano kadhaa ikiwemo Waislamu kushitakiwa kwa kusema "Yesu sio Mungu" hali ya kuwa maneno hayo yamo katika kitabu chao, Qur'an, ambacho kwacho Waislamu huapa na serikali hukubali viapo vyao.

Mifano mingine ambayo Waislamu wamekuwa wakiitoa kuonesha kutotendewa haki kwa sababu ya dini yao kama Katiba ya nchi inavyoagiza ni kuundiwa BAKWATA na serikali. Wakati hili linafanyika Waislamu wanadai Wakristo wamekuwa wakipewa uhuru wa kuunda na kuendesha taasisi zao bila ya kuingiliwa na serikali, na kuhubiri dini yao bila bughudha.

Mara kwa mara wahadhiri wa Kiislamu wamekuwa wakitiwa misukosuko, wakilazwa rumande na kufunguliwa mashitaka kwa kutamka yale ambayo wanayasoma katika Kitabu chao.

Kwa kuzingatia madai ya Waislamu na utendaji wa serikali sisi tuna kila sababu ya kukubaliana na madai ya Waislamu, kwamba vitendo vya serikali na vyombo vyake ni kinyume kabisa na uhuru wa dini uliotolewa na katiba yetu ya Jamhuri.

Kwa hiyo, tunaikumbusha serikali iweke katika matendo uhuru wa kuabudu uliotolewa na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ikiwa ni kweli "Yesu si Mungu" ni maneno yaliyomo katika Qur'an, na kwa kuwa serikali inaitambua Qur'an kuwa ni kitabu kitukufu kiasi cha kuweza kukubali kiapo cha mtu anayeapa kwa hiyo Qur'an, inakuwaje basi Waisalmu wasumbuliwe kwa vile tu ni kinyume cha imani ya Mtanzani mwingine?

Mbona kauli na matendo ya dini zingine zisizokuwa Uislamu ambazo zinakwenda kinyume na Imani ya Kiislamu haziwatii katika misukosuko kama ilivyo kwa Waislamu.

Pamoja na kuikumbusha serikali kwamba kutotenda haki baina ya raia wake ni 'kutengeneza nyufa katika kuta za jengo la amani', pia tunatahadharisha kuwa gharama za kirejesha amani ni kubwa zaidi.

Juu
 

YALIYOMO
 

Tahariri
Uhuru wa kuabudu utiwe katika matendo bila ya ubaguzi

Kauli ya Sumaye yawakera wananchi

Licha ya Katiba ya nchi kutambua uhuru na haki ya kuabudu: Qur’an kizimbani

CCM yapata kiwewe

Wapinzani Waishutumu sheria mpya ya uchaguzi

Mtoto wa Afrika yutaabani

CCM wanatumia pesa za serikali kwa kampeni - Chenyenge

USHAURI NASAHA
Dhuluma haiondoki bila kubadili mfumo

Habari za Mikoani

Kalamu ya Mwandishi
Kweli CUF ni ngangari!

MAKALA
Manabii wa kale na mageuzi

MAKALA
CCM na sera za maendeleo

MAKALA
Wajibu wa wananchi kwenye uchaguzi mkuu

Habari za Kimataifa

Lishe
Kuhifadhi matunda kwenye jokofu

RIWAYA
Dunia ndivyo ilivyo - 3

MASHAIRI

MICHEZO

  • Uingereza, Ujerumani nje
  • Washabiki wamshangaa Mkapa, wambeza Sumaye
  • BMT waipiga ngwara FAT

  • -

       Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita