|
|
| Chakula
ni silaha ya kukabiliana na changamoto ya kansa
Na Mujahid Mwinyimvua KANSA au saratani inawezekana kuwa ndiyo ugonjwa unaoshika nafasi ya kwanza kwa kuogopwa ulimwenguni. Kwa madaktari kansa ni ugonjwa wa kawaida kwa kiasi fulani, lakini kwa watu wenye ugonjwa huo, huona kana kwamba wameshahukumiwa adhabu ya kifo. Baadhi ya wanasayansi wanasema kuwa woga kuhusu ugonjwa huo hauna msingi. Kwa sababu katika miaka ya hivi karibuni tumejifunza njia za kujikinga na pia za kutibu maradhi ya aina za kansa. Wanasayansi hao wanaamini kuwa utafiti unaozidi kufanywa huenda ukaleta mafanikio makubwa hasa katika upatikanaji wa tiba bora zaidi kwa aina zote za kansa. Kimsingi kansa si ugonjwa rahisi na unahitaji juhudi za mtu binafsi na zile za watalaamu. Kwa upande wa mtu binafsi, jambo la kuzingatia ni kuwa kansa haitokei kwa ghafla. Bali hukua kidogo kidogo na hasa kwa kuchochewa na aina ya vyakula vya mtu anavyokula na aina ya maisha anayoishi kwa ujumla. Makala hii imekusudiwa kutazama mchango wa chakula katika kukabiliana na tatizo la kansa. Aina ya chakula anachokula mtu na aina ya maisha yake ni silaha kubwa ya kuukabili ugonjwa wa kansa na silaha hiyo ni rahisi na wala hahitaji fedha za kigeni. Kwa kigezo cha ugonjwa wa kansa, vyakula vinagawanywa katika makundi makubwa matatu. Kundi la kwanza ni vyakula vinavyochochea kansa. Kundi la pili ni vyakula vinavyozuia kansa na kundi la tatu ni vyakula ambavyo vipo kati kwa kati (neutral). Yaani havichochei wala havizuii kansa. Mfano wa makundi ya vyakula vilivyotajwa hapo juu na maelezo yake ya kina na aina ya kansa inazoweza kuchochea au kuzuia tutaziona katika makala zetu zijazo panapomajaaliwa. Kwa leo tuanzie makala yetu kwa kutazama mwongozo wa chakula utakavyosaidia kukabiliana na changamoto ya kansa. Vile vile katika mwongozo huo tutaona mfano wa baadhi ya makundi ya vyakula vilivyotajwa hapo awali. Mwongozo wa vyakula Kula kiasi kidogo vyakula vyenye mafuta. Hapa ni vyema nikakumbusha kuwa vyakula vinavyokaangwa kwa mafuta na halafu mafuta yanabaki kwa wingi katika vyakula hivyo, kwa mfano chips – mayai, ni hatari kwa afya. Badala yake kula vyakula vilivyopikwa. Mafuta yanachangia sana kupatikana kwa kansa hasa ya tumbo, matiti na ile ya viungo vya uzazi. Hata hivyo, usiache kula kabisa vyakula vyenye mafuta kwa sababu mafuta yanahitajika kwa maendeleo ya afya yako. Kinachosisitizwa na watalaamu ni kutokula kiasi kikubwa cha vyakula hivyo. Kula chembechembe/punje za nafaka (zisizokobolewa) zilizopikwa kila siku. Mfano mzuri hapa ni chakula cha kande (makande) mseto (choroko) au kunde na mchele). Kula mboga za majani na matunda kila siku. Matunda hasa yanayosisitizwa hapa ni yale ya jamii ya machungwa (machungwa, machenza, n.k) na mboga za majani ni zile zenye vitamini A kwa wingi kwa mfano karoti. Vyakula kama vile nyanya, viazi vitamu na kabichi vinasaidia kuzuia kansa. Vile vile inaaminika kuwa vyakula vyenye madini ya ‘selenium’ ni kinga ya ugonjwa wa kansa. Madini hayo yanapatikana kwa wingi katika samaki na vyakula vya nafaka (mahindi, mchele, mtama, n.k.) zisizokobolewa. Kula kiasi kidogo vyakula vilivyotengenezwa au vilivyohifadhiwa kwa kutumia chumvi. Vyakula hivyo ni vile vinavyotengenezwa kiwandani na pia kienyeji kwa mfano papa, nguru, ham, sausage, hot dogs, bacon, mboga mboga (vegetables) n.k. Kula kiasi kidogo cha vyakula vilivyokaushwa au vilivyobanikwa kwa kutumia moshi. Vyakula vya kundi la hapo juu vinachochea kansa ya tumbo na kolomeo (Eosophagus). Acha kunywa pombe na uvutaji wa sigara, tumbaku, bangi, n.k. na utumiaji
wa vileo na madawa ya kulevya yote kwa ujumla.
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Wasomi watetea haki ya wananchi kumiliki ardhi Serikali izungumze na wananchi–Mzee Gonga Akina mama watakiwa kushikamana na dini yao Maoni
Dondoo
za Saikolojia: Hoja kengeza
Makala ya mtangazaji
Makala
Tanzania
tuna sera gani kuhusu kanda
Mdahalo
kati ya Waislamu na Wakristo- 2
Teknologia
Makala na habari
Mwinyimkuu
kufanya sensa ya waumini Magomeni
Wazazi
Mwanza wahimizwa kuwashonea watoto wao Hijab
Tuwaige
Wangazija, 'tutafanikiwa'
Serikali
imeweka rekodi ya kutisha – Sheikh Salim
Muhadhara
waunguruma Geita
Fuateni
Sharia ya Allah - Sheikh
Wanawake wa Kiislamu Mburahati wahimizwa kutafuta elimu Mafunzo
ya Qur'an
Chakula na lishe
|