|
|
| Akina
mama watakiwa kushikamana na dini yao
AKINA mama Waislamu wametakiwa kushikamana na dini yao kama njia pekee ya kujikomboa. Hayo yamesemwa na wahadhiri mbalimbali kwenye kongamano la siku moja lililofanyika Oktoba 24, katika Msikiti wa Ijumaa Kigogo CCM Jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo lililohudhuriwa na akina mama wa Kiislamu wapatao 1500 lilianza saa mbili asubuhi kwa Qur’an tukufu, na kufuatiwa na mada ya elimu iliyotolewa na Amirah wa akinamama - Wilaya ya Kinondoni, Bi. Zaituni Ahmad ambaye alisisitiza kuwa elimu haina faida kama haitekelezwi. La muhimu ni kufanyia kazi yale yote tulioyasoma, alisema na akawataka akina mama wote ambao mpaka leo bado hawajajiunga na darsa za akina mama haraka sana wajiunge. Alisema Uislamu hautaki watu wajinga, na huwezi kuwa na uchungu na Uislamu ikiwa huufahamu. Mada ya pili ilikuwa ni harakati za Kiislamu iliyotolewa na Ummu Hamza kubwa zaidi aliloliongelea ni kuusimamisha Uislamu katika maisha ya kila siku na kwamba Uislamu ndio mkombozi pekee wa kweli wa matatizo ya akina mama. Aidha, alisema kwamba Qur’an ndio dira na mwongozo wa Waislamu na wala haitakiwi kutekeleza baadhi ya Aya bali Aya zote. Bi Fatuma Lazaro, Katibu wa Kamati ya Kutetea Haki za Akinamama (T),
alielezea kuwa tatizo kubwa kwa Waislamu ni kutokuishi Kiislamu katika
maisha yao ya kila siku, na dawa pekee ya huku kunyanyaswa na kudhalilishwa
ni kuuteleza Uislamu vilivyo, kwani nusra haiji kwa kutamani tu basi, bali
huja baada ya kuchukua sababu za nusra na Allah habadilishi hali za watu
mpaka wajibadilishie wao wenyewe kwanza.
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Wasomi watetea haki ya wananchi kumiliki ardhi Serikali izungumze na wananchi–Mzee Gonga Akina mama watakiwa kushikamana na dini yao Maoni
Dondoo
za Saikolojia: Hoja kengeza
Makala ya mtangazaji
Makala
Tanzania
tuna sera gani kuhusu kanda
Mdahalo
kati ya Waislamu na Wakristo- 2
Teknologia
Makala na habari
Mwinyimkuu
kufanya sensa ya waumini Magomeni
Wazazi
Mwanza wahimizwa kuwashonea watoto wao Hijab
Tuwaige
Wangazija, 'tutafanikiwa'
Serikali
imeweka rekodi ya kutisha – Sheikh Salim
Muhadhara
waunguruma Geita
Fuateni
Sharia ya Allah - Sheikh
Wanawake wa Kiislamu Mburahati wahimizwa kutafuta elimu Mafunzo
ya Qur'an
Chakula na lishe
|