AN-NUUR 
Na.173 Rajab 1419, Oktoba 30 - Novemba 6, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
 
makala ya mtangazaji 

Khatamy sio Gorbacheiv!!! 

Gorbacheiv Mkomonisti !!! 
 

BWANA Khatamy Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Irani anataka kusahihisha na kurekebisha tu na hali ya kuwa anafuata misingi ya Uislamu. Waandishi wa khabari Duniani baada ya miaka ishirini ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Irani mpaka hivi sasa haya Mapinduzi hawajayaelewa wanatoa tafsiri na uchambuzi potofu kama walivyokuwa wakitoa mwanzo wa Mapinduzi haya. 

Waandishi, wafasiri na wachambuzi wengi wa habari duniani ni Wakimagharibi (WAZAYUNI) na mara nyingi wamekiri kuchambua na kufasiri habari za Iran na Kiislamu kimakosa. Makosa yao yanatokana na kutokufahamu Uislamu vizuri pamoja na Mapinduzi ya Kiislamu. Waislamu wote wanafuata mwongozo mmoja ambao haujabadilika kwa muda wa miaka 1400 hivi sasa nao ni Qur’an na Sunnah. Leo vyombo vya waandishi wa habari vya Kimagharibi vinayarudia makosa na tuhuma zao zilizopita !! Ambazo lengo lao ni kuatia Waislamu mashaka na uongozi na viongozi wao mpaka wavunjike moyo. 

Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwenye Umoja wa Mataifa ililenga kwenye kurekebisha uhusiano wa kimataifa kwa njia ya mazungumzo (diplomasia) vyombo vya habari vya Kimagharibi vimeelewa vibaya kama kawaida yao, na kutoa habari za uzushi kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imebatwilisha Hukumu ya Kifo kwa Mwandishi wa kitabu cha Aya za Shetani (The Satanic Verses) Salman Rushdie. 

Hawa maadui wa Kiislamu waelewe kuwa Iran haina uwezo wa kubadilisha Hukumu za Kiislamu na Hukumu hiyo itabaki vile vile kwa mujibu wa Waislamu wote Duniani kuitekeleza. 

Hivi sasa baadhi ya mashirika nchini Iran yameongeza zawadi kwa mtu atakayemuua Salman Rushdie mpaka kufikia Dola za Kimarekani milioni mbili (2,000,000 $). Viongozi wa Iran wakati wowote ule hawakusema wala hawatasema kuwa Hukumu ya kifo (Fatwa ya Imam Khomein) kwa Salman Rushdie imebatwilishwa. 

Ulamaa wa viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umetaka kuona hukumu ya Imam Khomein ikitekelezwa kwa haraka iwezekanavyo. Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Bwana Khatamy ni Ulamaa na ni miongoni mwa wanafunzi bora kabisa wa Imam Khomein na anaelewa vizuri sana kuliko mtu yeyote yule. 

Hukumu ya Imam Khomein lazima itekelezwe. Bwana Khatamy anaelewa, anaamini na kufuata vizuri Fikra za Imam Khomein na misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu kuliko mtu mwingine ama maadui wa Kiislamu na vyombo vyao vya habari hutoa taswira na picha mbaya na potovu juu ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. 

Bwana Khatamy anataka kusahihisha tuhuma, uongo na upotofu uliosingiziwa Mapinduzi ya Kiislamu, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Bwana Khatamy anataka kubainisha kinaga ubaga picha na taswira halisi na sahihi ya Mapinduzi ya Kiislamu ulimwenguni, vyombo vya habari vya Magharibi kama kawaida yao kupotosha habari kwa ajili ya manufaa yao. Hatuwezi kabisa kumfananisha Bwana Khatamy Ulamaa Mkubwa wa Kiislamu na Mikail Gorbacheiv Mkomonisti. Mikail Gorbacheiv hakuusambaratisha Ukomonisti bali Ukomonisti wenyewe ulikuwa hauwezi kwenda na wakati kwa hiyo ulijisambatarisha wenyewe na kabla ya kusambaratika kwa Urusi Imam Khomein alitangaza kuwa Dola kubwa ya Kikomonisti itasambaratika na akawaonya wasifuate tena mwendo wa Kimagharibi bali aliwataka wafuate mfumo wa Kiislamu baada ya Ukomonisti, alikuwa bila ya washauri na kudhibitiwa. Lakini Bwana Khatamy yuko chini ya kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatollah Khamenei na vyombo mbalimbali ambavyo ndiyo vinavyoongoza Iran kwa pamoja ili kuyapatia ushindi Mapinduzi haya ya Kiislamu Duniani. 

YADUMU MAPINDUZI YA KIISLAMU 

MUHAMMAD JAVAD TASKHIRI 

MWAMBATA WA UTAMADUNI 

UBALOZI WA IRAN – NCHINI TANZANIA 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 

TAHARIRI 
Wakipewa fursa watainusuru nchi

Wasomi watetea haki ya wananchi kumiliki ardhi

Serikali izungumze na wananchi–Mzee Gonga

Akina mama watakiwa kushikamana na dini yao

Maoni
Serikali inaWhite Paper:  Wananchi mna nini?

Dondoo za Saikolojia: Hoja kengeza
Na Abu Halima Sa Changwa

Makala ya mtangazaji
Khatamy sio Gorbacheiv!!!

Makala
Malipo ya fadhila
Na Mohamed Saleh

Tanzania tuna sera gani kuhusu kanda
Na Abu Abdullah, Tanga

Mdahalo kati ya Waislamu na Wakristo- 2
Na Nandenga wa Mkomidachi

Teknologia
Jifunze Kuunganisha Kompyuta (3)
Na Hassan Omar

Makala na habari
'Usiiparamie ovyo Theolojia'
Na Charles Kamuhabwa, DSA Mtwara

Mwinyimkuu kufanya sensa ya waumini Magomeni
Na Jamillah Nassoro

Same tusilimu upya

Wazazi Mwanza wahimizwa kuwashonea watoto wao Hijab
Na Idd Katimba, Mwanza

Tuwaige Wangazija, 'tutafanikiwa'
Mwandishi: Maalim Bassalah

Serikali imeweka rekodi ya kutisha – Sheikh Salim
Na Mwandishi Wetu

Muhadhara waunguruma Geita
Na Hussein Abdallah, Geita

Fuateni Sharia ya Allah - Sheikh
Na Badru Kimwaga

Wanawake wa Kiislamu Mburahati wahimizwa kutafuta elimu

Mafunzo ya Qur'an
Vijana wa pangoni

Barua za wasomaji 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na lishe
Chakula ni silaha ya kukabiliana na changamoto ya kansa
Na Mujahid Mwinyimvua

 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita