|
Wasomi na Wataalamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wameelezea haja ya kuangalia upya suala la umiliki wa ardhi kuwa mikononi mwa Mamlaka Kuu pekee (Executive) na wananchi wengine kuwa kama kwamba hawana haki yoyote katika ardhi zao za asili.
Wamesema mwananchi leo anayemiliki ardhi kwa taratibu za mila hana haki na anaweza kuhamishwa wakati wowote na akihurumiwa sana alipwe fidia ya mazao na sio ardhi
Hayo yalisemwa na wasomi hao kufuatia tukio la wananchi wa Nzasa kuhamishwa
kwenye makazi na mashamba yao bila hata ya fidia. Endelea...
Serikali imeweka rekodi ya kutisha – Sheikh Salim
Na Mwandishi Wetu
KITENDO cha serikali kuchoma moto mashamba na vyakula vya wananchi wa Nzasa kimemuhuzunisha kila mtu aliye japo na chembe ya ubinadamu katika nafsi yake.
Hayo yameelezwa katika khotuba ya Ijumaa katika Msikiti wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Oktoba 23, 1998.
Katika khotuba yake, Khatibu Sheikh Salim Khotour alisema kwamba serikali
imeweka rekodi ya kutisha na ya kipekee kwa kufanya vitendo ambavyo dunia
nzima huvinasibisha na ama wahuni au magaidi. Endelea...
|
|
|