|
|
|
WAKATI mfuko wa sadaka Tanga ukiingia mwaka wake wa nne, zimetolewa habari zenye kuzidi kutia moyo. Katika taarifa yake ya mwaka ambayo hutolewa kila mwezi wa Ramadhani, inaonyesha kuwa jumla ya shilingi 263,720 zilikusanywa kutokana na visanduku vinavyoning’inizwa sehemu za biashara za Waislamu. Taarifa hiyo iliyosainiwa na mdhamini wake mkuu, Sheikh Nassor Rashid, inaonyehs pia kuwa shilingi 60,000 zilipatikana kama zaka za mali kutoka Waislamu waliovutiwa na taarifa ya mwaka jana. Zaidi ya fedha hizo kutumiwa kuwalipa walimu wa Maarifa ya Kiislamu wa shule za msingi ya Mwanzange, pia shilingi 33,000 zilitolewa mkopo kwa mwalimu mmoja anayejitolea kufundisha somo hilo kwenye shule za sekondari ili zimsaidie kuendeleza mradi wake. Akizingumza na mwandishi wa habari hizi kufuatia kutolewa kwa taarifa hiyo, Sheikh Nassor alionyesha kukasirishwa na baadhi ya watu wenye kupinga sadaka za aina hii, hasa kwenye jiji la Dar es Salaam. Badala yake alitoa wito kwa Waislamu kuwa madhubuti kwa suala hili, na akapendekeza kwa kila Muislamu kuwa na sehemu ya kukusanyia sadaka kwenye biashara yake pamoja na zaka zenye kuwawajibikia. Akifafanua juu ya namna bora ya utekelezaji, alisema kila mmoja anaweza kutengeneza sehemu hiyo kulingana na nafasi yake, inaweza kuwa cha kuning’inia au kwa kutoboa kwenye kuta. Alisema mara sadaka ya kutosha ya fedha itakapopatikana, mfnyabiashara mwenyewe achukue jukumu la kuzipeleka sehemu maalum ya kukusanyia itakayokuwa na jukumu la kutatua matatizo mbalimbali ya Waislamu wa eneo hilo. Kwa uzoefu wake alisema, ukusanyaji wa aina hiyo hutumika katika nchi za Ghuba, na sehemu kubwa kupelekwa kwenye nchi maskini za Kiislamu kama yetu. Kutokana na ufinyu wa bajeti, taarifa ya mwaka huu haikuweza kupelekwa kwa kila mkusanyaji na wameombwa radhi kwa hilo. Wale wote wenye maombi na maswali juu ya namna ya kutekeleza mradi huu wanaweza kutumia anuani ifuatayo: Katibu, MSADAT, S.L.P. 6082, Tanga.
Mjue Usama bin Ladin VYOMBO vya habari vya nchi za Magharibi vimekuwa vikimtangaza kama ni gaidi wa Kimataifa na serikali za nchi hizo Marekani ikiwa mbele, zinamsaka kwa udi na uvumba kwa madai ya vitendo kadhaa vya kigaidi. Je, umepata kumsikia bin Ladin mwenyewe akijieleza? Je bin Ladin anapambana na nani na kwa maslahi ya nani? Basi kuyajua hayo na mengineyo mengi, usikose toleo lijalo. Insha-Allah.
|
YALIYOMO
Tahariri Baada ya futari nzuri: Tuwatupie macho wenye njaa Rais Mkapa kuwa mgeni rasmi Baraza la Idd Waumini, Masheikh Arusha wasutana kwa futari ya Mrema Dondoo za saikolojia
MSADAT yazidi kutia moyo Tanga MAFUNZO KUHUSU FUNGA YA RAMADHANI Michezo isiyoruhusiwa katika Uislamu Ustadh Farid: Kijana aliyejitolea kuwapa Da'awa watalii Hakuna Magharibi wala Mashariki:
Uislamu ni ubinaadamu
Ijue madrasati Mar-wa ya Dodoma
mjini
Ijue Madrasat Jadidul Fiqhyyat
- Tabata Kimanga
Madrasat Hidayatul Muumini Mwadui Washindi wa mashindano ya Hadithi za Mtume (s.a.w.) wapatikana Madrasa Shafii Ujiji Kigoma yaonyesha umahiri wake Waanzisha mifuko kusaidia wagonjwa Dodoma Waislamu Kondoa waomba msaada kumalizia Msikiti Mnyororo wa imani-2
Kutoka magazeti ya zamani:
Jengo la Waislamu Moshi lageuzwa
Kanisa la Walokole
Masjid Nurania yaswaliwa
Ijumaa
Jabal Hira kutoa mafunzo
ya Kompyuta Morogoro
Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|