AN-NUUR 
Na.184 Ramadhan 1419, Januari 15 - 21, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Kutoka magazeti ya zamani:
Wanaoshitakiwa kwa uhaini kortini leo
Uhuru, Jumatano, Juni 24, 1970 Na. 1817
 

USIKILIZAJI wa kesi ya uhaini ya watu saba ambayo ilipangwa kuanza leo katika Mahakama Kuu, huenda ukahairishwa kwa sababu ya kutoelewana juu ya Mawakili watakaowatetea washitakiwa. 

Mpaka jana jioni ilikuwa haijajulikana ni nani atakayemtetea Michael Kamaliza. Bw. Kassam ambaye ndiye aliyekuwa amepangwa kumtetea tangu hapo awali amejitoa katika shughuli hiyo kwa sababu anakwenda ng’ambo kwa mafunzo zaidi. 

Bw. Talati, ambaye alichukua nafasi ya Bw. Kassam anasemekana kuwa ameondoka Dar es Salaam. Mwandishi wake aligoma kumweleza Mwandishi wa UHURU ni mahali gani alikokwenda ijapokuwa amesema atarejea baada ya siku mbili. 

Washitakiwa saba wanaokabiliwa na mashitaka ya makosa manne ya uhaini. Mashitaka yao yanaeleza vitendo mbalimbali vya uhaini na mojawapo ni kushirikiana na mkimbizi Oscar Kambona katika mpango wa kutaka kumuua Rais na kuipindua serikali halali ya Tanzania mnamo Oktoba mwaka jana. 

Mmoja wa washitakiwa hao, William Chacha ambaye mpaka hivi karibuni alikuwa Ofisa wa Mambo katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania katika Peking, inasemekana alidai kutoka kwa Kambona jumla ya shilingi milioni 20 kama bei ya kuipindua serikali ya Tanzania. 

Washitakiwa wengine ni Gray Likungu Mattaka (34), Mwandishi wa Habari, John Dustan Lifa Chipaka (38), Katibu Mkuu wa zamani wa chama marehemu cha African National Congress, Bibi Titi Mohammed (45), Rais wa zamani wa Umoja wa Wanawake, Michale Marshal Mowbray Kamaliza (46), Katibu wa zamani wa TANU na Waziri wa Kazi, Eliya Dustan Lifan Chipaka (32), Kapteni wa zamani wa Jeshi la Ulinzi na Alfred Philip Millinga (27), Luteni wa zamani wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania. Wote wamekanusha hatia ya mashitaka. 

Upande wa mashitaka utasimamiwa na Mwanasheria Mkuu wa serikali Bw. Mark Bomani, akisaidiwa na Makamu wa Mwanasheria Mkuu. 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
Tahariri 
Baada ya futari nzuri: Tuwatupie macho wenye njaa 

Rais Mkapa kuwa mgeni rasmi Baraza la Idd 

Ubungo yakumbwa na ukame 

Waumini, Masheikh Arusha wasutana kwa futari ya Mrema 

Dondoo za saikolojia 
Na. Abu Halima Sa Changwa 

Waislamu turejee kwa Allah 

MSADAT yazidi kutia moyo Tanga 

Mjue Usama bin Ladin 

MAFUNZO KUHUSU FUNGA YA RAMADHANI 

Michezo isiyoruhusiwa katika Uislamu 

Ustadh Farid: Kijana aliyejitolea kuwapa Da'awa watalii 

Hakuna Magharibi wala Mashariki: Uislamu ni ubinaadamu 
Na Abubakari S. Marwillo 

Ijue madrasati Mar-wa ya Dodoma mjini 
Na Abu Zuberi, Dodoma 

Ijue Madrasat Jadidul Fiqhyyat - Tabata Kimanga 
Na B. Mwakangwale 

Madrasat Hidayatul Muumini Mwadui 

Washindi wa mashindano ya Hadithi za Mtume (s.a.w.) wapatikana 

Madrasa Shafii Ujiji Kigoma yaonyesha umahiri wake 

Waanzisha mifuko kusaidia wagonjwa Dodoma 

Waislamu Kondoa waomba msaada kumalizia Msikiti 

Mnyororo wa imani-2 
Na Sheikh Bernard P. Nyangasa 

Kutoka magazeti ya zamani: 
Wanaoshitakiwa kwa uhaini kortini leo 

Jengo la Waislamu Moshi lageuzwa Kanisa la Walokole 
Na Mwandishi Wetu, Moshi 

Masjid Nurania yaswaliwa Ijumaa 
Na Rajab Rajab, Morogoro 

Jabal Hira kutoa mafunzo ya Kompyuta Morogoro 
Rajab Rajab na Mussa Ally, Morogoro 

Sayansi na Teknolojia 
[Internet ni nini?] 

Masomo ya Dini ya Kiislamu 

Barua za Wasomaji 

Mashairi 

Chakula na lishe 
[Thamani ya mlo wa Uyoga] 
 


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita