|
|
|
Washindi wa mashindano ya Hadithi za Mtume Muhammad(S.A.W.) yaliyo andaliwa na Africa Muslims Agency wamepatikana. Washindi hao ni: Abdi Kassim Jiba wa Daarul-Hadiith Assalafiyya ya Tanga Aliyeshika nafasi ya kwanza na alijipatia Shilingi.75,000/-, Cherehani na kitabu cha Sahiih Bukhaariy. Aliyeshika nafasi ya pili ni Ibrahim Kibwana kutoka Madrasatul-Azhar ya Dar es Salaam na alijipatia Shilingi .50,000/, Radio Cassette na kitabu cha Sahiih Bukhaariy Ally Jumanne wa Ma’had Ansaar Sunna ya Arusha alishika nafasi ya tatu na alijipatia Shilingi 25,000/= na Fani ya wima. Aidha washindani wote kumi walio shiriki katika mashindano hayo walipata zawadi za vitabu, boksi moja la tende na shuka (saruni). Mashindano hayo yalishirikisha vijana kumi kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Arusha na Iringa na yalifanyika Desemba 5, 1998 katika ukumbi wa Star Light Jijini Dar es Salaam. Akitoa nasaha zake katika mashindano hayo, mgeni rasmi Sheikh Abdulqadir Juneid alilipongeza Shirika la Africa Muslims Agency kwa kuandaa mashindano hayo na pia aliwapongeza vijana washindani kwa uwezo wao mkubwa walio uonyesha wa kuhifadhi, kufahamu na kuzichambua Hadithi. Naye Mkurugenzi wa Africa Muslims Agency Bw. Abderraheem Ben-Ainouss akizungumza katika mashindano hayo alisema kuwa Shirika lake limeandaa mashindano hayo ya Hadithi ili kuikumbusha jamii ya Kiislamu juu ya umuhimu wa Hadithi ambazo ndio chimbuko la pili la sheria za Kiislamu baada ya Qur’ani. Aidha mratibu wa mashindano hayo Sheikh Mbwana A. Urari aliwashukuru wale wote walio fanikisha mashindano hayo na hasa wale walio toa zawadi kwa washindani. WANACHUONI 58 wa madrasati Shafii ya Ujiji katika Halmashauri ya mji wa Kigoma hivi karibuni walifanya maonyesho ya masomo siku ya kufunga chuo hicho ambacho ni tawi la madrasati Muumin kwa ajili ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Katika sherehe hiyo wanachuo walifanya maonyesho ya Hadith, Sira pamoja na sheria na mashairi kuhusu dini ya Kiislamu, mafunzo ambayo yalilenga katika kujenga uadilifu kwa Waislamu mbele ya Mwenyezi Mungu. Mwajuma Yasin (14) alianza kwa kuwakumbusha Waislamu ubora wa kufunga katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ambayo ni nguzo ya nne kati ya nguzo tano za dini ya Kiislamu. Mwanachuo huyo alisema Muislamu katika kufunga anatakiwa ajizuie kula, kunywa na pia kuacha kukutana kimwili kati ya mke na mume wakati wa mchana kama njia ya kuonyesha utii mbele ya Mwenyezi Mungu. Mwanachuo mwingine Zuhura Mwamadi (13) aliwaasa Waislamu kutoshiriki katika kunywa pombe, kinywaji ambacho kimeharamishwa na Mwenyezi Mungu, kwani ni chanzo kikubwa cha kuchochea maasi. Aidha, wakati wa maonyesho hayo yaliyohudhuriwa na wazazi wa wanachuo, wanachuo wengine waliotoa nasaha zao kupitia aya mbalimbali ni pamoja na Sungura Ruti (14) aliyewataka Waislamu kuitafuta elimu na baadaye kuieneza kwa wenzao ili kusaidia maendeleo yao. Sungura alitoa mifano ya elimu kama vile useremala, kushona na kufuma nguo, kuwafundisha Waislamu ufasaha mambo yaliyoamrishwa kufanywa na Mwenyezi Mungu ikiwa ni pamoja na yaliyokatazwa kwa kutumia vitabu vya dini. Mwanachuo Sango Mwamadi na Zawadi Abdallah nao waliwataka Waislamu kutofurahia kuona machafu, yaani madhambi, mfano kutukana na kusengenya pamoja na kuwaheshimu wazazi kama alivyoamrisha Mtume Muhammad (s.a.w.). Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya maonyesho hayo, mwalimu wa madrasa hiyo Ustadh Jalaleni Ramadhani aliwakumbusha baadhi ya wazazi ambao huchelewa kulipa ada, kufanya hivyo bila kuathiri utaratibu wa chuo hicho. |
YALIYOMO
Tahariri Baada ya futari nzuri: Tuwatupie macho wenye njaa Rais Mkapa kuwa mgeni rasmi Baraza la Idd Waumini, Masheikh Arusha wasutana kwa futari ya Mrema Dondoo za saikolojia
MSADAT yazidi kutia moyo Tanga MAFUNZO KUHUSU FUNGA YA RAMADHANI Michezo isiyoruhusiwa katika Uislamu Ustadh Farid: Kijana aliyejitolea kuwapa Da'awa watalii Hakuna Magharibi wala Mashariki:
Uislamu ni ubinaadamu
Ijue madrasati Mar-wa ya Dodoma
mjini
Ijue Madrasat Jadidul Fiqhyyat
- Tabata Kimanga
Madrasat Hidayatul Muumini Mwadui Washindi wa mashindano ya Hadithi za Mtume (s.a.w.) wapatikana Madrasa Shafii Ujiji Kigoma yaonyesha umahiri wake Waanzisha mifuko kusaidia wagonjwa Dodoma Waislamu Kondoa waomba msaada kumalizia Msikiti Mnyororo wa imani-2
Kutoka magazeti ya zamani:
Jengo la Waislamu Moshi lageuzwa
Kanisa la Walokole
Masjid Nurania yaswaliwa
Ijumaa
Jabal Hira kutoa mafunzo
ya Kompyuta Morogoro
Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|