AN-NUUR 
Na.184 Ramadhan 1419, Januari 15 - 21, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Tahariri
Baada ya futari nzuri:
Tuwatupie macho wenye njaa
  

KAMA ilivyo kawaida ya kila mwaka viongozi wa ngazi za juu serikalini Ramadhani hii wamewaandalia futari Masheikh na baadhi ya wazee mashuhuri jijini Dar es Salaam. Japo futari hii huandaliwa mara moja tu kwa mwezi, lakini ina ujumbe mzito zaidi ya chakula chenyewe. 

Kwanza ni kujenga maelewano, mapenzi na udugu kama Mtume (s.a.w.) alivyousia kwamba: "Alikaneni (kwa chakula n.k.) mtapendana". Pili na kubwa zaidi ni zile fadhila na thawabu anazozipata muumini anapomfuturisha Muislamu mwenzake aliyefunga. 

Japo si Waislamu wote waliopata fursa ya kufuturishwa Ikulu au kwa Mh. Makamu wa Rais; lakini ule udugu na kutakiana kheri kuliko onyeshwa hapana shaka kunakusudiwa kwa Waislamu wote. 

Yeyote mwenye kutoa sadaka kwa imani na ikhlasi huichunga sadaka yake isiruke patupu. Haifuatilii kwa maneno ya kero na adha. Na yeyote aliyehiji Hija Mabrur haitii matope hija yake anaporejea. 

Ni matarajio yetu kwamba baada ya kupeana futari nzuri tutapeana pia mkono wa kheri wa Idd el Fitr. Hatutarajii leo tufuturu pamoja kwa furaha siku mbili baadae tena furaha yote ya Eid itumbikie nyongo kwa kauli zetu za masimango na kejeli. 

Siku ya Eid el Fitr ni siku adhim ni siku ya furaha, siku ya kula na kunywa vilivyo vizuri basi tupeane fursa ya kusherehekea. Tupeane kauli njema; tupongezane na tupeane nasaha za matarajio mema. 

Wakati wengine tukila futari kwa wasaa, vyombo vya habari vinaarifu kwamba huko Kilwa wanafuturu embe. Basi hawa nao tuwazingatie na tuwahurumie. 

Moja ya mafunzo ya funga ni kutupa fursa kupata hisia azipatazo ashindae na njaa kwa umasikini wake. Kama tunaweza kuwafuturisha wenzetu ambao tangu hapo wana uwezo wa kujifuturisha; kama ishara ya kuonyesha udugu na mapenzi miongoni mwetu; basi udugu huo unastahiki tuuonyeshe zaidi kwa hawa wenzetu wafuturuo embe. 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
Tahariri 
Baada ya futari nzuri: Tuwatupie macho wenye njaa 

Rais Mkapa kuwa mgeni rasmi Baraza la Idd 

Ubungo yakumbwa na ukame 

Waumini, Masheikh Arusha wasutana kwa futari ya Mrema 

Dondoo za saikolojia 
Na. Abu Halima Sa Changwa 

Waislamu turejee kwa Allah 

MSADAT yazidi kutia moyo Tanga 

Mjue Usama bin Ladin 

MAFUNZO KUHUSU FUNGA YA RAMADHANI 

Michezo isiyoruhusiwa katika Uislamu 

Ustadh Farid: Kijana aliyejitolea kuwapa Da'awa watalii 

Hakuna Magharibi wala Mashariki: Uislamu ni ubinaadamu 
Na Abubakari S. Marwillo 

Ijue madrasati Mar-wa ya Dodoma mjini 
Na Abu Zuberi, Dodoma 

Ijue Madrasat Jadidul Fiqhyyat - Tabata Kimanga 
Na B. Mwakangwale 

Madrasat Hidayatul Muumini Mwadui 

Washindi wa mashindano ya Hadithi za Mtume (s.a.w.) wapatikana 

Madrasa Shafii Ujiji Kigoma yaonyesha umahiri wake 

Waanzisha mifuko kusaidia wagonjwa Dodoma 

Waislamu Kondoa waomba msaada kumalizia Msikiti 

Mnyororo wa imani-2 
Na Sheikh Bernard P. Nyangasa 

Kutoka magazeti ya zamani: 
Wanaoshitakiwa kwa uhaini kortini leo 

Jengo la Waislamu Moshi lageuzwa Kanisa la Walokole 
Na Mwandishi Wetu, Moshi 

Masjid Nurania yaswaliwa Ijumaa 
Na Rajab Rajab, Morogoro 

Jabal Hira kutoa mafunzo ya Kompyuta Morogoro 
Rajab Rajab na Mussa Ally, Morogoro 

Sayansi na Teknolojia 
[Internet ni nini?] 

Masomo ya Dini ya Kiislamu 

Barua za Wasomaji 

Mashairi 

Chakula na lishe 
[Thamani ya mlo wa Uyoga] 
 


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita