|
MASHAIRI
Nyoka mleleka
Bismillahi hakika, ninaanza kuandika,
Kwa jina lake Rabbuka, ambae ametukuka,
Naomba zake baraka, kadiri atavyotaka,
Wazee kufuga nyoka, nyoka si wa kufugika.
Wazee twawakumbuka, wengine wametutoka,
Wamekwenda kwa Rabbuka, siku zilipowafika,
Majina sintotamka, huzuni imenishika,
Wazee kufuga nyoka, nyoka si wa kufugika.
Walichofanya hakika, ni wema waliutaka,
Ndipo walipomshika, kuona ahangaika,
Nyoka akakamatika, kawa mwana ‘Mleleka’
Wazee kufuga nyoka, nyoka si wa kufugika.
Ndani wakaja muweka, kwa furaha na kucheka,
Wakatandika mikeka, kumkaribisha nyoka,
Kisha akafukuzwa paka, aondoke kwa haraka,
Wazee kufuga nyoka, nyoka si wa kufugika.
Chakula wakakipika, “Karamu” wakaandika,
Wakamfariji nyoka, mwana asiye na kaka,
Kila alichokitaka, kwake kikakamilika,
Wazee kufuga nyoka, nyoka si wa kufugika.
Nyoka alipozinduka, kwamba “uemi” ataka,
Kisha ameaminika, wazee hawana shaka,
Ndipo alipotamka, Baleghe imeshafika,
Wazee kufuga nyoka, nyoka si wa kufugika.
Wazee bila ya shaka, wala inda kutendeka,
Mambo yakatimizika, na fedha zikachangika,
Ulaya kukaendeka, kafaulu mwana nyoka,
Wazee kufuga nyoka, nyoka si wa kufugika.
Alipovuka mipaka, kuacha Afrika,
Akaomba kwa Rabbuka, ili salama kufika,
Na huko alipofika, mikakati akaweka,
Wazee kufuga nyoka, nyoka si wa kufugika.
Mikakati aloweka, kawambia wahusika,
Kwamba anachokitaka, ni mwitu aliotoka,
Akabidhiwe waraka, atawale Tanga na nyika,
Wazee kufuga nyoka, nyoka si wa kufugika.
Hilo halikupingika, kwa hao wahusika,
Ila walilomtaka, awe wao ‘kibaraka’,
Na ipate enezeka, itikadi ya mashaka,
Wazee kufuga nyoka, nyoka si wa kufugika.
Kakabidhiwa waraka, akarudi kwa haraka,
Kajaza anavyotaka, ndugu zake wa Ki-nyoka,
Msitu akaushika, kadhibiti madaraka,
Wazee kufuga nyoka, nyoka si wa kufugika.
Hatamu aliposhika, sheria zikatungika,
Hakuna wa kutamka, kupinga anavyotaka,
Nyoka wasohesabika, wakazunguka mipaka.
Wazee kufuga nyoka, nyoka si wa kufugika.
Yeyote alohisika, kuhoji mambo ya nyoka,
Ndani kasahaulika, na kifo kikamfika,
\Sumuye haina shaka, inaua kwa haraka,
Wazee kufuga nyoka, nyoka si wa kufugika.
S.M. SAIDI LINZE,
Masjid Nuur,
S.L.P. 116,
MPANDA.
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Maoni yetu: Wananchi kataeni
kupotoshwa
SUALA LA MWEMBECHAI: Wabunge
wataka kujua nani aliamrisha kuua
Na Mwandishi wetu
Katiba ya nchi yapuuzwa: Waislamu
wapigwa marufuku kuhubiri
Mtihani darasa la saba 1998: Manispaa
Moro yaagiza ipewe majina ya wanafunzi Wakatoliki
Na Rajab Rajab, Morogoro
“Wushu”ya Waislamu wa China
na jinsi ilivyowasaidia kupambana na dhulma dhidi yao
Na MUSSA ALLY
Yesu wa kwenye Mathayo siyo Yesu wa
kwenye Luka
Na. Masoud Mohammed
Ni nani hawa Waislamu wa Siasa Kali
?
Na USTADH A.S. FUNDI
Waislamu tuondokane na unyonge
Na Abubakar Marwilo
Maisha ya ndoa kwa Mwislamu
Waislamu wana mwelekeo wao
Na Sheikh Pandukizi Dilunga
Ni mwaka gani Yesu alianza kuitwa
Mungu
Na MCHUNGAJI A.T. MANONI
Wanawake wameamua kuwa wazi
kweli kweli
Na Bi. Fatma Musa
Kimya kingi kina mshindo mkuu:
Vipi Mhe. Rais wale walioua?
Na Mussa Ally
Mtazamo wa madhalimu wa Tanzania
kwa Waislamu
Na Rajab Isa
Aliyoyasema KK bungeni
Waislamu mkoa wa Morogoro
wampinga Yahya
Na. Abu Adli
Polisi wachafua mazingira
ya msikiti wa Mwembechai
Na Badru Kimwaga
Wanawake wa Kiislamu Ubungo
darajani wamuunga mkono Sheikh Bafadhil
Na Kassim Juma
Barua za wasomaji
Mashairi
Mafundisho ya Qur'an: Kanuni
za kumkumbuka Allah na kutumia katika njia yake
Masomo
Chakula na lishe: Lishe ya
mtoto aliyekuwa mgonjwa
Na Mujahiid Mwinyimvua
|