AN-NUUR
Na.158 Rabi' Awal 1419, Julai 17 - 23, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
 Waislamu mkoa wa Morogoro wampinga Yahya

Na. Abu Adli  

KUFUATIA tamko la Bakwata Makao Makuu Dar es Salaam la kumtaka Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Alhaj Omar M. Bafadhil ajiuzulu, Waislamu mkoani humo wametoa tamko la kupinga hatua hiyo. 

Waislamu hao wamesema kutokana na katiba ya Bakwata, Sheikh Omar amechaguliwa kihalali na Waislamu wa mkoa huo hivyo ataendelea na wadhifa wake hadi mwisho wa uhai wake. 

"Sisi sote tunaungana naye kwa khutuba yake aliyoitoa katika mkesha wa Maulidi ya kuadhimisha kuzaliwa mtukufu huko Bagamoyo", wamesema Waislamu wa mkoa huo katika tamko lao. 

Aidha, wamemtaka Sheikh Yahya Hussein aende mkoani humo ili apeleke takwimu ni maendeleo gani Bakwata imewaletea Waislamu hadi sasa. 

"Tunakutaka uje hapa ueleze toka Bakwata liundwe 1968 hadi 1998 kuna maendeleo gani ndani ya Uislamu miaka thelathini?", wamehoji Waislamu hao na kuwaomba Waislamu kote nchini waunge mkono tamko la Sheikh Omar kuwa kuna udhaifu katika Bakwata na ikibidi wafanye maandamano ya amani kwa pamoja kuliunga mkono tamko hilo. 

Tamko hilo pia limedai kuwa Yahya Hussein siyo Bakwata na kwamba yeye ni Balukta na alikuwa mpinzani mkubwa wa Bakwata na sasa anaendeleza uadui wake akiwa ndani ya Baraza hilo. 

Wakati huo huo, Sheikh Omar Bafadhili amesema kwamba hana muda wa kujibizana na Yahya Hussein magazetini kwani kwa kufanya hivyo atakuwa amejivunjia hadhi yake kwa waumini. 

Sheikh Omar aliyasema hayo nyumbani kwake alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hizi mwishoni mwa wiki. 

"Siko tayari kujibizana na Yahya, yeye anafahamu Sheikh na mjumbe wa Kamati ya Maulamaa Taifa wana hadhi na wajibu gani ndani ya Bakwata kulinganisha na watendaji wa kawaida", alisema Sheikh Bafadhil bila kufafanua. 
Juu
  

Polisi wachafua mazingira ya msikiti wa Mwembechai

Na Badru Kimwaga 

POLISI wafanyao doria maeneo ya msikiti wa Mwembechai wamelalamikiwa kwa kuchafua majengo yaliyozunguka msikiti huo. 

Wakitoa malalamiko yao, wakazi wa maeneo ya jirani wamedai kuwa askari hao wanaolinda eneo hilo yapata miezi mitano, tangu kutokea vurugu, huwa wakijisaidia haja ndogo ndani ya majengo ya msikiti huo, yaliyo nyuma ya msikiti, pembezoni mwa banda la kuuza vinywaji liitwalo Uroja wa Kiunguja, na majengo mengine ambayo hayajamalizwa kujengwa. 

Wakiongea kwa kuficha majina yao, wakazi hao wamesema kuwa wamekuwa wakiwashuhudia askari hao wakiwa katika sare zao pamoja na silaha zao, wakigeuza majengo hayo kama. 

Wakazi hao wameongeza kusema kuwa imeonekana mipira ya kiume (kondom) nje ya chumba wanacholalalia kisicho na mlango hali ambayo wamedai kuwa inatia wasiwasi kwamba eneo hilo la ibada huenda limegeuzwa kuwa danguro. 

Lakini baada ya wenye msikiti kuhoji, juzi majira ya jioni, mkuu wa maskari hao, ambaye Mwandishi hakuweza kumtambua akiwa ndani ya Hyundai TZM 3445, aliwasili eneo hilo na tangu siku hiyo, askari hao wameacha kulala katika chumba hicho. 

Haieleweki kama mkuu huyu aliwasili eneo hilo kikazi au alikuwa katika jitihada ya kufuatilia malalamiko hayo. 

Askari hao ambao wako eneo hilo tangu wavamie msikiti wa Mwembechai na kuua watu wanne,wamedaiwa kuwa kero kwa wakazi wa hapo. 

Uvamizi wa polisi Msikiti wa Mwembechai umeathiri sana mipango ya Ibada ikiwa ni pamoja na kupungua kwa idadi ya waumini. 
Juu

 
Wanawake wa Kiislamu Ubungo darajani wamuunga mkono Sheikh Bafadhil

Na Kassim Juma 

WANAWAKE Waislamu wa Msikiti wa Ubungo Darajani Jijini wameunga mkono hotuba ya Sheikh Bafadhil aliyoitoa mjini Bagamoyo hivi karibuni. 

Wakizungumza kwa niaba ya wenzao, wanawake sita ambao walifika katika ofisi ya gazeti hili Mtaa wa Mahiwa Kariakoo Jijini mwishoni wa wiki iliyopita, wamesema Sheikh Omar ni mfano wa kuigwa na masheikh wengine nchini. 

"Sisi wanawake wa Msikiti wa Ubungo tunamuunga mkono Sheikh Omar Bafadhil kwa sababu amezungumza mambo ya msingi kwa Waislamu", walisema kwa pamoja akina mama hao. 

Aidha walishutumu kauli ya Sheikh Yahya Hussein iliyomtaka Sheikh Bafadhil kujiuzulu kwa madai ya kuiumbua Bakwata hadharani. 

Hotuba ya Sheikh Omar katika mkesha wa Maulid mjini Bagamoyo, imeibua mijadala miongoni mwa Waislamu sehemu mbali mbali nchini. 

Katika hotuba yake hiyo pamoja na mengine aliyoyazungumza, Sheikh Omar aliitaka Bakwata kubadili mwenendo ilionao sasa wa kuwa mbali na Waislamu badala yake iwe mtetezi na msemaji wa haki za Waislamu nchini. 
 

Juu 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI  

Maoni yetu: Wananchi kataeni kupotoshwa 

SUALA LA MWEMBECHAI: Wabunge wataka kujua nani aliamrisha kuua 
Na Mwandishi wetu  

Katiba ya nchi yapuuzwa: Waislamu wapigwa marufuku kuhubiri  

Mtihani darasa la saba 1998: Manispaa Moro yaagiza ipewe majina ya wanafunzi Wakatoliki 
Na Rajab Rajab, Morogoro 

 “Wushu”ya Waislamu wa China na jinsi ilivyowasaidia kupambana na dhulma dhidi yao 
Na MUSSA ALLY  

Yesu wa kwenye Mathayo siyo Yesu wa kwenye Luka 
Na. Masoud Mohammed 

Ni nani hawa Waislamu wa Siasa Kali ? 
Na USTADH  A.S. FUNDI  

Waislamu tuondokane na unyonge 
Na Abubakar Marwilo 

Maisha ya ndoa kwa Mwislamu 

Waislamu wana mwelekeo wao 
Na Sheikh Pandukizi Dilunga 

Ni mwaka gani Yesu alianza kuitwa Mungu 
Na MCHUNGAJI A.T. MANONI  

Wanawake wameamua kuwa wazi kweli kweli 
Na Bi. Fatma Musa 

Kimya kingi kina mshindo mkuu: Vipi Mhe. Rais wale walioua? 
Na Mussa Ally 

Mtazamo wa madhalimu wa Tanzania kwa Waislamu 
Na Rajab Isa 

Aliyoyasema KK bungeni 

Waislamu mkoa wa Morogoro wampinga Yahya 
Na. Abu Adli  

Polisi wachafua mazingira ya msikiti wa Mwembechai 
Na Badru Kimwaga 

Wanawake wa Kiislamu Ubungo darajani wamuunga mkono Sheikh Bafadhil 
Na Kassim Juma 

Barua za wasomaji  

Mashairi  

Mafundisho ya Qur'an: Kanuni za kumkumbuka Allah na kutumia katika njia yake 

Masomo  

Chakula na lishe: Lishe ya mtoto aliyekuwa mgonjwa 
Na Mujahiid Mwinyimvua 
 
 

 

 

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita