|
|
WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania wameitaka serikali ieleze ni nani alitoa amri ya kuuliwa wananchi pale Mwembechai. Aidha wabunge hao wanahoji ni hatua gani zimeshachukuliwa dhidi ya Polisi walioua na ni kwa nini serikali inakuwa na tabia ya ubalakala katika utendaji wake. Pamoja na hoja hizo wabunge wametaka ufafanuzi juu ya suala la kashfa na kusisitiza umuhimu wa serikali kuunda Tume ya uchunguzi juu ya Mauaji ya Mwembechai kwani mpaka sasa serikali haina maelezo yenye kueleweka. Akizungumza bungeni juzi Mbunge wa Konde, Mhe. Salim Ahmed Said alisema kwamba kwa taratibu za jeshi la polisi, polisi hawezi kufanya jambo bila ya amri, hivyo akataka kujua ni nani alitoa amri ya kuua pale Mwembechai, ni OCD, RPC, Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, IGP au Waziri? Katika kuonyesha jinsi gani haki isivyotendeka na kuwepo kwa uonevu na ubalakala Mhe. Salim alihoji na kushangaa kwamba ni vipi mbwa aliyeuliwa kule Sumbawanga alitetewa mpaka na Jaji hili la mauaji ya Waislamu linyamaziwe. Mheshimiwa Hashul Nassor Ali ambaye ni Msemaji wa Upinzani Wizara ya Mambo ya Ndani akilizungumzia suala hili alisema kwamba limelitia doa jeshi la polisi na kwamba imejenga chuki baina ya polisi na wananchi. Alisema kila aliyeangalia televisheni alishuhudia Afisa wa polisi akiamrisha "Piga yule na yule". Aidha alisema watu walishuhudia kwamba kijana yule aliyeuliwa na polisi alipoanguka alikuwa na jiwe dogo mkononi. "Ile ilikuwa ni ‘Cold Blood Murder’ ilifanywa makusudi na polisi", alisema Mhe. Hashul. Kuonyesha ubalakala (double standard) wa serikali alioanisha na pengine chuki yake dhidi ya Waislamu Mhe. Hashul alioanisha tukio hili la Mwembechai ambapo serikali imeua kwa madai ya kuzuia ghasia na polisi kuzidiwa nguvu na lile la Arumeru ambapo wananchi wa huko wapatao 5000 wakiwa na sime na mikuki walikabiliana na polisi, na haikutolewa amri ya piga yule. Sambamba na hilo Mhe. Hashul Nassor Ali alihoji juu ya suala la kashfa za kidini. Alisema Muislamu kusema Yesu sio Mtoto wa Mungu ndivyo hasa Qur’an yake inavyosema. Lakini akasema wapo wale Morani wa Arumeru wao wanasema kwamba kwaya na mahubiri ya Kanisa ni kelele zinazowanyima usingizi, na ni laana kwa mujibu wa mila zao. Na wamechukua hatua ya kuchoma moto makanisa, ili kuthibitisha kukerwa kwao. "Pale Mwembechai piga yule kwa risasi ilitekelezwa", lakini Arumeru polisi waliwakimbia wananchi waliochoma makanisa. Katika kusisitiza umuhimu wa kuundwa kwa Tume ya uchunguzi Mhe. Hashul alisema kwamba kwa mara ya kwanza Mhe. Waziri wa Mambo ya Ndani alisema vyama vya upinzani vinahusika. Baadaye nchi fulani za kigeni na baadaye mujahidina. Kwanza Mhe. Hashul alitaka kujua hawa Mujahidina ndio nani. Lakini katika hotuba ya Waziri wa Mambo ya Ndani Bungeni Mhe. Hashul amesema kwamba sasa inasemwa kwamba ni vyama vya kidini vilivyoandikishwa kwa nia njema. Ni kutokana na kujikanganya huko Wabunge wamesema kwamba ni muhimu uchunguzi ufanyike. Mbunge wa Kigamboni Mhe. Kitwana Kondo, amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani akafanye uchunguzi aje na kauli thabiti. Pamoja na nukta hiyo Mhe. Kondo alitaka kujua wale askari walioua wamechukuliwa hatua gani. Aidha Mhe. Kitwana Kondo alimhoji Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi juu ya askari wanaolinda msikiti wa Mwembechai hivi sasa. Hali ambayo amesema imesababisha msikiti kutokuswaliwa na darasa mbali mbali zilizokuwa zikiendeshwa msikitini hapo kusita. Zaidi ya hayo Mhe. Kitwana Kondo alionyesha masikitiko yake dhidi ya hatua ya Polisi kuwakamata wazee watu wazima –Mzee Chata na Mzee Katambo na kusema kwamba wanaofanya matendo haya ndio wasioitakia nchi yetu mema na wala sio yeye anayeiambia kweli serikali yake na viongozi wake. Na katika kuisherehesha nukta hiyo Mhe. Kondo akamhoji Mhe. Waziri wa Mambo ya Ndani kwamba, je!, haioni hatari mbaya ingetokea au wazee wale wangefia jela? Kuhusu suala la "Parole" Mhe.Kitwana Kondo ameshangaa ni kwanini Mhe. Ali Ameir anachukua muda mrefu kuiunda (kupata watu wa upande mwingine). Katika hilo akamshauri aige mfano wa Mtume Mussa (a.s.). Kwamba alipopewa utume aliomba apewe msaidizi kutokana na kuwa na kigugumizi. Na Mwenyezi Mungu akampa Haruni (a.s.). Sasa na yeye kama hawaoni wasomi Waislamu arudi kwa Rais aombe msaada atapewa akina Harun wanao wajua. Akichangia hoja hiyo ya Wizara ya Mambo ya Ndani Mbunge wa Magu,Mhe. John Cheyo alisema kwamba kinachogomba katika suala la Mwembechai na mengine ni matumizi ya nguvu yaliyokithiri na kusema kwamba hakuna amani bali ni uvumilivu wa wananchi na zaidi kwamba watu wanaogopa. Wabunge wengi waliochangia hoja hiyo wametahadharisha juu ya matendo ya askari yanayokiuka sheria kama vile kufanya upekuzi usiku, kuwatesa na kuwaua raia. Walisema hali hiyo inajenga uhasama na uadui baina ya polisi na raia. Awali katika hotuba yake Mhe. Waziri wa Mambo ya Ndani alisema kwamba suala la Mwembechai limesababishwa na vikundi vya kidini ambavyo vingine vimesajiliwa kisheria lakini vimejihusisha na mahubiri ya kashfa na chuki baina ya dhehebu moja na jingine au baina ya dini moja na nyingine. Na katika kujibu hoja za Wabunge Mhe. Waziri akasema kwamba hakuna haja ya Tume kwani kila kitu kinajulikana; kwamba kulikuwa na vurugu. Hata hivyo kuhusu vifo akasema kwamba bado majalada yanafanyiwa uchunguzi na Wizara ya sheria.
|
TAHARIRI Maoni yetu: Wananchi kataeni kupotoshwa SUALA LA MWEMBECHAI: Wabunge
wataka kujua nani aliamrisha kuua
Katiba ya nchi yapuuzwa: Waislamu wapigwa marufuku kuhubiri Mtihani darasa la saba 1998: Manispaa
Moro yaagiza ipewe majina ya wanafunzi Wakatoliki
“Wushu”ya Waislamu wa China
na jinsi ilivyowasaidia kupambana na dhulma dhidi yao
Yesu wa kwenye Mathayo siyo Yesu wa
kwenye Luka
Ni nani hawa Waislamu wa Siasa Kali
?
Waislamu tuondokane na unyonge
Waislamu wana mwelekeo wao
Ni mwaka gani Yesu alianza kuitwa
Mungu
Wanawake wameamua kuwa wazi
kweli kweli
Kimya kingi kina mshindo mkuu:
Vipi Mhe. Rais wale walioua?
Mtazamo wa madhalimu wa Tanzania
kwa Waislamu
Waislamu mkoa wa Morogoro
wampinga Yahya
Polisi wachafua mazingira
ya msikiti wa Mwembechai
Wanawake wa Kiislamu Ubungo
darajani wamuunga mkono Sheikh Bafadhil
Mafundisho ya Qur'an: Kanuni za kumkumbuka Allah na kutumia katika njia yake Chakula na lishe: Lishe ya
mtoto aliyekuwa mgonjwa
|