AN-NUUR
Na.158 Rabi' Awal 1419, Julai 17 - 23, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Maisha ya ndoa kwa Mwislamu
 

KWA kawaida yangu mimi, hupendelea zaidi kusoma kurasa za Makala katika magazeti kuliko habari nyinginezo, kutarajia kupata mawazo mbali mbali ya wapenzi wenzangu juu ya maisha kwa jumla. Kwa bahati niliposoma makala ya Bi- Zahra Tajiri kwenye toleo la AN-NUUR la Mei 22-28,1998 (Muharram – 1419); yalinipa changamoto ya kutoa mawazo yangu kwa mara ya kwanza. Si juu ya "uke wenza’ tu, bali kuhusu maisha ya ndoa za Waislamu kwa jumla. 

KAMA tujuavyo Waislamu kuwa, Mtume (s.a.w.), hakuondolewa ulimwenguni mpaka amekamilisha kazi aliyopewa na Allah (s.w.t.) ya kuwaongoza walimwengu wote kwenye mfumo sahihi wa maisha yao hapa duniani. Natusome: "………Leo nimekukamilishieni dini yenu, na kukutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe dini yenu….." (5:3) 

Kukamilika kwa dini ya Uslamu, ni pamoja na kuwepo utaratibu madhubuti wa maisha ya ummah, ambayo mwanzo wake ni katika ndoa. Mtume mwema Muhammad (s.a.w.) ameweka utaratibu huo, kwa vitendo, yeye akiwa ni ruwaza njema – si katika ndoa ya mke mmoja tu, bali hata katika ndoa ya mitala – na akasema: 

"Mbora kwenu ni yule aliye mbora kwa familia yake, na mimi ndiye mbora kwenu kwa familia yangu; hajawakirimu wanawake ila mkarimu, na hawadhalilishi wanawake ila bakhili – Mchungu:. (ibnu Assalif) 

Hivyo Waislamu hawatakuwa na nguvu ya hoja ya kujitetea siku ya hukumu mbele ya Allah (s.w.t.) atakapompa haki kila aliyedhulumiwa duniani. Maana Allah (s.w.t.) amewatuma M