AN-NUUR
Na.158 Rabi' Awal 1419, Julai 17 - 23, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
 Chakula na lishe

Lishe ya mtoto aliyekuwa mgonjwa 

Na Mujahiid Mwinyimvua 

WAKATI mtoto (au mtu mzima) anaugua, mwili wake unapoteza viinirishe vingi, kwa mfano vitamini A na madini ya chuma. 

Vitamini A inasaidia kuupa mwili kinga na pia inasaidia macho kuona vizuri. Madini ya chuma yanatumika mwilini kutengeneza damu. 

Kutokana na kupotea kwa viinirishe (virutubisho) mwilini, mtoto (au mtu mzima) aliyetoka katika ugonjwa, huwa na njaa kuliko ilivyo kawaida. Kwahiyo, huwa anakula sana na kukua kwa haraka kuliko ilivyo kawaida mpaka mwili wake utakaporudia hali yake ya kawaida, vile ulivyo. 

Kipindi hiki kwa kimombo kinaitwa ‘catch –up growth’ kwa lugha yetu ya Kiswahili tunaweza kukiita kipindi cha kufidia makuzi yaliyoathiriwa kwa sababu kadhaa, mojawapo ni maradhi. 

Kipindi hiki cha kufidia makuzi pia hupatikana kwa watoto waliokuwa na minyoo. Kwa maneno mengine, watoto wenye minyoo, huwa wanamahitaji makubwa ya chakula hasa baada ya minyoo aliyokuwa nayo kuuliwa kwa dawa. 

Baadhi ya wazazi hukasirika kuwaona watoto wao wanakula zaidi kuliko ilivyo kawaida hasa wanapotoka katika maradhi. Tabia kama hii si nzuri, hivyo basi nawaomba wazazi wenzangu wawape chakula kizuri, safi, salama na cha kutosha watoto (au watu wazima) waliotoka katika maradhi. 

Hii ni kwa sababu watoto waliokuwa wagonjwa wasipopatiwa mlo wa kutosha, miili yao haitaweza kufidia kwa haraka virutubisho vilivyoharibika au vilivyopea. Hali hiyo inaweza kuchangia ugonjwa kurudi au mwili wa aliyekuwa mgonjwa kuzidi kuwa dhaifu na kuathiri ukuaji wa mtoto kwa ujumla. 

Watoto waliotoka katika maradhi ambao bado wananyonya, wanyonyeshwe maziwa ya mama mara nyingi, hata zaidi ya mara kumi na tano katika kipindi cha saa 24. Watoto hao kama wana umri zaidi ya miezi minne waongezewe chakula kinachostahiki kwa umri wao. Somo hili tulishalizungumza katika makala zetu zilizopita. 

Watoto au watu wazima waliokuwa wagonjwa wapewe vyakula mchanganyiko (wanga, protini,vitamini, maji, madini, nyuzi nyuzi, n.k.). 

Pia lazima wapewe vyakula vyenye sifa maalumu ya kujenga na kulinda mwili. Vyakula hivyo ni kama vile nyama, samaki, maziwa, maini, mayai, embe, mafuta, siagi (margarine) mboga za majani, nanasi, uyoga, n.k. 

Hata hivyo, ni vyema ikakumbukwa kuwa, vyakula vilivyotajwa hapo juu vina kanuni yake. Kwa mfano, ni hatari kwa afya kuweka mafuta au siagi nyingi katika chakula. Mafuta yanayotokana na mimea ni salama zaidi kwa afya kuliko yale yanayotokana na wanyama. 

Kanuni nyingine ya vyakula ni kuwa mayai si chakula kizuri kwa watoto wadogo (chini ya miaka miwili) kwa sababu yana mafuta ya hatari "cholesterol", hivyo basi mtoto mdogo apatiwe vyakula vingine vyenye protini kwa wingi kama vile maziwa, maini n.k. 
 

Juu 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI  

Maoni yetu: Wananchi kataeni kupotoshwa 

SUALA LA MWEMBECHAI: Wabunge wataka kujua nani aliamrisha kuua 
Na Mwandishi wetu  

Katiba ya nchi yapuuzwa: Waislamu wapigwa marufuku kuhubiri  

Mtihani darasa la saba 1998: Manispaa Moro yaagiza ipewe majina ya wanafunzi Wakatoliki 
Na Rajab Rajab, Morogoro 

 “Wushu”ya Waislamu wa China na jinsi ilivyowasaidia kupambana na dhulma dhidi yao 
Na MUSSA ALLY  

Yesu wa kwenye Mathayo siyo Yesu wa kwenye Luka 
Na. Masoud Mohammed 

Ni nani hawa Waislamu wa Siasa Kali ? 
Na USTADH  A.S. FUNDI  

Waislamu tuondokane na unyonge 
Na Abubakar Marwilo 

Maisha ya ndoa kwa Mwislamu 

Waislamu wana mwelekeo wao 
Na Sheikh Pandukizi Dilunga 

Ni mwaka gani Yesu alianza kuitwa Mungu 
Na MCHUNGAJI A.T. MANONI  

Wanawake wameamua kuwa wazi kweli kweli 
Na Bi. Fatma Musa 

Kimya kingi kina mshindo mkuu: Vipi Mhe. Rais wale walioua? 
Na Mussa Ally 

Mtazamo wa madhalimu wa Tanzania kwa Waislamu 
Na Rajab Isa 

Aliyoyasema KK bungeni 

Waislamu mkoa wa Morogoro wampinga Yahya 
Na. Abu Adli  

Polisi wachafua mazingira ya msikiti wa Mwembechai 
Na Badru Kimwaga 

Wanawake wa Kiislamu Ubungo darajani wamuunga mkono Sheikh Bafadhil 
Na Kassim Juma 

Barua za wasomaji  

Mashairi  

Mafundisho ya Qur'an: Kanuni za kumkumbuka Allah na kutumia katika njia yake 

Masomo  

Chakula na lishe: Lishe ya mtoto aliyekuwa mgonjwa 
Na Mujahiid Mwinyimvua 
  

 

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita