NASAHA
Na. 060 Jumatano  Agosti 9 - 15, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
Lishe

Ulaji wa matunda

Na Mariamu M. Mbwambo

MATUNDA ni mojawapo katika vihitajio muhimu sana katika kulinda mwili wa binadamu. Ingawa watu wengi ulaji wao wa matunda ni wa nadra kwa kutokufahamu umuhimu na faida zinazopatika kwenye matunda.

Natuone basi baadhi ya faida na matumizi ya matunda.

Matunda kwa ujumla hutupatia proteni kwa kujenga mwili, mafuta kwa ajili ya kuupa nguvu mwili,mafuta hupatikana kwa wingi kwenye maparachichi, tunapata wanga katika muundo wa sukari. Pia vitamini C ambayo ipo katika kiwango kikubwa sana.

Vile vile matunda yana madini kama "kalsiam" madini ya chuma, asidi ya matunda ambayo hupatikana zaidi kwenye "citrus fruits" kama malimao, machungwa n.k. Maji yaliyomo kwenye matunda ni kama asilimia themanini na tano .

Matunda yanafaa yaliwe yakiwa yameoshwa na katika hali ya kuvutia, yasiwe yenye madoadoa na yenye kuonyesha kukaa zaidi ya kufikia kupoteza virutubisho muhimu vihitajikavyo mwilini. Pia ni vizuri matunda kuliwa/kuchaguliwa unaponunua yakiwa yameiva,kwani matunda mabichi huwa magumu kuyeyushwa kwa urahisi tumboni (DIGESTIoN) kutokana na asidi iliyomo humo. Pia ni vizuri matunda yakatumiwa yakiwa kwenye msimu na yahifadhiwe vizuri yasiharibike.

Baadhi ya matunda yanaweza kupikwa na kutumwika kama chakula,mfano wa hayo ni ndizi mbichi, hii husaidia kulainisha matunda hayo ili yaweze kusagwa kwa urahisi tumboni.

Pia matunda yanapopikwa husaidia kuyahifadhi na kukaa kwa muda mrefu, vilevile bakteria waliomo kwenye matunda hayo hufa.

Matunda mengine huliwa yakiwa yamemenyewa au na maganda yake. Haya ni kama maembe, ndizi, machungwa,tikiti maji, papai na mananasi, kwa lugha ya kigeni matunda haya yanajulika kama (SERVING FRUITS).

Matunda yana kazi kubwa katika kuilinda miili yetu isipatwe na magonjwa.Hivyo basi matumizi haya hutegemea sana asili ya tunda hilo, mfano ndizi itakapochanganywa na unga wa ngano na kutengenezwa mkate itatumika kama kitafunwa yaani (SNACK) na inaweza kutumika kutengeneza juisi itakapochanganywa na maziwa.

Pamoja na hayo kuna baadhi ya matunda huweza kutengenezewa supu mfano nyanya, jhamp, vinywaji kama juisi, viungio vya mboga kama limao, pia matunda huweza kuchanganywa pamoja katika vipande vyembamba na vidogo vidogo kama salad.

Hivyo basi tunashauriwa kutumia matunda ipasavyo hasa kwa watoto, watu wazima pamoja na watu wote kwa ujumla ili kuchangamsha mfumo mzima wa neva,vilevile kuilinda miili yetu na magonjwa.

Juu
 

YALIYOMO
 

KAULI YA WAISLAMU
BAKWATA na Kanisa

Karume adaiwa ‘kutafuta ujiko’ kwa kutofautiana na Mkapa

Mkapa akiuka sera yake-Chuo Kikuu

Uandikishaji wapiga kura waanza

NLD, NRA, PONA vyamruka Mrema

CUF  yataja wagombea wake Temeke

CCM yamtuhumu Mwenyekiti wake pandikizi

Propaganda ya Udini itaisambaratisha nchi - CHADEMA

USHAURI NASAHA
Kumsaidia mtoto aweze kujitegemea

MAKALA
Lengo la propaganda

MIPASHO NASAHA
NJOZI! NJOZI!

MAKALA
Tujihadhari na risasi za sukari

KALAMU YA MWANDISHI
Popo Bawa la kisiasa

Je, unajua haki yako unapokamatwa na polisi?

Habari za Kimataifa

LISHE
Ulaji wa matunda

MASHAIRI

MICHEZO

  • Baada ya kuitumia kuigaragaza Simba: Shungu akiri ‘ngangari' ni kiboko
  • Manga azikwa Moro
  • •••Dewji ahusishwa na kifo cha mnyama Simba
  • Lunyamila, Kayoza waongoza kwa mabao

  •  


    Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita