|
Na. 060 Jumatano Agosti 9 - 15, 2000 |
|
|
|
|
|
NJOZI! NJOZI!
Na Abu Halima Sa Changwa
NJOZI! Njozi! Hilo sasa limekuwa midomoni mwa watu. Hapo mwanzo ilikuwa macho huku na kule, "Ponda! Ponda!" Hiyo ilitokea baada ya Ponda kuponda hoja za Mkuu fulani kwenye vyombo vya habari, zinazo husiana na ukweli kuhusu "Mwembechai Killings", Khe, wasiomjua Ponda wakamjua. Wengi wakasema, huyo ndo mwenyekiti wao. Tumekwendaaaa, ikaja nyingine" "Mbukuzi! Mbukuzi!"Hii nayo ilitokea baada ya Mbukuzi kubukua masuala yanayohusishwa na "Mwembechai Killings". Naye hivyo hivyo akayasemea. Ikawa "Mkamateni, mswekeni lupango". Khe, Mbukuzi naye watu wakamjua mno. Sasa naye aitwa Amiri wa Shura ya Maimamu. Katika kitabu cha "The Trial of Deadan Kimathi" (Hukumu ya Dedan Kimathi), kilochoandikwa na mwanafasihi maarufu wa Kenya, Ngugi wa Thiong'o, akishirikiana na Githae Mugo, yupo mwanamke aliyekuwa akiwasimulia vijana wawili machokora, mmoja wa kiume na mwingine wa kike, kuhusu huyo Deadan Kimathi, askari mwanamapinduzi, kiongozi wa Mau Mau, ambaye wakoloni walimchukulia kama mhalifu, mchochezi anaehatarisha amani na utulivu wa wakoloni. Yule mwanamke alisema: "There are people, my child,with blessed blood.And when something happens to them,the wind and the rain and the sun will tell. Even hyenas.Their death can shake mountains and give life to the volcanoes long thought to be dormant." (Uk.211). Tafsiri: Kuna watu,mwanangu wenye damu iliyobarikiwa. Na jambo lolote linapowatokea, upepo na mvua na jua vyote vitasema. Hata mafisi. Vifo vyao vinaweza kutingisha milima na kuzipa uhai volkano ambazo siku nyingi zilidhaniwa kuwa zimekufa). Haya. Asojua maana hambiwi maana! Historia inatuonyesha kwamba wewe unaweza kumfanya mtu kuwa mbaya, adui, jangili, gaidi, kumbe nyuma yake kuna kundi la watu wanaomfanya kuwa kipenzi. Na ukitaka kujitafuatia maadui, basi mfanye huyo kuwa adui. Wakoloni walipomfanya Dedan Kimathi kuwa adui, walijikuta wamejiongezea maadui zaidi. Na suala alilolisimamia Dedan Kimathi, liliwahusu wananchi wengi. Hakujifanyia mwenyewe. Kwa nini awe tayari kuteswa, au kufa kwa ajili ya kuwasimamia watu wengine? Kwa nini Kimathi aliamua kuishi msituni, na mafisi, majoka na hatari nyingine zote?Je yeye hakutaka kulala nyumbani? Na je,ni kweli wakoloni walikuwa hawajui kwamba wao wanawafanyia Waafrika unyama? Hata kama walimwita Kimathi mwehu,je,ni kweli alikuwa mwehu? Tunarudi hapa. Huu ni wakati wa ukweli na uwazi. Na siku zote tunasisitiza: "UKWELI NA...." "UKWELI NA...". Sasa, Huyu Ponda, ni kweli ni Mwehu tu? Lakini hata kama ukweli na uwazi wetu unatutuma tuamini kwamba ni mwehu,je mwehu huhukumiwa? Au hutafutwa akifanya uhalifu? Halafu, mwehu na "Mwembechai Killings" wapi na wapi! Haya. Mbukuzi naye je? Ni kweli ni msema hovyo, kama baadhi ya magazeti yalivyomripoti? Anaposema haki haitendeki anasema hovyo au anasema kitu ambacho ni cha kusikilizwa na kuangaliwa kwa makini, kwa vile huu ni wakati wa "UKWELI NA...."? Mimi ninavyoona, isijekuwa tuko kwenye NJOZI ya kulizima suala la Mwembechai. Ni suala ambalo linaweza likatuponda nakutubukua, tusipoangalia. Leo nimeamua kuwa siriazi kidogo na kuacha utani utani kwenye mpasho. Kama tuna mikakati yakulifanya suala la "Mwembechai Killings" lisahauliwe hivi hivi tu, na hali lina UKWELI kwa sababu lilitokea (sio fiction), na lina UWAZI kwa sababu hakuna Mbongo ambaye halijui, na limo kwenye mkanda mzima wa video. Na watu wanazo hizo kanda nyumbani kama ambavyo wana kanda za Sarafina na Rambo. Kama tulikuwa tunadhani kwamba "Mwembechai Killings"ni issue ya kusahaulika,basi sasa tujue kwamba tumo kwenye NJOZI. Hata tukipiga marufuku kitabu kinachoelezea yaliyotokea, bado tutakuwa tu ndani ya NJOZI. Baada ya"Ponda! Ponda!" "Mbukuzi! Mbukuzi!" Sasa imekuwa "NJOZI! NJOZI!". Halafu ....teh! ....teh! ....teh! Wachanicheke ki....kidogo kwa.....kwanza.Hivi wakati huu wa sayansi na tekonolojia,na makompyuta na vikokotoo,na maintaneti,na maluninga na televisheni zake pamoja na video, ni wakati wa kupiga mafuruku....Ai mimi....marufuku nanino....kitabu? Hata! Tumbo kwenye NJOZI! NJOZI! |
YALIYOMO
KAULI
YA WAISLAMU
Karume adaiwa ‘kutafuta ujiko’ kwa kutofautiana na Mkapa Mkapa akiuka sera yake-Chuo Kikuu Uandikishaji wapiga kura waanza CUF yataja wagombea wake Temeke CCM yamtuhumu Mwenyekiti wake pandikizi Propaganda ya Udini itaisambaratisha nchi - CHADEMA USHAURI NASAHA
MAKALA
MIPASHO NASAHA
MAKALA
KALAMU YA MWANDISHI
Je, unajua haki yako unapokamatwa na polisi? LISHE
|
|
|
|
|