NASAHA
Na. 060 Jumatano  Agosti 9 - 15, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
MAKALA
 
 

Tujihadhari na risasi za sukari

Na Mfukamanga

PENGINE wasomaji watastushwa na kichwa cha habari, RISASI ZA SUKARI, lakini risasi ni risasi tu, zote ni mbaya na zote zinaua. Ila zinatofautiana kwa namna zinavyoua.

Kuna risasi za moto na risasi za sukari. Watu wengi wanagongwa risasi za moto na kufa hapo hapo.

Wanakufa wakiwa na misimamo yao thabiti. Risasi za sukari ambazo ndizo kiini cha makala hii huua kwa namna ya ajabu sana. Huua mtu kwa zaidi ya mara mbili.

Katika makala hii napenda nizumgumzie vifo vitokanavyo na risasi za moto na za sukari kwa watu ambao ni waumini. Wale wanaomtambua Mola wao mmoja tu. Na hivyo wakaishi kulingana na imani hiyo.

Hivi sasa kuna tatizo kubwa la risasi za sukari. Kuua kwake kwa mwanzoni ni kumbadilisha muumini awe kafiri yaani atoke katika uumini au awe mnafiki yaani awe huku na huko (muumini wa dini zaidi ya moja). Muumini utaacha wajibu wako unaokupasa na kujiunga na vilabu visivyo na manufaa kupigia debe vyama vyama dhalimu wanaodhulumu jamii.

Kama muumini alikuwa na wadhifa fulani kama vile Imamu wa msikiti basi kazi yake itakuwa ni kuwagawa waumini katika makundi ili wasiwe na umoja. Kama ulikuwa na wadhifa serikalini basi kazi yako itakuwa kuwasema vibaya

Waislamu kwa kuwalaumu na kuwatukana kwanza hawawezi kuongoza nchi na wako nyuma kielimu kwa uzembe katika mikutano yao.

Risasi za sukari ni neno la kisaikolojia ambazo zinaweza kujitokeza katika hali zifuatazo:- Kwanza ni kwa kukaa meza moja na maadui wa

Allah (s.w.) -watu wanaoupiga vita Uislamu. Kukaa nao meza moja ni kwa maana pana ikiwa ni pamoja na kula au kunywa nao vyakula na vinywaji kwa madai kuwa ni kodi zetu, kupeana mikono (shake hands), kupiga nao picha, mikutano ya mara kwa mara na wao n.k. Mojawapo kati ya hayo likishafanyika basi hapo risasi ya sukari imeshafika mwilini na itakusababishia kigugumizi cha kutoibainisha haki na kuichukia. Utakifumbia macho kile ambacho wenzako wamekutuma au wanakipigania.

Pili ni kwa kuahidiwa na ukahadaika kwamba fanya hivi au vile kisha tutakufaa kwa hili au lile.

Yaani utafunguliwa 'account' benki, au utapewa nyumba Msasani ama kununuliwa gari. Hapa mtu atatangaza kujitoa kwenye vyama vya haki vya wanyonge kama 'East African Muslim Welfare Society' au ukahamasisha kuipa kura za ndiyo Chama Cha kuleta Maumivu. Hapa risasi ya sukari imeshaingia na utakuwa mtu wa maneno mengi matamu lakini si ya kumjua Allah.

Wakati mwingine risasi yasukari huja kwa njia ya ajira. Unapata ajira hewa ya kukufitinisha na wenzako na kuingizwa kwenye 'payroll'. Hapa utawalazimisha 'Waumini waswali Idi moja ya Kitaifa badala ya ile ya kimataifa.

Mwisho yule ambaye ataziepuka risasi hizo za sukari huyo sasa ndiye hukabiliwa na risasi za moto. Huyu ndiye mja wa Allah. Wakati wa kufa huonyeshwa hali halisi ya kule anakoelekea peponi. La kheri zaidi na kilele cha yote ni kule kuwa shahidi wa Allah utakayeshuhudia udhalimu uliofanywa na maadui wa Allah (s.w.).

Juu
 

YALIYOMO
 

KAULI YA WAISLAMU
BAKWATA na Kanisa

Karume adaiwa ‘kutafuta ujiko’ kwa kutofautiana na Mkapa

Mkapa akiuka sera yake-Chuo Kikuu

Uandikishaji wapiga kura waanza

NLD, NRA, PONA vyamruka Mrema

CUF  yataja wagombea wake Temeke

CCM yamtuhumu Mwenyekiti wake pandikizi

Propaganda ya Udini itaisambaratisha nchi - CHADEMA

USHAURI NASAHA
Kumsaidia mtoto aweze kujitegemea

MAKALA
Lengo la propaganda

MIPASHO NASAHA
NJOZI! NJOZI!

MAKALA
Tujihadhari na risasi za sukari

KALAMU YA MWANDISHI
Popo Bawa la kisiasa

Je, unajua haki yako unapokamatwa na polisi?

Habari za Kimataifa

LISHE
Ulaji wa matunda

MASHAIRI

MICHEZO

  • Baada ya kuitumia kuigaragaza Simba: Shungu akiri ‘ngangari' ni kiboko
  • Manga azikwa Moro
  • •••Dewji ahusishwa na kifo cha mnyama Simba
  • Lunyamila, Kayoza waongoza kwa mabao

  •  


    Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita