|
Na. 060 Jumatano Agosti 9 - 15, 2000 |
|
|
|
|
|
BAKWATA na Kanisa AGOSTI 5, mwaka huu watu wa BAKWATA na Makanisa ya Kikristo nchini walitangaza umoja wao. Miongoni mwa watu wa BAKWATA waliokuwepo katika sherehe hizo zilizofanyika Dodoma ni Sheikh Mkuu wao Hemedi Juma na aliyewahi kuwa Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Bw. Ali Hassan Mwinyi. Kwa mujibu wa matangazo yao, madhumuni ya umoja huo wa BAKWATA na Wakristo ni kusuluhisha migogoro yao, kuweka upendo na mshikamano miongoni mwao. Katika hafla ya uzinduzi wa umoja huo, Mwinyi alisema kwamba yeye kama Muislamu kwa kuujua ubaya wa vita vya kidini asingependa kuona vita hivyo vinakuja Tanzania ambako kuna 'amani'. Aidha, kwa kauli iliyoashiria kushangilia umoja huo, Mwinyi alisema Wakristo na Waislamu ni kitu kimoja. Kwa vile hakuna Muislamu yeyote miongoni mwa Wasilamu zaidi milioni 15 wa nchi hii asiyefahamu kuwa BAKWATA si chama cha kuwawakilisha Waislamu, basi tunaamini jambo hili halitawashughulisha. BAKWATA inaujua ukweli huu, Mwinyi naye hivi sasa anaujua ukweli huu pia. Lakini mwenendo huu wa BAKWATA na washirika wake wa kung'ang'ania kutaka waonekane kuwa wanawawakilisha Waislamu nchini ndio utakaozusha balaa na zahama katika nchi hii. Wakati Waislamu nchi nzima wamehuzunishwa kwa kupuuzwa madai yao ya kutaka haki itendeke dhidi ya wale waliomwaga damu ya ndugu zao Waislamu Mbwembechai mwaka 1998, msimamo wa BAKWATA umekuwa sawa sawa na ule wa viongozi wa Kanisa, waliotajwa kuchochea chanzo na kuyashangilia mauji yale. Miaka kumi iliyopita kauli hiyo aliyosema Mwinyi ingesameheka, kwa kuwa alionesha kutoijua BAKWATA. Mwaka 1991 aliwaambia BAKWATA kama wao ni chombo cha Waislamu hawana budi kuwasikiliza na kutenda wayatakayo Waislamu. BAKWATA walimpinga. Akitoa msimamo huo wa chama Hemed Jumaa alisema huko Shinyanga, kwamba Mwinyi hajui kwanini BAKWATA ilianzishwa nchini. Sheikh huyo alifafanua kwa kusema kwamba, inaelekea Mwalimu Nyerere aliyeianzisha BAKWATA hakumfahamisha madhumuni ya kuanzishwa chama hicho. Leo Mwinyi anajua BAKWATA ni ya nani na madhumuni yake nini. Mwinyi vilevile anajua kuna vita wanapigwa Waislamu; anafahamu kwamba amani imeondolewa, na Waislamu hawana amani. Nchi yetu ina katiba inayompa haki kila mwananchi. Lakini Waislamu wameuliwa kwa tamko la Paroko. Paroko alitamka dhidi ya Waislamu. Waliohusika hawakutaka kuchunguza, hatimaye Waislamu wakauliwa. Na haijakuwa chochote licha ya kuwepo sheria na utawala unaodai kufanyakazi kwa mujibu wa sheria. Pamoja na Waisamu kupigwa vita na kuuawa kikatili namna hiyo bado Mwinyi anadai kwamba eti nchi hii kuna amani. Hivi kweli katika mazingira kama hayo mtu anaweza kusimama na kuzungumzia kuwepo kwa amani na upendo? Ni upendo gani wa watu kuuliwa kisha wauaji kupongezwa? BAKWATA na Washirika wake wasijidanganye kwa kudhani kwamba mauaji yale ya Mwembechai yamekwishapita wala wasidhani kwamba Waislamu wamekwishazikubali dhuluma wanazofanyiwa. Na waelewe kwamba siku zote madhalimu na wakandamizaji hawawezi kufuzu. Jitihada na ghiliba kama hizi hazisaidii. UWAWARU ulipelekwa Rufiji na ulidai kuwakilisha umoja wa Waislamu na Wakristo, nao chimbuko lake lilikuwa hilo hilo la BAKWATA na Waislamu walivyogundua hilo na ghiliba za kuendeleza Ukristo kwa kisingizio cha amani na upendo wamelisusa. Na umoja huu uliotangazwa unaokuja katika mazingira ambayo wahadhiri wa Kiislamu wakifanya mihadhara wakamatwe, wateswe na kufungwa; Wakati Wakristo wakiachiwa kufanywa watakalo hadi kuwagawia Biblia hata watoto wadogo wa Kiislamu mashuleni huku wakisimamiwa na Serikali. Waislamu hawatavumilia. Ni vema BAKWATA na washirika wake wakalielewa hilo, umoja wao wabaki nao huko huko, wasithubutu kuuleta kwa Waislamu. Wabillah Tawafiq Jumuiya ya Wanataaluma wa Kiislamu Tanzania |
YALIYOMO
KAULI
YA WAISLAMU
Karume adaiwa ‘kutafuta ujiko’ kwa kutofautiana na Mkapa Mkapa akiuka sera yake-Chuo Kikuu Uandikishaji wapiga kura waanza CUF yataja wagombea wake Temeke CCM yamtuhumu Mwenyekiti wake pandikizi Propaganda ya Udini itaisambaratisha nchi - CHADEMA USHAURI NASAHA
MAKALA
MIPASHO NASAHA
MAKALA
KALAMU YA MWANDISHI
Je, unajua haki yako unapokamatwa na polisi? LISHE
|
|
|
|
|