|
MASHAIRI:
NYERERE UMESAHAU?!
1. Kumradhi Mhariri, niweke japo pembeni,
Dosa Aziz Mahiri, Rama Mashando Plantani,
Dustan wa Omari, Takadir, Selemani,
Nyerere umesahau, mashujaa wa uhuru.
2. Wajukuu taabani, Nyerere umesahau,
Islam Gerezani, utadhani maumau,
Chuki mwana Athumani, Mola ammpe nafuu,
Nyerere umesahau, mashujaa wa uhuru.
3. Abduwahad Saki, uhuru kapigania,
Tena naye Ally Saki, John Rupia shawia,
Ni vipi hawazinduki, hao ulowaacha,
Nyerere umesahau, mashujaa wa uhuru.
4. Pat mwana wa Kunambi, Tabora Bantu Kasela,
Wapeleka rambirambi, wakirejea kwa Mola,
Uhaiwao vitimbi, sasa twafia jela,
Nyerere umesahau, mashujaa wa uhuru.
5. Kumsahua Milinga, Germa Pacha Kimalando,
L. MwanaMakaranga, Nusura yake upondo,
Asha Ngoma mwana Yanga, jina lake ni mdondo,
Nyerere umesahau, mashujaa wa uhuru.
6. Japhet mwana Kirilo, Saadani Abdi Kandoro,
Bugohe Kitwana Kwalo, jina lenye mgogoro,
Titi Mohammed Kolo, Iddi mwafongo Kasoro,
Nyerere umesahau, mashujaa wa uhuru.
7. Mohammed Mtamila, na Tatu Bonyi Mzee,
Haidari Mwinyimvua, Saidi Tanu Tawae,
Gerezani wanalia, Islamu uwatoe,
Nyerere umesahau, mashujaa wa uhuru.
8. Ramia Mwana Hamadi, naye Hassani Amiri,
Ulichukuwa ahadi, Islam kustiri,
Walsh Alikurudi, Dosa kabeba Khatari,
Nyerere umesahau, mashujaa wa uhuru.
Masare S.R. Ndwata (Mrambowa ’71),
S.L.P. 70535,
Dar es Salaam.
Uhodari gani huo wa majumba kuchomwa moto?
1. Gari limepamba moto, Abiria sote mbio,
Na dereva Kiroboto, mtu asomasikio,
Hata panapo mkito, mwendo wake yeye mbio,
Uhodari gani huo, majumba kuchomwa moto?
2. Cheo chanzo cha mapato, siwatu kosa mafao,
Leo wakubwa watoto, hawahishiwi kilio,
Bado wapo tumbo joto, kwa kusoka kwa makao,
Uhodari gani huo, majumba kuchomwa moto?
3. Kuchomewa nyumba moto, hali kuwafikirio,
Awamu hii majuto, zimekithiri tukio,
Uwamuzi wa mkato, mwavuruga vyenu vyeo,
Uhodari gani huo, majumbe kuchomwa moto?
4. Nyoyo zenu sitakato, mwathamini oshanguo,
Na mlalapo kwa mito, mwaoga kwa misuguo,
Fadhira zenu mpito, hamkumbuki chaguo,
Uhodari gani huo, majumbe kuchomwa moto?
5. Kutokuwa hata ndoto, katika lile tukio,
Mlihuwa na watoto, ma kaka na baba zao,
Mwaka hujawa mpito, Wanzasa nao vilio,
Uhodari gani huo, majumba kuchomwa moto?
6. Mwembe Chai, swala zito, lipi kwenu listuo,
Asikali kila pato, na wakuu wa vituo,
Kuja leta mkong’oto, hati hudai tishio,
Uhodari gani huo, majumba kuchomwa moto?
7. Njia nikua mpito, Wallahi kwa siku hiyo,
wenyewe bila msito, kwa kuvaa kwao ngao,
Asikali wa mseto, Polisi fefu yu nao,
Uhodari gani huo, Majumba kuchomwa moto?
9. Beti nafanya mkato, Sitozidi endeleo,
Sikulia si kushoto, nafanya maangalio,
Nafananisha na chato, alapo pasi mlio,
Uhodari gani huo, Majumba kuchomwa moto?
Dk. Shamte “A’ Mpita (Kijukuu cha Malenga),
c/o Lambalamba,
S.L.P. 66563,
Dar es Salaam.
Watatu kuwa mmoja
Ongeza moja na moja, mbili jibu utapata,
Kizidi nyingine moja, huwa tatu siyo sita,
Kusema jibu ni moja, unayaleta matata,
Hesabu sijaiona, watatu kuwa mmoja.
Ya hivyo sikuiona, shule zote nilopita,
Yeyote ataiguna, kwa kuona ina tata,
Jaribu kutwa mchana, jawabu kulitafuta,
Hesabu sijaiona, watatu kuwa mmoja.
Baba na mwana pamoja, na roho akiwakuta,
Ni watatu bila hoja, akilini inakita,
Vingine huwa kioja, bure tabu mnaleta,
Hesabu sijaiona, watatu kuwa mmoja.
Kauli hii kunena, hakika inawasuta,
Mashiko hasa haina, kwenye hoja kuileta,
“Mtafuma na kushona”, kinyume hamtopata,
Hesabu sijaiona, watatu kuwa mmoja.
“Baba” huyo ni mmoja, hesabu inavyoleta,
:”Mwana” kwa Baba akija, wawili tunawapata,
Jaribu vyanda kukunja, jawabu linajileta,
Hesabu sijaiona, watatu kuwa mmoja.
“Fumbo”tumeshaliona, twaliachia kupita,
Nasi huko kubishana, twakatazwa katakata,
Tunayo bora hazina, mafunzo yalotakata,
Hesabu sijaiona, watatu kuwa mmoja.
Witiri Mungu mmoja, uungu hana mwambata,
Pekee ninamtaja, mwenziwe hutompata,
Nufusi tatu kutaja, moyo wangu unasita,
Hesabu sijaiona, watatu kuwa mmoja.
JIHAD R. SABALLA,
S.L.P. 347, SHINYNAGA.
|
YALIYOMO
'White Paper ni ulaghai wa
Serikali ya CCM'
Na Mwandishi wetu
Sheikh Omar Bashir awekwa rumande
Na Mwandishi Wetu
Mpango wa 'Kupindua' uongozi
wa Bakwata: Masheikh Dar waitwa polisi kuhojiwa
Na Mwandishi Wetu
Zahrau Day yatikisa Tanga
Na Mwandishi Wetu
MAKALA: Hatuna haja ya maelekezo ya
yule aliyetufikisha hapa
Na Alhaj Yusuf Kalala, Washington DC USA
Huduma za afya Kondoa haziridhishi
Na Abu Zubeir
Wasemavyo wanaharakati
Tunahitaji 'UN' ya Waislamu!
Na Twahir Rashid
Hoja binafsi: Wawekezaji watuondokesha
makwetu
Jamii inapokuwa soko huria...
Na Said Rajab
Someni kwa ajili ya Allah - Sheikh
Baruti
Na Muhibu Said
Madrasa Al-Ii'Tiswamu
Al-Umaahaati Fiisabiililillah - Moro
Na Rajab Rajab, Morogoro
Madrasat Hidayat Mbagala
Na Mussa Salum
Hali ya Uislamu Moro
Vijijini yazidi kuwa mbaya
Na Rajab Rajab, Morogoro
Sheikh Masoud Mwinyi awaonya
Waislamu kuacha migogoro Babati
Na Abu Zuberi - Babati
Tusikaribishe mfungo wa Ramadhani
kwa Vunja Jungu
Na Abeid Poyo
'Acheni zinaa muepukane
na ukimwi'
Na Mussa Salum
Wavunja jungu watahadharishwa
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
Hoja/Uchambuzi:
Je, hivi tuendelee kushika
amri za Mungu tena?
Na Mwinjilisti Bunga E. Dettu
Njia ya uzimani ni nyembamba,
waionao ni wachache
Na Yasin Valerian Massawe
Habari:
Semina ya Maimamu Tanga yadai:
Maimamu wanapuuzwa
Na Mwandishi Wetu
Kesi ya Waislamu Mwembechai
yaahirishwa kwa mara nyingine
Na Muhibu Saidi
Kongomano la wanawake wa
Kiislamu Bagamoyo
Na Mwandishi Wetu
Sayansi na Teknolojia
[Kuongeza RAM kwenye Kompyuta]
Masomo ya Dini ya Kiislamu
Barua za Wasomaji
Mashairi
Chakula na lishe
[Madini ya Zinc] |