AN-NUUR 
Na.178 Shaaban  1419, Desemba 4 - 10, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Habari:
 
Semina ya Maimamu Tanga yadai:
Maimamu wanapuuzwa
 

• Watakiwa kuwa na kauli moja 

• Waonywa wasing’ang’anie Uimamu 
 

Na Mwandishi Wetu 

IMEELEZWA kwamba hadhi na thamani ya Maimamu nchini imekuwa ya chini sana kiasi kwamba hata waumini wenyewe wamefikia hatua ya kuwapuuza. 

Aidha kutokana na Maimamu kutokuthaminiwa na nafasi zao kama viongozi wa Waislamu kutokutambuliwa katika jamii, malalamiko ya Waislamu yamekuwa hayasikilizwi wala kupewa umuhimu wowote. 

Wakizungumza katika semina ya Maimamu iliyoandaliwa na Taasisi ya Jamaatul Kheir, baadhi ya Maimamu pamoja na kuonyesha dosari hiyo kubwa wamesema kwamba imekuwa ni vigumu kilio cha Waislamu kusikilizwa kwani Maimamu wenyewe hawana kauli moja. 

Sheikh Mohammed Idd katika nasaha zake, alisema kwamba ni muhimu Maimamu waungane wawe kitu kimoja ili kuziba mwanya ambao maadui waweza kuutumia kuwaparaganya Waislamu. 

Akizungumza katika semina hiyo iliyofanyika Novemba 29, mwaka huu katika hoteli ya Kola Prieto, Sheikh Abdallah Bawaziri aliwahimiza Maimamu wawe wanakutana mara kwa mara kusalimiana na kujuliana hali kama njia moja ya kufikia kwenye umoja alioutaja Allah (s.w.) katika Qur’an (3:103). 

Naye Sheikh Mohammed Kombora aliwatanabahisha Maimamu wasiwe ni wenye kung’ang’ania Uimamu pale waumini wanaponyesha kutokuridhika na utendaji wao. Kwa upande mwingine Sheikh Kombora aliwakumbusha Waislamu kuwa wanawajibika kumtii Imamu na kama Imam huyo kakiuka maadili basi juhudi za mara moja zifanywe kumuweka mwingine. 

Semina hiyo ya Maimamu imekuwa ni ya kwanza na ya pekee mjini Tanga kwani imewakutanisha Maimamu kutoka zaidi ya Misikiti 40 iliyo chini ya taasisi mbalimbali. 

Sheikh Ali Zumo kutoka Ansaar Suna ndiye aliyesoma Qur’an tukufu ya ufunguzi ambayo ilifasiriwa na Sheikh Suleiman Bakar wa TAMTA. 

Sheikh Suleiman katika kuifasiri aya ya 35 ya Suratul-Nuur aliwataka Waislamu wawe ni nuru ya kuongoza umma katika kheri. 

Katika hotuba ya kuwakaribisha wanasemina, Sheikh Shauri Abubakar wa Jamaatul Kheir alizitaka taasisi mbalimbali za Kiislamu kujiimarisha na kusambaza huduma zao hadi ngazi za wilaya na kata. 

Katika jumla ya maazimio ya semina hiyo ni kwamba fursa ziandaliwe ili Maimamu wawe wanakutana mara kwa mara ili kujenga umoja na uongozi imara wa Waislamu. 


Kesi ya Waislamu Mwembechai yaahirishwa kwa mara nyingine
 

• Yadaiwa hakimu anaumwa 

• Kesi nyingine kusikilizwa Kisutu 
 

Na Muhibu Saidi 

KESI ya tuhuma ya kufanya "ghasia" maeneo ya Mwembechai, Jijini Dar es Salaam iliyofunguliwa na serikali katika mahakama ya Kivukoni, Jijini dhidi ya Waislamu kumi imeahirishwa tena hadi Desemba 21, mwaka huu, tarehe ambayo inatazamiwa tena kuanza kusikilizwa. 

Kesi hiyo ilipangwa kuanza kusikilizwa mahakani hapo mapema Desemba 2, mwaka huu, ambapo mashahidi wa upande wa serikali walitarajiwa kutoa ushahidi wao. 

Hata hivyo, mahakama hiyo imeamua kuahirisha kesi hiyo kwa madai kwamba Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Bw. Gabriel Mirumbe anaumwa. 

Kesi hiyo yenye namba 407/98 ilifunguliwa mahakama ya Hakimu mkazi ya Kisutu, Jijini mapema mwezi Machi , mwaka huu ambapo baadae ilihamishiwa katika mahakama ya Kivukoni Jijini Dar es Salam, 

Watuhumiwa katika kesi hiyo ni pamoja na Rutemba Shaaban, Iddi Selemani, Ismaili Hamisi, Jafari Mohamed, Omari Hemed, Hassan Habibu, Hamisi Nassoro, Ally Daudi, Juma Ali na Nurdin Abbas. 

Wakati huo huo, kesi nyingine namba 184/98 ya tuhuma ya kufanya ghasia na kujeruhi inayowakabili Waislamu kumi na mmoja, inatazamiwa kuanza kusikilizwa hapo Desemba 14, mwaka huu katika mahakama ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam. 

Aidha, kesi nyingine namba 192/98 ya tuhuma ya kufanya ghasia, kuharibu mali hapo Mwembechai, inayowakabili Waislamu wengine kumi na mbili nayo pia inatazamiwa kuendelea kusikilizwa hapo Desemba 14, mwaka huu pia katika mahakama ya Kisutu. 


Kongomano la wanawake wa Kiislamu Bagamoyo:

Kikwete, Msabaha, Mikidadi, Ramiya, Kimbau kualikwa 

Na Mwandishi Wetu 

Kongamano la wanawake wa Kiislamu litakalofanyika mjini Bagamoyo hivi karibuni linatazamiwa kuhudhuriwa na maelfu ya wanawake kutoka sehemu mbali mbali nchini. 

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake wa Kiislamu nchini, Bi Fatma Lazaro kongamano hilo litawashirikisha wanawake kutoka mikoa ya Pwani, Dar es Salaam, Morogoro, Iringa na Dodoma. 

Mwenyekiti huyo amesema huenda wakawalika Wabunge wa Mkoa wa Pwani katika kongamano hilo. 

"Tutawaalika waheshimiwa Waheshimiwa Jakaya Kikwete, Dk. Msabaha, Prof. Mikidadi, Ramiya na Kanali Kimbau katika kongamano ili tuwakabidhi risala na maazimio yetu" alisema Mwenyekiti huyo, alipokuwa akizungumza na mwandishi nyumbani kwake Manzese Jijini Dar es Salaam. 
 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
'White Paper  ni ulaghai wa  Serikali ya CCM' 
Na Mwandishi wetu 

Sheikh Omar Bashir awekwa rumande 
Na Mwandishi Wetu 

Mpango wa 'Kupindua' uongozi wa  Bakwata: Masheikh Dar waitwa polisi kuhojiwa 
Na Mwandishi Wetu 

Zahrau Day yatikisa Tanga 
Na Mwandishi Wetu 

MAKALA: Hatuna haja ya maelekezo ya yule aliyetufikisha hapa  
Na Alhaj Yusuf Kalala, Washington DC USA 

Huduma za afya Kondoa haziridhishi 
Na Abu Zubeir 

Wasemavyo wanaharakati 

Tunahitaji 'UN' ya Waislamu! 
Na Twahir Rashid 

Hoja binafsi: Wawekezaji watuondokesha makwetu 

Jamii inapokuwa soko huria...  
Na Said Rajab 

Someni kwa ajili ya Allah - Sheikh Baruti  
Na Muhibu Said 

Madrasa Al-Ii'Tiswamu Al-Umaahaati Fiisabiililillah - Moro 
Na Rajab Rajab, Morogoro 

Madrasat Hidayat Mbagala 
Na Mussa Salum  

Hali ya Uislamu Moro Vijijini yazidi kuwa mbaya  
Na Rajab Rajab, Morogoro 

Sheikh Masoud Mwinyi awaonya Waislamu kuacha migogoro Babati  
Na Abu Zuberi - Babati 

Tusikaribishe mfungo wa Ramadhani kwa Vunja Jungu  
Na Abeid Poyo 

'Acheni zinaa muepukane na ukimwi'  
Na Mussa Salum 

Wavunja jungu watahadharishwa 
Na Mwandishi Wetu, Morogoro 

Hoja/Uchambuzi: 
Je, hivi tuendelee kushika amri za Mungu tena? 
Na Mwinjilisti Bunga E. Dettu 

Njia ya uzimani ni nyembamba,  waionao ni wachache 
Na Yasin Valerian Massawe 

Habari: 
Semina ya Maimamu Tanga yadai: Maimamu wanapuuzwa  
Na Mwandishi Wetu 

Kesi ya Waislamu Mwembechai yaahirishwa kwa mara nyingine  
Na Muhibu Saidi 

Kongomano la wanawake wa Kiislamu Bagamoyo 
Na Mwandishi Wetu 

Sayansi na Teknolojia 
[Kuongeza RAM kwenye Kompyuta] 
 
Masomo ya Dini ya Kiislamu 

Barua za Wasomaji 

Mashairi 

Chakula na lishe 
[Madini ya Zinc] 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita