|
|
|
Na Mwinjilisti Bunga E. Dettu NIKIWA Mwinjilisti katika Kanisa la Waadventista wa Sabato, mara nyingi sana nimekumbana na swali hili, tena kwa watu mbalimbali, kwa nafsi hii naitumia kutoa majibu ya swali hili kwa kirefu. Tafadhali nifuatilie kwa makini. Swali hili limekuwa swali kubwa kwa watu mbalimbali, hata limegawa watu katika makundi mawili, wanaokubali na kushika amri za Mungu. Na wanaokataa kwamba sasa hauna amri, ziliishia msalabani tena amri zilikuwa za Musa na wana wa Israeli. Kwa makala hii fuatana ili kupata hatima ya swali hili. Kwanza kabisa kwa msomaji ama kwa mwenye swali hili apendaye kupata jibu sahihi yampasa amfahamu kwanza huyo Mungu anayemwabudu kwamba ni Mungu yupi. Nimesema haya kwa sababu tangu mwanzo mwanadamu ameshindwa kumfahamu Mungu wake aliyemuumba na badala yake amekuwa akiabudu miungu ambayo haina sifa ya uumbaji. Musa aliwaonya wana Israeli wasiabudu miungu mingine. Kumbukumbu la Torati 11:16 "Jitunzeni nafsi zenu, mioyo yenu isije ikadanganywa, mkageuka na kutumikia miungu mingine na kuiabudu". Soma pia Kumbu. 32:17, shida hii imeenea kizazi baada ya kizazi hata nyakati za Bwana Yesu giza hili liliendelea kufunuka wanaadamu wakaendelea kuabudu miungu wasiyoijua wakidhani kwamba wanamwabudu Mungu aliyewaumba. Soma Yohana 4:20-23. Mtume Paulo naye katika kueneza Injili huko Athene alishangaa kuona watu wakifanya ibada ndani ya majengo makubwa bila kujua kwamba wanamwabudu Mungu yupi! Matendo 17:23 "Kwa sababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona mambo ya ibada yenu, naliona madhabahu iliyoandikwa maneno haya, Kwa Mungu Asiyejulikana. Basi mimi nawahubirini habari zake Yeye ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua". Shida hii haikushia nyakati za Paulo tu bado imeenea hata katika kizazi chetu hiki. Na ndiyo sababu kubwa leo ya watu kuwa makundi makundi wakati tunadai kwamba Mungu wetu ni mmoja, ili tuondokane na shida hii hatuna budi kujiuliza maswali haya na kupata majibu sahihi. 1. Mungu tunayemwabudu anaitwa nani?
Katika kuangalia mambo haya, maandiko katika Kumbukumbu la Torati 4:39 na Isaya 26:4 yanabainisha wazi jina la ukuu wa Mungu wetu, Torati 4:39 inasema "Kwa hiyo ujue, leo hivi, ukaweke moyoni mwako, ya kuwa Bwana ndiye Mungu katika mbingu juu, na katika nchi chini, hapana mwingine. Cheo chake pia kimeelezwa katika kutoka 20:11 "Maana kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na chini na bahari na vyote vilivyomo akastarehe siku ya saba kwa hiyo Bwana akaibariki siku ya Sabato akaitakasa. Hapa cheo chake kimeleezwa wazi kwamba ni Muumbaji wa Mbingu na nchi na bahari na vyote vilivyomo. Na mamlaka yake pia yameelezwa hapo hapo kwamba ni juu ya mbingu na nchi na vyote vilivyomo. Sifa hizi ndizo pekee zinazomtofautisha na miungu mingine ambayo inaitwa miungu lakini haikuumba chochote, haitawali mbingu na nchi, wala haina mamlaka juu ya vyote. je Mungu unayemwabudu wewe ana sifa gani? Baada ya kupata jibu ya maswali hayo matatu, sasa tuangalie kipengele muhimu sana, hiki cha nne, na hicho ndicho kitatupatia jibu la swali letu. Mungu anazo tabia mbili na tabia hizi hazitenganishwi Ufunuo 15:4 "Ni nani asiyekucha, Ee Bwana na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako u mtakatifu, kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele zako kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa". Tabia ya pili ya Mungu imetajwa katika waraka wa kwanza wa Yohana 4:7-8 "Wapenzi, na tupendane kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila ampendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu yeye asiyempenda hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo". Hapo tumeona tabia ya Mungu imeelezwa waziwazi kwamba Mungu ni Mtakatifu na Mungu ni Upendo. Utakatifu wa Mungu unaonyeshwa katika sheria na amri zake. Na sheria ina tabia ya kudai itimizwe ndiyo maana sheria daima inatumia neno hili Usi...Usiibe, Usiue, Usizini ikumbuke Sabato n.k. Na upendo wa Mungu unaonyeshwa na kufunuliwa katika Injili. Na Injili maana yake ni habari njema za matendo makuu ya Mungu kumwokoa mwanadamu katika Yesu. Na upendo ambao ndio Injili una tabia ya kutoa. Yohana 3:16 "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Kazi ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu inafanyika kwa njia ya Neno lake (Biblia). Na Biblia nzima imejaa utakatifu wa Mungu na upendo wa Mungu ambao ndio Sheria na Injili. Agano lote la kale limejaa sheria na Injili na Agano jipya limejaa Injili na sheria. Mwanadamu hapati kuokolewa kwa kuhubiriwa Injili tu, wala hapati kuokolewa kwa kuhubiriwa sheria tu, lazima ahubiriwe Neno lote la Mungu ambalo ni sheria na Injili. Wala siyo sahihi kusema kwamba Agano lote la kale ni sheria tu, hivyo hivyo ni makosa kusema kwamba Agano jipya lote ni Injili tu, wala Injili si vitabu vya Mathayo, Marko, Luka na Yohana pekee. Hebu nitoe mifano michache ya Injili katika Agano la Kale na sheria katika Agano jipya. Adamu na Hawa walipewa sheria, wasile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Haya ni maneno ya sheria yaliyowadai Adamu na mkewe wayatimize. Na walipopavunja Mungu hakuwaacha hivyo hivyo, aliwapa ahadi kwamba katika uzao wa Hawa atatokea mtu atakayemponda kichwa shetani. Je, mwamjua mtu huyo? Ni Yesu! Inaendelea toleo lijalo
Na Yasin Valerian Massawe a) ZABURI 14:1-2 - "Mpumbavu amesema moyoni, hakuna Mungu, wameharibu matendoyao na kuyafanya chukizo, hakuna atendaye mema. Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu." (b) MITHALI 12"1-2: "Kila apendaye mafundisho hupenda maarifa. Bali yeye achukiaye kulaumiwa ni kama mnyama. Mtu mwema atapata upendeleo kwa Bwana; bali mtu wa hila atahukumiwa naye." (c) MITHALI 29:1: "Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, atavunjika ghafla, wala hapati dawa." (d) MITHALI 27"22" "Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano; upumbavu wake hautamtoka." 1. Elimu haina mwisho Binadamu ni kiumbe wa Kiroho. Katika mbingu na ardhi zimo ishara kubwa sana za kuonyesha hakika ya Mwenyezi Mungu. Vile vile katika maumbile yetu wenyewe zimo ishara nyingi. Kwa maana hii ni lazima binadamu ajue hakika ya Mungu ni yupi kwa vile imani ni nyingi. Mungu wa haki ni mmoja tu aishiye milele na imani ya haki ni moja tu iliyofundishwa na Manabii. Jambo la kwanza lililosisitizwa na Manabii katikamafundisho yao ni "Utakatifu wa Mungu" kwamba utakatifu wake ni "Alama" kwamba baina yake ni viumbe ni "Tofauti kubwa" Ajabu! Haiwezekani kumfananisha - kumlinganishawala kumsawazisha kwa sababu yeye ni "Mkamilifu" (Isaya 40:18,25, 46:5,9, Zaburi 89:6, 113:5, 86:8-10, Kumb:33:"26 n.k.). "Mungu ni Mmoja tu Milele na hata milele". Hakuongezewa kitu wala hakupunguziwa kitu. Ni Mmoja tu (The Unique?) (Yoshua bin Sira 42:21). (a) MITHALI 14:15-16" "Mjinga huamini kila neno; bali mwenye busara huangalia sana aendavyo. Mwenye hekima huogopa, akajitenga na uovu; bali mpumbavu ana ufidhuli, nakujitumai." (i) Mwanzo 1:26-27 "... Mungu aliumba mtu kwa sura na mfano wake......"!!! (ii) Yohana 1:1-3 ".....Neno (Yesu) si kiumbe...." Yohana 1:18 "....Mungu Mwana Pekee....."!!! (iii) 1 Yohana 5:8 "...Wako watatu washuhudiao mbinguni....." !!! (iv) 1 Yohana 4:1-3 "....Roho isiyokiri kwamba Kristo (ni Mungu) alikuja katika mwili, basi Roho hiyo haitokani na Mungu...."!!! (b) Yohana 17:3 "(Yesu anasema) Na uzimawa milele ndiyo huu, wakujue wewe, Mungu wa Pekee wa kweli, naYesu Kristo uliyemtuma." (c) Yohana 6:65 (Yesu) Akasema, kwa sababu hiyo nimewaambia ya kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amejaliwa na Baba yangu (Bwana)." Ukimwuliza Mkristo Yesu alitumwa na nani, bila shaka atasema alitumwa na Mwenyezi Mungu, au ukimuuliza ni nani aliyemtuma Malaika Gabriel kwenda kwa Maryam kumpasha habari ya kuzaa Mwana bila Mume, bila shaka atakwambia ni Mwenyezi Mungu. SWALI: Sasa basi, ni nini kinamshinda Mkristo kuamini kuwa yule Mwana aliyezaliwa (Yesu) ni Kiumbe wa Mwenyezi Mungu? Mkristo anasema Yesu ni Mwana wa Mungu (Mungu Mwana), mara wengine wanasema Yesu ndiye Mungu mwenyewe!!! Mara atarudi kuwahukumu wazima na wafu!!! Mimi binafsi siwezi kumdharau Mkristo kwa sababu najua kwamba hekima au uwezo wa kufasiri maandiko au Roho ya kujua hili ni kweli au hili ni uongo, hawezi kuwa nao mtu mpaka apewe na Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu humsaidia yule anayependa kufahamu. Kuna tofauti kubwa sana kati yakusoma, kuamini na kuelewa. Kwa sababu wamesoma wengi, wana imani wengi lakini wanaoelewa (waliojaliwa Ujuzi wa Kumjua Mungu) ni wachache. "Kuelewa" maana yake ni kuijua Anwani sahihi ya Mungu na kusimama na wale wanaoitumia. Answani sahihi ya Munguni hii ifuatayo:- Marko 12:28-34 "Na mmojawapo wa waandishi akafika, akawasikia wakisemezana naye, akatambua ya kuwa amewajibu vema, akamwuliza, katika amri zote ni ipi iliyoya kwanza? Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyohii, sikia, Israel, Bwana Mungu wetu ni Bwana Mmoja. Nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. Na ya pili ndiyo hii, mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi. Yule mwandishi akamwambia, hakika, Mwalimu, umesema vema ya kwamba "Mungu ni Mmoja", wala hakuna mwingine ila yeye; na kumpenda yeye kwa moyo wote na kwa ufahamu wote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama nafsi yako, kwafaa kuliko sadaka nzima za kuteketezwa na dhabihu zote pia. Naye Yesu alipoona kwamba amejibu kwa busara, alimwambia, wewe huu mbali na ufalme wa Mungu. Wala hakuthubutu mtu kumsaili neno tena tokea hapo." Yesu kasema "Munguni Mmoja". Moja maana yake ni -1- haiongezewi kitu wala haipunguziwikitu.Munguni Mpekee (Mkongwe wa Wakongwe) ambaye hana mshirika katika vitendo vyake, majina yake, sifa zake, Uungu wake na amri zake. 2. Kupoteza maarifa (wisdom) Manabii wakuu tukiwaorodhesha wanafikia ishirinina watano (25). Yule wa ishirini na nne (24) aliumbwa kimwujiza, akafanya miujiza mingi, akaondokakimwujiza ambapo katika mafundisho yake alitahadharisha mambomengi. Kwa kuwataja kwanza hao ishirini na wanne (24) ni hawa:- Adam, Henoko (Idrisa), Nuhu, Hud, Salehe, Ibrahim, Ishmael (Ismail), Isaka, Luti, Yakobo, Yusufu, Jethro (Shuaib), Ayubu, Musa, Haruni, Ezekiel (Thu’l-Kifl), Daudi, Suleiman, Eliya, Elisha, Yona, Zakaria, Yohana (Yahya) na Yesu (Issa). Inaendelea toleo lijalo
|
YALIYOMO
'White Paper ni ulaghai wa Serikali ya CCM' Na Mwandishi wetu Sheikh Omar Bashir awekwa rumande
Mpango wa 'Kupindua' uongozi
wa Bakwata: Masheikh Dar waitwa polisi kuhojiwa
Zahrau Day yatikisa Tanga
MAKALA: Hatuna haja ya maelekezo ya
yule aliyetufikisha hapa
Huduma za afya Kondoa haziridhishi
Tunahitaji 'UN' ya Waislamu!
Hoja binafsi: Wawekezaji watuondokesha makwetu Jamii inapokuwa soko huria...
Someni kwa ajili ya Allah - Sheikh
Baruti
Madrasa Al-Ii'Tiswamu
Al-Umaahaati Fiisabiililillah - Moro
Madrasat Hidayat Mbagala
Hali ya Uislamu Moro
Vijijini yazidi kuwa mbaya
Sheikh Masoud Mwinyi awaonya
Waislamu kuacha migogoro Babati
Tusikaribishe mfungo wa Ramadhani
kwa Vunja Jungu
'Acheni zinaa muepukane
na ukimwi'
Wavunja jungu watahadharishwa
Hoja/Uchambuzi:
Njia ya uzimani ni nyembamba,
waionao ni wachache
Habari:
Kesi ya Waislamu Mwembechai
yaahirishwa kwa mara nyingine
Kongomano la wanawake wa
Kiislamu Bagamoyo
Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|