|
|
|
Dr Yousuf Alqaradhawy: Kuporomoka kwa Waislamu katika mawanja yote ya maisha ya Kiislamu ni matokeo ya kuwambali kwao na Uislamu uliyo sahihi, kwa kuuelewa na kuutekeleza. Hapana makosa kuzichukua elimu za kawaida kutoka kwa wasio kuwa Waislamu, lakini makosa ni kuuchukua utamaduni wao, na ada zao. Kukosea katika dhati yake siyo aibu, lakini kuyaridhia maskoa na kuendelea kuyafanya na kuyatetea ndiyo makosa makubwa sana. Mwenye akili ni yule ambaye amelizingatia jambo kabla ya kutokea kwake, na akaliandalia maandalizi yake. Maneno hayachukui nafasi ya matendo. Unyuma ndilo tatizo la akili ya Kiislamu. Kuzitawanya nguvu za Waislamu huko ndiko kuudhoofisha Uislamu, katika kukabiliana na maadui zake. Utulivu haupatikani kwa amani, na asiye kuwa na uhuru hana amani. Al-Ustadh Ahamad Muhammad Rahoma: Msingi wa Da’awah na mategemeo yake ni Qur’an. Ni katika shirki kubwa kuifanya isiyo kuwa Qur’an sheria na mwongozo. Uislamu umewaita watu kwenye kufikiri. Qur’an imekusanya kheri za dunia na akhera kwa watu wote. Maisha hayatatengenea ila kwa Qur’an. Dini siyo milki ya mtu yeyote. Hapana kitu cha kuingia kati, kati ya Mwenyezi Mungu na viumbe wake. Qur’an huchagua katika mawaidha yake ambayo mna ndani yake maonyo na mazingatio. Haikupigwa mifano ndani ya Qur’an kwa mchezo na pumbao. Qur’an ina mfasiria mwanaadamu siri ya kupatikana kwake. Al-Ustadh Muhammad Qutub: Kujifunza historia ya nchi za Magharibi kutatupa faida kubwa katika kuvitafiti hivi vita vikali vilivyopo leo kati ya nchi hizo na nchi za Kiislamu. Mwanaadamu ni mwanaadamu, pajapo tokea tofauti kati ya mtu na mtu na kati ya taifa na taifa na kati ya kizazi na kizazi. Mwanaadamu yuko chini ya kanuni ambazo zinayatawala maisha na pia zina utawala ulimwengu. Fiqhi ya Kiislamu ni utekelezaji wa kimatendo wa fikra ya maendeleo ya watu na jukumu lake wakati wote ni kutafiti ufumbuzi mpya wenye kuchukuliwa katika misingi ya dini na kiini chake. Ametaka Mwenyezi Mungu wawe watu ndiyo nyenzo ya utendaji katika ardhi. Mwanaadamu ndiye anayeibadili hali iliyopo, na ndiye anaye buni mipango na mabadiliko hayo ndiyo matakwa ya Mwenyezi Mungu. Sura ya Uislamu iliyoharibiwa ndiyo adui wa kwanza leo wa fikra ya Uislamu. Uislamu ni utaratibu wa kimatendo hautosheki na mawaidha na maelezo tu. Hakuna Uislamu wa maendeleo na mwingine uko nyuma. Taratibu za Mwenyezi Mungu zina kwenda pasina na upendeleo, na historia hayimngoji mtu yeyote. Qur’an imefungwa katika tundu la chuma. Itakapoachwa huru Qur’an na umma utakuwa huru. Imekuja dini kwa ajili ya mwanadamu hakuja mwanaadamu kwa ajili ya dini. Akili za Waislamu zinafanya kazi upande mmoja tu, zinapokea, na hazitoi. Hali tuliyoifikia ni jukumu la utawala sio jukumu la Qur’an. Uislamu ni itikadi na sheria. Kutenganisha kati ya dini na dola ni urithi wa fikra ya kimagharibi ambayo ilichukua nafasi yake katika fikra ya Waarabu katika zama za kuporomoka na kurudi chini. Waislamu wako katika jangwa na dunia iko katika jangwa jingine. Zilikutanika sababu nyingi zilizoufanya Uislamu ni utaratibu wa kiakhera ambazo haupiti duniani bali unachupa tu, kwenda peponi au motoni. Tawheed ndiyo msingi wa itikadi na uadilifu ndiyo msingi wa sheria. Kufanya uadilifu kati ya watu ndilo lengo lililokusudiwa kwa sheria ya Kiislamu. Ni lazima pawe na uwiano kati ya dini ya Uislamu na dunia yake. Tuanze kwa kukiandaa kizazi cha Kiislamu, na nyenzo yake ni hekima na mawaidha mema. Kuzitengeneza kanuni ni jambo, lakini ugumu unapatikana katika kukiandaa kizazi kipya ambacho kinaziamini. Wito wa kuzitekeleza sheria za Kiislamu unapita katika jangwa wakati kumuandaa Muislamu atakayezitekeleza kunapita katika jangwa jingine. Wale ambao wanautangaza Uislamu juu ya kuwa ni ujumbe wa kutoa adhabu na wala si ujumbe wa kuwaongoza na kuwafanikisha, hao hawako sahihi. Uislamu ni itikadi ya jumla haibadili, kugawanya na kutiwa viraka. Umetoka umma wa Kiislamu katika uzalishaji na kuwa walaji, na badala ya kuwa chimbuko la historia wamekuwa ndiyo simulizi kwa watu wengine. Akili za Waislamu zimo katika mapumziko ya muda mrefu sana. Mwanaadamu ndani ya Qur’an ni kiumbe aliye tukuzwa. Qur’an imeondolewa katika nafasi ya kuongoza na kufungiwa katika jumba la makumbusho. Kuna utengano kati ya dini na dunia katika hali halisi ya maisha ya Waislamu. Kutokana na kutenganishwa Qur’an na utawala kumetokea maharibiko makubwa katika ulimwengu wa Kiislamu. Huko nyuma ulikuwa utawala umewekwa
kwa maslahi ya Qur’an, mambo yamegeuzwa, hivi sasa imewekwa Qur’an kwa
maslahi ya utawala.
|
YALIYOMO
'White Paper ni ulaghai wa Serikali ya CCM' Na Mwandishi wetu Sheikh Omar Bashir awekwa rumande
Mpango wa 'Kupindua' uongozi
wa Bakwata: Masheikh Dar waitwa polisi kuhojiwa
Zahrau Day yatikisa Tanga
MAKALA: Hatuna haja ya maelekezo ya
yule aliyetufikisha hapa
Huduma za afya Kondoa haziridhishi
Tunahitaji 'UN' ya Waislamu!
Hoja binafsi: Wawekezaji watuondokesha makwetu Jamii inapokuwa soko huria...
Someni kwa ajili ya Allah - Sheikh
Baruti
Madrasa Al-Ii'Tiswamu
Al-Umaahaati Fiisabiililillah - Moro
Madrasat Hidayat Mbagala
Hali ya Uislamu Moro
Vijijini yazidi kuwa mbaya
Sheikh Masoud Mwinyi awaonya
Waislamu kuacha migogoro Babati
Tusikaribishe mfungo wa Ramadhani
kwa Vunja Jungu
'Acheni zinaa muepukane
na ukimwi'
Wavunja jungu watahadharishwa
Hoja/Uchambuzi:
Njia ya uzimani ni nyembamba,
waionao ni wachache
Habari:
Kesi ya Waislamu Mwembechai
yaahirishwa kwa mara nyingine
Kongomano la wanawake wa
Kiislamu Bagamoyo
Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|