|
|
|
• Kiwege kijiji chenye Waislamu wengi hakina msikiti • Makanisa yajengwa na kubatiza Waislam • Hutembea kilometa
10 kuswali Ijumaa
Na Rajab Rajab, Morogoro
HALI ya Uislamu katika vijiji vingi vyenye Waislamu wengi Mkoani hapa ipo mashakani kufuatia vijiji hivyo kukosa misikiti, madrasa pamoja na masheikh na kufikisha ujumbe, hali iliyopelekea makanisa kuvamia vijiji hivyo na kuwabatiza mamia ya Waislamu. Uchunguzi uliofanywa na Mwandishi wa habari hizi katika Tarafa ya Ngerengere hususan katika kijiji cha Kiwege umebaini kuwa tangu tupate uhuru mwaka 1961 kijiji hicho kilikuwa na asilimia 95 ya Waislamu wanaoishi kijijini hapo, lakini wengi wao hivi sasa wamebatizwa. Kadri miaka ilivyozidi kusogea ndivyo Uislamu katika kijiji hicho ukawa unapotea hasa kutokana na kukosekana msikiti pamoja na madrasa, jambo ambalo lilipelekea dini nyingine kuingia kijijini hapo kwa kasi na kuwabatiza Waislamu ambao wengi wanaona bora waingie katika dini hiyo kuliko kuwa Waislamu bila ya kuufahamu Uislamu wenyewe. Baada ya hali ya Uislamu kuendelea kuwa mbaya kijijini hapo, kukatokea vijana wenye uchungu na dini yao ambapo mnamo tarehe 24, June, 1998 kuanzisha madrasa chini ya Mwembe kwa lengo la kuwafundisha watoto wadogo kwa matazamio ya kuja kunusuru Uislamu kijijini hapo. Madrasa hiyo iliyopewa jina la Rukhuman la kijiji Kiwege kilometa 10 kutoka Ngerengere ulianzishwa na Ustaadh Yusufu Ally Mohamed, Saidi Ally Mbulu pamoja na Juma Rashid Mlali ambapo wawili kati yao wanakaa mjini Morogoro na wanalazimika karibu kila siku kufanya safari ya kwenda kufundisha madrasa hiyo ambayo ina wanafunzi 103 wasichana kwa wavulana. Akiongea na gazeti hili mmoja na walimu hao amesema kama kuwa kijiji chao hakina msikiti wao na baadhi ya Waislamu wengine wanalazimika kila Ijumaa kusafiri kwa mguu mwendo wa kilomekta kumi (10) kutoka kijijini kwao Kiwege mpaka Ngerengere kuswali Ijumaa, huku wakiwaacha Waislamu wenye imani ndogo, wagonjwa na wanawake nyumbani. Katika kujikwamua na hali ya kukosa msikiti waalimu hao kwa kushirikiana na wanafunzi na madrasa na baadhi ya Waislamu wa kijiji hicho wameanza kuzungushia miti katika eneo la madrasa ambapo wanajaribu kuziba zulia ili wapate sehemu ya kufanyia Ibada. Mbali ya Madrasa hiyo iliyoanzishwa chini ya Mwembe, na kuwa kero wakati wa mvua na jua, pia madrasa hiyo iliyotembelewa na mwandishi wa habari hizi ina upungufu wa majamvi ya kukalia na majuzuu ambapo wastani na juzuu moja linasomwa na watoto kumi kwa wakati mmoja hali ambayo ni kinyume kabisa na taratibu za ufundishaji. Walimu hao wa madrasa wamewaomba Waislamu popote pale walipo katoa misaada
yao kwa ajili ya kuunusuru Uislamu kwa kujenga msikiti na madrasa ambapo
wanakijiji wa Kiwege nguvu zao ni ndogo na ukizingatia kijiji hicho sasa
hivi kimekumbana na njaa.
Na Abu Zuberi - Babati
IMAM wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa Mjini Babati, Sheikh Masoud Mwinyi amewatahadharisha Waislamu kuacha migogoro, kwa kuwaambia kamba penye migogoro kamwe hapawezi kukapatikana maendeleo. Sheikh Mwinyi aliyasema hayo katika madrasa yake alipotembelewa na ugeni uliotoka mjini Dodoma, ugeni huo uliongozwa na Sheikh Abdallah Ally wa Masjid Qubaa, Bwana Khalifa Abdallah (Hongera) na Ustadh Idrisa Simba. Sheikh Mwinyi alisema migogoro iliyodumu kwa muda hapa nchini hasa ile ya Misikiti imesababisha waumini kutokuwa na msimamo wa kushirikiana na viongozi wao kuleta maendeleo katika sehemu zao. "Muda mwingi unatumika pamoja na fedha kwa ajili ya kuweka mawakili kutatua kesi za kugombania Msikiti, inafikia hata mahakama kuyarudisha masuala hayo katika mikono ya Waislamu, Misikiti yote ni ya Mwenyezi Mungu iwe inamilikiwa na Taasisi au mtu binafsi au kikundi fulani, hiyo yote ni Misikiti ya Allah (s.w.) iheshimiwe na kuwaacha Waislamu waitumie katika kumwabudu Allah (s.w.)", alisema Sheikh Msoud. Alishauri kwamba Taasisi kubwa za Kiislamu zikae na kuona ni wakati muafaka kuhamasisha maendeleo kwa waumini wao. "Waislamu wanahitaji mambo mengi, vituo vya elimu, vituo vya kulea watoto yatima, miradi ya uchumi, uimarishaji wa Da’awah, mambo haya yatapatikana tu pale migogoro itakapotatuliwa na kuachwa mara moja", alisisitiza Sheikh Masoud. Aidha Sheikh Masoud alisema wanafunzi wake hulipa umuhimu suala la elimu, na nidhamu yake pia kwani bila ya nidhamu elimu haitapatikana. Akiunga mkono wito huo, Sheikh Abdallah Ally alisema, migogoro ya Misikiti ingeweza tu kupatikana ufumbuzi na Waislamu wenyewe bila ya hata kupoteza fedha na muda kwenda mahakamani. Sheikh Masoud anaendesha Da’awah kwa kuwa na madrasa za watoto, na hata
watu wazima. Kwa hivi sasa ameanza ujenzi wa jengo jipya la Msikiti ambalo
kwa sasa linahitaji msaada wa nondo, saruji na kokoto kwa mujibu wa tangazo
lililopo Msikitini karibu na Madrasati Al-Hijira.
|
YALIYOMO
'White Paper ni ulaghai wa Serikali ya CCM' Na Mwandishi wetu Sheikh Omar Bashir awekwa rumande
Mpango wa 'Kupindua' uongozi
wa Bakwata: Masheikh Dar waitwa polisi kuhojiwa
Zahrau Day yatikisa Tanga
MAKALA: Hatuna haja ya maelekezo ya
yule aliyetufikisha hapa
Huduma za afya Kondoa haziridhishi
Tunahitaji 'UN' ya Waislamu!
Hoja binafsi: Wawekezaji watuondokesha makwetu Jamii inapokuwa soko huria...
Someni kwa ajili ya Allah - Sheikh
Baruti
Madrasa Al-Ii'Tiswamu
Al-Umaahaati Fiisabiililillah - Moro
Madrasat Hidayat Mbagala
Hali ya Uislamu Moro
Vijijini yazidi kuwa mbaya
Sheikh Masoud Mwinyi awaonya
Waislamu kuacha migogoro Babati
Tusikaribishe mfungo wa Ramadhani
kwa Vunja Jungu
'Acheni zinaa muepukane
na ukimwi'
Wavunja jungu watahadharishwa
Hoja/Uchambuzi:
Njia ya uzimani ni nyembamba,
waionao ni wachache
Habari:
Kesi ya Waislamu Mwembechai
yaahirishwa kwa mara nyingine
Kongomano la wanawake wa
Kiislamu Bagamoyo
Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|