|
|
|
Masuala mengi kuhusiana na Dola kama vile kupanga mishahara ya wanajeshi, kuanzisha idara mbali mbali, kuwapa vibali wageni kufanya biashara katika Dola ya Kiislamu na kiwango cha kodi wanachotakiwa kulipa, n.k., yaliamuliwa na Khalifa baada ya kushauriana na kamati yake ya utendaji. Kamati hii ilikutana kila siku katika msikiti wa Mtume (s.a.w.). Taarifa za Wilayani na mikoani zilizowasilishwa na khalifa zilijadiliwa na kupitishwa maamuzi. Wanakamati wa kamati hii ya utendaji walipewa nyadhifa mbali mbali; kwa mfano - Abubakr alimteua Umar kuwa "Chief Justice" na msimamizi wa kugawa zaka. Ali aliteuliwa kuwa mkuu wa mawasiliano, kusimamia wafungwa wa kivita, fidia yao na namna ya kuwatendea. Ukiachilia mbali shuura teule, makhalifa wote walitumia shuura ya watu wote msikitini kama chombo cha kusaidia uendeshaji. Uteuzi wa majaji, wakuu wa mikoa, n.k. ulifanywa hadharani msikitini ili kama kuna upinzani wowote juu ya mteuliwa, raia walikuwa huru kupinga kwa hoja wazijuazo. si hivyo tu hata kama kiiongozi ameteuliwa bado raia walikuwa na fursa ya kuwasilisha malalamiko dhidi ya kiongozi muhusika. Ili kujua ukweli wa malalamiko ya watu na kufanya uchunguzi, Tume ya kufuatilia malalamiko ya raia dhidi ya viongozi wao iliundwa chini ya uwongozi wa Muhammad ibn Muslamah Ansar. Malalamiko yalipomfikia Khalifa, alitumwa Muhammad kufuatilia au watu wengine au aliitwa kiongozi muhusika kwa kuhojiwa. Chombo kingine cha utawala kilikuwa mkutano wa watendaji wote wa serikali waliokuwa wanakutana baada ya Hija. Wakati huu Khalifa alikuwa anamsikiliza kila mwenye malalamiko dhidi ya serikali. Kwa namna hii kila mwananchi alihusika na uendeshaji. Si hivyo tu bali khalifa uthman alianza utaratibu wa kusikiliza malalamiko ya wananchi kila Ijumaa.38 Jambo lingine muhimu katika uendeshaji ni kuwa serikali ilitoa mishahara mikubwa ili kuzuia rushwa na mambo yanayolingana. Kama ilivyokuwa wakati wa Mtume (s.a.w.) kwenye utawala, nchi iligawanywa kwenye majimbo na wilaya. idadi ya majimbo na wilaya ilitegemea kupanuka kwa mipaka ya Dola. Baadhi ya majimbo ni kama tulivyoonyesha kwenye kazi za Khalifa. Muhimu hapa ni kuwa ni kuwa kila jimbo au wilaya ilikuwa na viongozi watatu. Gavana au Walii, mkusanyaji mapato ya serikali, Amil na Kadhi (mwanasheria). Viongozi wa wilaya walikuwa chini ya Gavana na wilayani walikuwepo Amil na Kadhi tu. Gavana alifanya kazi zote za Khalifa mkoani kwake. Aliendesha swala za kila siku Ijumaa, Idi zote mbili, na kuongoza msafara wa hija wa watu wa mkoa wake. Alisimamia amani na utulivu mkoani kwake, pale ambapo hakuna kamanda wa kijeshi wa mkoa, mkuu wa mkoa ndie aliyejaza nafasi hiyo na kuwa kamanda wa majeshi ya mkoa na mara nyingine kuongoza mapigano. Pamoja na Gavana viongozi wengine waliokuwa mkoani ni Shaikh Ul-Kharaj au msimamizi wa mapato ya serikali. Sahib Ahdath (mkuu wa polisi), Kadhi na Kamanda wa majeshi. Wakati wa ukhalifa wa umar kiongozi alipoteuliwa aliorodhesha mali zake na ilipoonekana anaongezeko la mali lisiloeleweka aliulizwa na mali yake kutaifishwa. 12. Pato la Serikali Moja ya shughuli muhimu katika uendeshaji wa serikali ni namna serikali inavyopata mapato yake na inavyotumia. Wakati wa Mtume (s.a.w.) tumeonyesha vyanzo vya pato la serikali vikiwa zaka, Jizya, Kharaj, khums na fay. katika kipindi cha Makhalifa wanne vyanzo vya pato la serikali viliongezeka kama ifuatavyo: Ushr. (kodi ya mazao) kutoka katika ardhi ya Waislamu iliyotekwa kivita na kugawiwa askari waliopigana au ardhi ya serikali iliyoandaliwa kwa kilimo au mifugo. Kwa ardhi inayotegemea mvua ya asili, mabwawa na mito ya asili kima chake ni 1/10 ya mazao na kwa mashamba yaliyoyomwagiliwa kiwango cha ushuru ni 1/20 ya pato la mwaka. kharaj au kodi ya Ardhi; kodi hii iliwahusu wasio Waislamu ambao ardhi yao imetekwa kivita lakini wenyewe wameruhusiwa kuendelea kutumia ile ardhi iliyotekwa ambayo ni mali ya Dola ya Kiislamu. Kodi hii ilikadiriwa kufuatana thamani ya ardhi katika maana ya ukubwa wa ardhi na ubora au rutuba ya ardhi. Kodi hii iliwekwa kima maalum baada ya tathmini ya ardhi na ililipwa kwa mwaka. Jizya ilikuwa chanzo kingine cha pato la Taifa. kodi hii iliwahusu wasio Waislamu waliojulikana kwa jina la "Dhimmis". Serikali ya Kiislamu ilichukua dhamana ya kuwalinda wasio Waislamu wao na mali zao. Wasio Waislamu walilipa kodi hii ya jizya kwa kazi ya ulinzi wanayofanyiwa na Waislamu. Kodi hii pia iliwekswa kiwango maalum na haikuwahusu vikongwe, watoto, walemavu na wanawake. Zaka na sadaqa nazo zilibakia kuwa vyanzo vya msingi vya pato la serikali na maelekezo yake ni kama yalivyotolewa kwenye sura ya fiq-hi katika kitabu hiki. Ngawira ni mali inayopatikana kwa kumshinda adui. Hii nayo ilitumika kama chanzo cha pato la serikali. Fay ni mali iliyotolewa na adui hata bila kupigana. Kulikuwa na kodi za muda zilizotozwa kwa maslahi ya nchi hizi zilijulikana kwa jina Zaraib. Kulikuwa na wakfu, karlaz au kodi kutoka kwenye ardhi ya serikali na kodi nyinginezo kama za madini, mali inayoingia nchini au inayopitishwa n.k. Kwa vyanzo hivi serikali iliweza kukusanya mapato yaliyosaidia kuendesha serikali bila matatizo. Si hivyo tu, lakini kulianzishwa Baitul mal au mfuko wa pato la serikali (kwa sasa ndio Benk Kuu). Mali ya serikali ilitumika kwa mujibu wa maelekezo ya mafungu yake, maendeleo ya nchi na wananchi kwa ujumla. Serikali ya makhalifa wale, haikuwa na deni na maisha ya wanachi wake yaliboreshwa kwa kiwango kikubwa. Maendeleo yaliyopatikana kwa wakati ule ni kama ifuatavyo: Kujenga "Canals" wakati wa Khalifa Umar ulijengwa mfereji wa kutoa maji kutoka mto Euphrates hadi Basra kulikokuwa na ukame wa maji. mfereji (Canal) huu uliitwa kwa jina la gavana wa Basra Canal Abi Mussa. Mfereji mwingine uliitwa Canal Maakal. Maakal bin Yasar ndie aliyeusimamia. ulitoa maji kutoka mto Euphrates na kuyapeleka sehemu kadhaa. Canal Saad ulijengwa na Saad baada ya kuombwa na Gavana wa kufa ambae nae alishinikizwa na watu wake wa mji wa Anbar. Mfereji wa mwisho umejengwa na Gavana wa Misri Amir, lakini uliitwa jina la Canal Amirul-Muuminin kwa sababu mnamo mwaka wa 18 Hijra, Arabia kulikuwa na njaa. Khalifa Umar alipeleka nafaka kutoka majimbo mengine kwa kuchelea umbali, alimtaka Gavana wa Misri afikirie njia ya Canal ya kuunganisha mto Nile na Red Sea. Amir Gavana wa Misri alifanya hivyo na ulikuwa mrefu unaokadiriwa kuwa maili 10 hadi 12. Maendeleo mengine yaliyofanywa katika kipindi cha Ukhalifa ni ujenzi wa misikiti, kambi za wanajeshi, mabarabara, majengo ya maofisi na majengo ya ofisi za fedha. 13. Misikiti Misikiti elfu nne 39 inakadiriwa kujengwa wakati wa umar. Hali
kadhalika misikiti ya Makka na Madina ilipanuliwa kwa kununua nyumba zilizokuwa
jirani na Misikiti hiyo. Kazi ya upanu
|
YALIYOMO
Maoni Kuwa na mawazo ya kufugwa tunajidharaulisha Sakata la
mabucha ya Nguruwe kuibuka upya
Bakwata yairushia polisi makombora Ngaramtoni MACHO YA
SHUTUMA
Serikali
yatakiwa iwachukulie hatua wauaji
Historia ya Msikiti wa Ngaramtoni Silaha yetu
ni kura ya pamoja
Anuani
ya fikra
Tunahitaji
"UN' ya Waislamu!
Kongamano la wanawake wa Kiislamu Newala lafana Umuhimu
wa Elimu ya Awali kwa watoto wadogo - 2
Kesi mojawapo ya mihadhara yafutwa Wasaidieni watoto wenye vipaji - Prof. Kilonzo Mahafali ya kidato cha nne Thaqafa: Wazazi wakumbushwa wajibu wao Wanafunzi
Mwanza wadai haki za kuabudu mashuleni kwa usawa
Saidianeni katika shida - Sheikh Abdallah Waislamu, Wakristo Rufiji watakiwa kuunda umoja Someni muiokoe jamii kimaadili Kesi
nyingine ya Waislamu Mwembechai yaahirishwa
Kusilimu kwa Wakristo kwaleta kero Mwanza Nzasa waomba msaada wa chakula, madawa Katibu wa Bakwata Moro ang'olewa Msikitini Chakula
na lishe
|