AN-NUUR 
Na.176 Shaaban  1419, Novemba 20 - 26, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Historia ya Msikiti wa Ngaramtoni
 

TANGU awali Msikiti wa Ngaramtoni ndio Msikiti wa Mtaa na waumini wake ndiyo wa mtaa wa Ngaramtoni, hivyo ilikuwa uongozi wa Msikiti ndiyo huo wa Mtaa. 

Mwanzoni waumini wachache wenyeji wa Ngaramtoni hawakuwa na Msikiti hadi pale uongozi ulivyanza kuchaguliwa baada ya kuundwa Bakwata mwaka 1968. 

Katika uchaguzi wa awali, Sheikh Ally Almasi alichaguliwa Sheikh wa Msikiti na Mtaa, Sheikh Juma Shaabani Katibu wa Msikiti na Mtaa. 

Na Sheikh Othman Salim alichaguliwa Makamu Mwenyekiti wa Msikiti wa mtaa kwenye miaka ya 70 baada ya waumini kukosa sehemu/Msikiti kwa kufanyia ibada. 

Mzee Bawazir anayeishi hapa mjini Arusha aliwahi kununua nyumba ya biashara kwa Mzee John Mkingo ambayo baadaye aliitoa Waqfu. 

Aliyekuwa Katibu Mzee Juma na pia fundi mjenzi waliirekebisha nyumba hiyo kuanzia chini kwa kutumia paa lililokuwepo na wakaanza kuitumia kama Msikiti. 

Baadae palitokea kero za jirani ambae alijenga kilabu na kupitisha maji machafu sambamba na mpaka wa Msikiti. Baada ya kero hiyo kukosa ufumbuzi Muislamu mmoja aitwaye Mohammed Gahir alinunua eneo (kiwanja) kwa thamani ya shilingi 4,000 kwa ajili ya kujengwa Msikiti kuepukana na kero za majirani wa Msikiti wa awali. 

Baada ya kupatikana kiwanja hicho Sheikh Abdulwalii aliyekuwa amehamia Ngaramtoni na mzee mwingine kwa jina moja Mbwana walitumwa na uongozi kwenda Dar es Salaam kuchangisha fedha za kujenga Msikiti na baada ya harakati hizo Msikiti ulikamilika ambao ndiyo Msikiti uliopo hadi leo. 

Katika mabadiliko mbalimbali ya uongozi wamekuwepo waliochaguliwa tofauti wakiwemo kina Sheikh Mohammed Kisiwa. 

Kila aliyepiga vita uganga na kula mali za Waislamu ilifanywa juu chini aondolwe. Tatizo jingine kubwa ni kwamba wapo watu wanaodai Msikiti ni wao (Waarabu na Wasomali) kwa kuwa Msomali ndiye aliyenunua kiwanja na Mwarabu ndiye aliyekwenda Dar es Salaam kuchangisha fedha za ujenzi. 

Kwa ajili hiyo wanadai kwamba wao ndiyo wenye mamlaka ya kuwachagulia waumini viongozi kupitia vigezo vyote hivyo wamekuwa wakilinda maslahi binafsi kama kutopenda kukosolewa. 

Baada ya waumini na hasa chini ya uongozi wa mtaa uliopo kuchoka na kuikataa hali hiyo, pamekuwepo na nia ya kuirekebisha. Jitihada walizozifanya hao watu wachache ni kuwapiga marufuku Waislamu kuwahutubia waumini Msikitini na ili kufanikisha hilo wamekuwa na mahusiano ya karibu na Polisi wa kituo cha Ngaramtoni. 

Katika tukio la hivi karibuni walipofika kundi la Tabligh Msikitini na wakaamriwa kuswali tu na hawakupewa ruhusa ya kuzungumza lolote Msikitini hapo. Baada ya kuarifiwa hilo waliondoka na njiani wakakutana na Sheikh Shaaban Juma Lulu, Sheikh wa Mtaa. 

Sheikh aliwauliza sababu ya kuondoka. Baada ya kufahamishwa alirudi nao na baada ya swala aliwatahadharisha waumini juu ya tabia sugu yakuwazuia wageni kuwanasihi waumini wenzao. 

Waumini nao hawakuafiki chuki za wachache wanaofanya njama za kuwaondoa waalim/maimamu ambao hawaendani na maslahi yao. 

Baada ya hapo waliondoka. Watu hao wachache na walimwita OSS na kutaka amchukulie hatua Sheikh Shaabani Juma Lulu. 

Siku iliyofuata OSS alimtumia wito Sheikh Shaaban kwenda kituoni na huko alimtahadharisha kuchukuliwa hatua kali kwa kuwavuruga waumini Msikitini na kwamba yeye aswali tu. Walitofautiana jinsi gani anawavuruga waumini. 

Iliamriwa Sheikh akamatwe na akawekwa rumande kituoni na baada ya viongozi na waumini kuandamana huko kituoni walimwekea dhamana na kituoni aliandikiwa tuhuma ya kuvuruga mkutano wa waumini. 

Baadae alipelekwa mahakamani na kusomewa shitaka la kuhatarisha amani na utulivu kwa waumini wa Ngaramtoni kwa kuwagawa waumini waliokuwa kwenye mkutano. 

Sheikh alipelekwa mahabusu gereza la mjini Arusha hadi pale taratibu za dhamana zilipokamilishwa baada ya siku tatu na Sheikh kutolewa mahabusu. 

 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
Maoni 
Kuwa na mawazo ya kufugwa tunajidharaulisha 

Sakata la mabucha  ya Nguruwe kuibuka upya 
Na Mwandishi Wetu  

Kondom sio kinga ya Ukimwi 

Bakwata yairushia polisi makombora Ngaramtoni 

MACHO YA SHUTUMA 
Na Abu Halima Sa Changwa 

Serikali yatakiwa iwachukulie hatua wauaji 
Na Mwandishi Wetu 

Historia ya Msikiti wa Ngaramtoni 

Silaha yetu ni kura ya pamoja 
Na Alhaj Yusuf Kalala, Washington DC  U.S.A 

Anuani ya fikra 
Na Abu Halima Sa Changwa 

Kuukaribisha mwezi mtukufu 

Tunahitaji "UN' ya Waislamu! 
Na Said  Rajab 

Kongamano la wanawake wa Kiislamu Newala lafana 

Umuhimu wa Elimu ya Awali kwa watoto wadogo - 2 
Na Ustaadh Kupa Pazi Said 

Kesi mojawapo ya mihadhara yafutwa 

Wasaidieni watoto wenye vipaji - Prof. Kilonzo 

Mahafali ya kidato cha nne Thaqafa: Wazazi wakumbushwa wajibu wao 

Wanafunzi Mwanza wadai haki za kuabudu mashuleni kwa usawa 
Na Iddi M. Katiba, Mwanza 

Saidianeni katika shida - Sheikh Abdallah 

Waislamu, Wakristo Rufiji watakiwa kuunda umoja 

Someni  muiokoe jamii kimaadili 

Acheni Shirki 

Kesi nyingine ya Waislamu Mwembechai yaahirishwa 
Na Muhibu Said 

Kusilimu kwa Wakristo kwaleta kero Mwanza 

Nzasa waomba msaada wa chakula, madawa 

Katibu wa Bakwata Moro ang'olewa Msikitini 

Masomo ya Dini ya Kiislamu  

Barua za Wasomaji 

Mashairi 

Chakula na lishe 
[Umuhimu wa chakula katika shule za awali]  

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita