|
|
|
Mwenyezi Mungu (s.w.) anatufahamisha kwamba: "Enyi mlioamini mmelazimishwa kufunga (swaumu) kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu". (Qur. 2:183). Maneno haya matukufu yana mafunzo makuu matatu. Kwanza, kufunga ni amri wala si jambo la hiari. Pili, kutokana na maslahi yanayopatikana katika funga, maslahi ambayo ni muafaka kwa maumbile ya binadamu, amri hii pia inawahusu wanadamu waliokuwepo kabla yetu. Tatu, tunafahamishwa kuwa, kwa kuitekeleza amri hii tutalifikia lengo la kuumbwa kwetu. Lengo ambalo tusingelifahamu bila ya kuelimishwa na Mwenyezi Mungu (s.w.) pale alipotuambia kuwa: "Sikuwaumba majini na wanaadamu ila wapate kuniabudu" ( Qur’an 51:56) Ni vipi Mwenyezi Mungu (s.w) anatutaka tumuabudu katika mwezi wa Ramadhani? Je, hii ina maana kuwa katika miezi mingine ya mwaka hatutakiwi kumuabudu/kumtii Mwenyezi Mungu (s.w.)? Jawabu la swali la kwanza tutalipata katika toleo namba 4 la mfululizo wa makala hizi kuhusu funga ya Ramadhani. Ama jawabu la swali la pili ni kuwa, tunatakiwa kumuabudu/kumacha Mwenyezi Mungu (s.w.) kwa masaa yote 24 ya kila siku na katika kila kipengele cha maisha yetu kwa mwaka mzima. Pili tunatakiwa kumcha Mwenyezi Mungu kwa juhudi zetu zote hata mauti yatukute tukiwa Waislamu wa kweli. "Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu kama ipasavyo kumcha; wala msife isipokuwa mmekwisha kuwa Waislamu kamili". (3:102) Na katika kumtii Mwenyezi Mungu tunatakiwa tusichague baadhi ya mambo na kuacha mengineyo, bali, ni kufuata amri zote au kwa maneno mengine ni kutii kila kipengele kilichopo katika maisha yetu. "Enyi mlioamini! Ingieni katika hukumu za Uislamu zote, wala msifuate nyayo za shetani; kwa hakika yeye kwenu ni adui dhahiri". (2:208) Kama utaratibu wa kumuabudu Mwenyezi Mungu (s.w.) ndio huu, inakuwaje Allah (s.w.) atuamrishe kufunga Ramadhani ili tupate kumuabudu? Kuna hekima gani katika mwezi wa Ramadhani tofauti na miezi mingine? Jawabu ni kuwa, katika mwezi wa Ramadhani tunapewa/kutunukiwa nafasi ya pekee. Nafasi ambayo kama tutaitumia ipasavyo itatusaidia kulifikia lengo la kuumbwa kwetu kwa urahisi zaidi. Kuhusu kheri zinazopatikana ndani ya mwezi wa Ramadhani, Nabii Muhammad (s.a.w.) anasema: "Mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa Mwenyezi Mungu ambao ameujaza Rehma, Baraka na Msamaha". Na pia ni ukweli usio na shaka kuwa, kwa kutokuzingatia taratibu za mwezi wa Ramadhani tutakuwa ni wenye kuipoteza tunu hii, hivyo, kwa wenye hasara kubwa duniani na akhera. Mwezi wa Ramadhani unatupa nafasi ya kuanza maisha mapya na kujiwekea malengo bora zaidi kwa mwaka ujao. Endapo utakuwa umebahatika kuifahamu tunu hii na kuitekeleza ni kheri kwako. Endelea na ongeza juhudi. Na endapo utakuwa huifahamu tunu hii, basi hujachelewa bado, wakati ni huu; utumie na usiupoteze. Yanayofaa kujiandaa Tujipe mazoezi ya funga za sunnah kwa mfano: Jumatatu na Alhamisi, masiku meupe, masiku ya kiza na nyinginezo nyingi. "Aysha (r.a.) amesimulia kuwa Mtume wa Allah alikuwa akifunga (katika mwezi wa Shaabani) mfululizo mpaka tuseme hatafungua tena; na aliacha kufunga mfululizo mpaka tuseme hatafunga tena; na sikumuona Mtume wa Allah akifunga mwezi mzima, ila mwezi wa Ramadhani na sikumuona anafunga mwezi mwingine zaidi kuliko alivyokuwa akifunga mwezi wa Shaabani. (Muslim) Tujiandae kwa mahitaji muhimu katika mwezi wa Ramadhani kama vile; futari, daku, sadaka, zakatul-fitri na mengineyo muhimu. Tujiwekee malengo la kutekeleza ibada za ziada (sunnah) zilizotushinda mwaka uliopita, pia tujiwekee malengo ya kutekeleza majukumu muhimu maishani kwa mwaka unaofuata. Tahadhari: Tusijiwekee malengo mengi ambayo yatatushinda kutekeleza. Tujiwekee malengo makuu mawili au moja ili tutakapofanikisha tupate motisha ya kujiongezea mengine. Tujiwekee nia ya kutorudia tena kwenye maasi. Mtume wa Allah (s.w.) amesema: "Yeyote anayedhamiria kufanya jambo jema lakini hakufanikiwa kulifanya, anaandikiwa malipo (kama aliyefanya). (Bukhari na Muslim). Tujiweke vema na jamaa, ndugu au majirani ambao ilitokea hitilafu baina yetu. Tufuatilie mapema kalenda ya Kiislamu ili siku ya kuanza kufunga isitukute kwa mshtuko au kama ajali. Kwa kifupi tujiandae kwa kutekeleza yale yote yanayomfurahisha Mwenyezi Mungu; na tujiepushe kabisa na yote yasiyompendeza Allah (s.w.) Yasiyofaa katika kujiandaa Tuepukane na pumbao zote kama vile; kununua karata mpya ama kupangusa vumbi karata zilizosahaulika, kutafuta madrafti na kuyapaka rangi, kutafuta bao, kete, dhunna, kanda za mipasho (taarabu), manyanga na vigoma vya kula daku, na kadhalika. Michezo yote hii ni haramu; haifai, kwa sababu ni ya kupumbaza akili tu, na kumfanya binadamu asahau kushughulikia mambo yaliyo muhimu katika dunia na akhera yake. Tusijiandae kupandisha bei bidhaa muhimu zinazohitajika katika mwezi wa Ramadhani. Tupunguze bei kwa kukusudia kutoa sadaka nyingi. Tusijiandae kwa vunja jungu. Tunawezaje kukaribisha neema kwa kumkasirisha anayetuletea? Tukimkadhibisha anayetaka kutuzawadia ni vipi tunarajia zawadi kutufikia? Wenye tabia hii ya vunja jungu ni wale wanaokusudia kulifinyanga upya baada ya mwezi wa Ramadhani. Yaani wale wanaokusudia kurudia tena upotovu. Kwa maoni, maswali au mapendekezo, tafadhali tuandikie: Waandishi (Funga ya Ramadhani),
|
YALIYOMO
Maoni Kuwa na mawazo ya kufugwa tunajidharaulisha Sakata la
mabucha ya Nguruwe kuibuka upya
Bakwata yairushia polisi makombora Ngaramtoni MACHO YA
SHUTUMA
Serikali
yatakiwa iwachukulie hatua wauaji
Historia ya Msikiti wa Ngaramtoni Silaha yetu
ni kura ya pamoja
Anuani
ya fikra
Tunahitaji
"UN' ya Waislamu!
Kongamano la wanawake wa Kiislamu Newala lafana Umuhimu
wa Elimu ya Awali kwa watoto wadogo - 2
Kesi mojawapo ya mihadhara yafutwa Wasaidieni watoto wenye vipaji - Prof. Kilonzo Mahafali ya kidato cha nne Thaqafa: Wazazi wakumbushwa wajibu wao Wanafunzi
Mwanza wadai haki za kuabudu mashuleni kwa usawa
Saidianeni katika shida - Sheikh Abdallah Waislamu, Wakristo Rufiji watakiwa kuunda umoja Someni muiokoe jamii kimaadili Kesi
nyingine ya Waislamu Mwembechai yaahirishwa
Kusilimu kwa Wakristo kwaleta kero Mwanza Nzasa waomba msaada wa chakula, madawa Katibu wa Bakwata Moro ang'olewa Msikitini Chakula
na lishe
|