|
|
| Sakata
la mabucha ya Nguruwe kuibuka upya:
Waislamu watoa onyo la mwisho Serikali nayo yachukua tahadhari WAISLAMU na wananchi waishio Mwembe Madafu kata ya Ukonga wametishia kuchukua hatua mkononi endapo malalamiko yao dhidi ya uchomaji mishikaki katika maeneo yao hayatasikilizwa na vyombo vya dola. Wakiongea na gazeti hili, wananchi hao wamedai kwamba pamekuwa na uuzaji holela na uchomaji nyama ya nguruwe bila ya kuzingatia imani na hisia za wengine. Taarifa ya wajumbe saba wa mashina ya kata hiyo imedai kwamba Chaki amekuwa akiuza nyama ya nguruwe pamoja na mishikaki yake karibu na eneo la Msikiti. Aidha, wamesema kwamba hapo hapo anapouzia nyama ya nguruwe huuzwa pia Chips ambazo hununuliwa na watu mbalimbali wapita njia. Wajumbe hao Selemani Baridi, Mmasi Jihad Komba, Hassan Muhenga, Abdallah Hassan na Venant Baridi wameitahadharisha serikali ya mtaa ilifikishe suala hilo ngazi za juu na hatua za haraka zichukuliwe kabla ya kutokea matatizo. Katika kufuatilia suala hilo, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa - Mwembe Madafu Bw. T.F. Komba amemuamuru Bw. Chaki kuacha mara moja uchomaji huo wa nyama ya nguruwe katika eneo hilo. Katika barua yake ya Novemba 13, ameeleza kwamba mazingira anayochomea nyama hiyo ya nguruwe hayafanani na biashara hiyo na zaidi hata leseni hana. Aidha, barua hiyo imesema kwamba kwa kuwepo karibu na Msikiti na kuchanganya chips, kuku na nguruwe ni kukaribisha matatizo ya kuharibu amani na usalama wa raia. Ni kwa sababu hiyo barua ya serikali ya Mtaa imemalizia kwa kumwambia Bw. Chaki "Unaamriwa ... acha mara moja kuchoma nyama ya nguruwe, vinginevyo hatua kali dhidi yako zitachukuliwa". Hata hivyo, barua hiyo haikufafanua ni hatua zipi zingechukuliwa. Sakata ya uvunjaji wa bucha za nguruwe Jijini Dar es Salaam mwaka 1993 ilitokea baada ya malalamiko ya maimamu wa Misikiti kupuuzwa na serikali. Upuuzaji huo uliwapelekea waathirika kuchukua sheria mkononi. Kutoka uvunjaji wa bucha sakata hiyo ilichukua sura mpya na kufanywa operesheni maalum dhidi ya Waislamu walioitwa wa siasa kali. Operesheni hiyo iliharibu mahusiano kati ya Waislamu na serikali yao
na zaidi kati ya Waislamu na Chama Cha Mapinduzi.
|
YALIYOMO
Maoni Kuwa na mawazo ya kufugwa tunajidharaulisha Sakata la
mabucha ya Nguruwe kuibuka upya
Bakwata yairushia polisi makombora Ngaramtoni MACHO YA
SHUTUMA
Serikali
yatakiwa iwachukulie hatua wauaji
Historia ya Msikiti wa Ngaramtoni Silaha yetu
ni kura ya pamoja
Anuani
ya fikra
Tunahitaji
"UN' ya Waislamu!
Kongamano la wanawake wa Kiislamu Newala lafana Umuhimu
wa Elimu ya Awali kwa watoto wadogo - 2
Kesi mojawapo ya mihadhara yafutwa Wasaidieni watoto wenye vipaji - Prof. Kilonzo Mahafali ya kidato cha nne Thaqafa: Wazazi wakumbushwa wajibu wao Wanafunzi
Mwanza wadai haki za kuabudu mashuleni kwa usawa
Saidianeni katika shida - Sheikh Abdallah Waislamu, Wakristo Rufiji watakiwa kuunda umoja Someni muiokoe jamii kimaadili Kesi
nyingine ya Waislamu Mwembechai yaahirishwa
Kusilimu kwa Wakristo kwaleta kero Mwanza Nzasa waomba msaada wa chakula, madawa Katibu wa Bakwata Moro ang'olewa Msikitini Chakula
na lishe
|