AN-NUUR
Na.165 Jamadul Awwal 1419, Septembe 4 - 10, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Mafundisho ya Qur’an 

Mfalme aliyehojiana na Ibrahim kuhusu Mungu Muumba 

Aya ya 258 

HUKUSIKIA yule aliyehojiana na Ibrahimu juu ya Mola wake kwa sababu Allah alimpa ufalme? Ibrahimu aliposema, "Mola wangu ni yule ambaye huhuisha na hufisha", na yeye akasema: "Mimi pia nahuisha na kufisha". Ibrahimu akasema: "Allah hulichomozesha jua mashariki, basi wewe lichomozeshe magharibi". Akafedheheka yule aliyekufuru; na Allah hawaongozi watu madhalimu. 

Baada ya Allah (sw) kuelezea kuwa wanadamu wako wale wanaoongozwa na yeye mwenyewe na kupata ulinzi wake na wako wengine wanaoongozwa na Matwaghuut na kuwasukumiza kwenye upofu; sasa anatoa mifano ya makundi hayo mawili katika aya hii na mbili zinazofuata. 

Mfalme anaetajwa hapa ni Namrudh ambaye alikuwa ni mfalme wa Iraq ambamo Nabii Ibrahimu (as) alizaliwa na kukulia humo. Pamoja na kuwa Nabii Ibrahimu (as) alizaliwa katika nyumba ya kiongozi mkubwa wa dini ya nchi hiyo, msimamo wake, kwa kweli ulikuwa ni tofauti na unaopingana na dini ya baba yake na mfumo mzima wa kisiasa na kiutawala wa nchi hiyo. Mfumo wa dini (maisha na uendeshaji wa ) nchi hiyo ulikuwa na mambo yafuatayo kwa mazingatio ya msomaji: 

Kwa kuwa jamii hiyo ilikuwa ya kishirikina ilikuwa inaamini kuwepo kwa Allah kama Mungu wa Waungu wote na Bwana wa Mabwana. Hata hivyo bado walikuwa na Waungu wengine wadogo wadogo ambao alishirikishwa nao katika sifa zake, Uungu wake, mamlaka yake au hukumu zake. 

Uungu wa Allah (sw) uligawanywa katika nyanja mbii ili kutoa nafasi ya Uungu kwa Namrudh: 

Mungu Muumba asiyefikika na aliye nje ya upeo wa kawaida wa binadamu. 

Mamlaka ya Mungu yalivuliwa na kutengwa na Mungu Muumba na kuwekwa chini ya mfalme Namrudh. 

Katika nyanja ya kwanza, Allah alikumbukwa wakati wa shida na masahibu mengine yaliyo nje ya uwezo wa binadamu. Hata hivyo bado Allah aliwekewa wafu, majini, malaika, nyoka, milima, jua, mwezi na vitu vingine kuwa kama wasaidizi. Ibada zilifanywa kupitia waungu hao na siyo kwa Allah moja kwa moja. Kwa upande wa mamlaka ya Allah katika maisha ya kila siku ya wanadamu, jambo hili lilikabidhiwa kwa watawala ambao walishirikiana pamoja na familia za kifalme na makuhani au viongozi wa dini. Kwa sababu hii siku zote wakuu wa dini (viongozi wa mahekalu) walikuwa ni wapiga debe wakubwa wa mfumo huo wa utawala. 

Namrudh kwa upande wake alikuwa anafahamu kuwepo Mungu Muumba kwa ile maana ya kwanza na yeye mwenyewe kujidai Uungu katika nyanja ya pili. Siku zote alijidai Uungu kwa watu wake na kudai kuwa sheria na kauli yake nchini Iraq ndiyo ya mwisho na hakuna aliye juu zaidi yake. 

Mzozo au majadiliano yanayoelezwa katika aya hii yalitokea baada ya Nabii Ibrahim (as) kuyavunja masanamu na watu kushindwa katika masuala yao. Baba wa Nabii Ibrahim (Mzee Azar) katika kujikomba kwake baada ya kuvunjwa masanamu alikimbilia kwa Namrudh na kumkana mwanawe na ndipo alipoitwa Ibrahim mbele ya mfalme ili kuelezea hoja zake wazi wazi. Maelezo yaliyopo katika aya hii ndiyo mambo yaliyotokea kwenye ukumbi wa Namrudh wakati wa alipomuita Nabii Ibrahim (as). 

Maelezo yaliyomo katika historia ni kuwa huyu mfalme aliweza kufikia kwenye dai la pili baada ya kufanikiwa kimagube kulipindua dai la kwanza la Nabii Ibrahim (as). Baada ya kuambiwa na Nabii Ibrahim kuwa Mola wake (Ibrahim) anahuisha na kufisha naye Namrudh akadai hivyo kwa kuthibitisha kwa aina yake. Yeye hakuanzisha uhai kama afanyavyo Allah; bali aliagiza kuletewa wafungwa wawili ambao kwa sheria zake ilikuwa tayari wamekuhukumiwa kifo. Baada ya kufika aliamrisha mfungwa mmoja auliwe na wa pili aachiliwe huru. Kwa namna hii akajigamba kuwa ana uwezo wa kuhuisha na kufisha. Hoja ya pili ya Nabii Ibrahim haikuwa na mwanya kama ule wa kwanza nahivyo Namrudh alifedheheka kwani alijikuta hana namna ya kuburunda. 

Katika jitihada za kujikosha na kuthitibisha kuwa anaongozwa na Twaghuut pamoja na yeye mwenyewe kuwa Twaghuut aliamuru Nabii Ibrahim awekwe ndani kwa kipindi fulani na kisha kutoa hukumu ya kuchomwa moto. Ingawa Nabii Ibrahim (as) alitoka ndani ya moto huo salama lakini alipata agizo la Mola wake kuondoka Iraq na kwenda sehemu nyingine kuendelea na kazi yake ya kuwalingania wanadamu kwenye njia ya Allah ambayo ni Uislamu. 
 

Juu 
 

YALIYOMO
 
 

 TAHARIRI 
HAKI YA KUABUDU MASHULENI: Hoja ya uwingi isizuie haki ya wachache 

Aliyeandika Yesu si Mungu bado akabiliwa na kesi 
Na Mwandishi Wetu 

Wazazi walia na Mkuu wa shule Mkwawa 
Na Mwandishi Wetu, Iringa 

Serikali iache kudhulumu  Waislamu - Bakwata  
Na Mwandishi Wetu

KESI YA MIRATHI: Hukumu ya Jaji Agostino yatupwa 
Na Mwandishi Wetu 

Sumaye sasa atoa ‘waadhi’ Msikitini 
Na Mwandishi Wetu, Arusha 

Sekondari ya Kiislamu Sumbawanga, mtihani kwenu – Sheikh Akilimali 
Na Harun Rashid, Sumbawanga 

37 wasilimu  Mwanza 
Na Mwandishi Wetu, Mwanza 

Akamatwa kwa kusoma gazeti la ANNUUR ! 

MGOGORO WA CHWAKA NA MARUMBI: Serikali ya Dk. Salmin itafute ufumbuzi 
Na Mwandishi Wetu, Pemba 

MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA - 4 

Kwa nini walengwa wa mabomu wawe ni Marekani? 
Na Maalim Ali Bassaleh 

Profesa amekosea kusema kwamba... 
Na A.M. Hamza 

Ugaidi ni ugaidi, hata wa Marekani ni ugaidi 
Na Maalim Ali Bassaleh 

Dhana ya Udugu wa kiislamu 

UGAIDI: Chanzo si magaidi, ni dhuluma ya Marekani 
Na HASSAN KIMANGALE 

Jengeni familia bora 
Na Abuu Said, Iringa 

Tuwasaidie Waislamu kielimu na kiuchumi - Bi Zuhura 
Na SAID RAMADHANI KISSIMBA 

Tumieni uhuru wenu vyema 
Na Abuu Zaina, Iringa 

Hoja za kutofautisha Yesu na Issa ni udhaifu,  ni uzushi mtupu! - 4  
Na Muhibu Said 

Mihadhara ya Wakristo yatawala Handeni 
Na Mwandishi Wetu, Handeni 

Ziara ya Kadinali Pengo Moro  
Na Mussa Ally, Morogoro 

Aonyesha ujuzi wa kutengeneza Trekta 
Na Mwandishi Wetu 

Waislamu wasizifanye sharia za dini kuwa nzito – Sheikh Mzonge 
Na Ashraf  Yusuf, Moshi 

Sengerema waomba msaada 
Na Idd Katimba, Mwanza 
 
Mafundisho ya Quran 

Barua za wasomaji 

Mashairi: 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na Lishe 
Matunzo ya mtoto mwenye lishe duni 

Matangazo 
 

 

 

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita