|
|
| Dhana
ya Udugu wa kiislamu
Mafungamano ya Imani katika Uislamu yana haki, thamani na uzito zaidi kuliko udugu wa damu, nasaba,ukoo, kabila, Taifa au udugu wa aina nyingine yoyote ile: Hakika waumini wote ni ndugu" (49:10). Uzito wa mafungamano hayo ya kiimani umezingatia udugu wa Wanaadamu wote kwamba wanatokana na baba na mama mmoja, yaani asili moja na wote wanaiwania hatima moja. Umoja na udugu wa binaadamu unatokana na hao binadamu kuwa ni kizazi cha Adamu na Hawa. Kila binadamu ni memba wa familia hii, na hivyo kila memba anastahiki kupata haki zake katika familia hii kama alivyopia na dhima ya kutimiza wajibu wake. Udugu wa kiimani haukomei katika kuwa na asili moja bali pia katika kuwa na lengo na nafasi moja hapa ulimwenguni, Mwenyezi Mungu anatufahamisha katika Qur’an: (7:172), (49:13). Upeo huu mpana wa Qur’an kuhusu asili ya mwanaadamu, ndiyo kiini cha udugu mzito wa kiimani katika Uislamu. Udugu huo unaimarika zaidi ndani ya makundi ya harakati za Kiislamu yenye madhumuni ya kufanya mageuzi ya Kiislamu katika jamii. Mageuzi ambayo si tu yatasimamisha haki bali pia yatajenga na kuboresha utu, mahusiano na maaingiliano ya wanajamii chini ya mfumo mpya wa sera na itikadi inayokwenda sambamba na maadili yake, yaliyofunzwa na kudhibitiwa na mjuzi, makamilifu na Muumba wa vyote. Kujenga udugu na mafungamano haya ya kiimani kwahitajia mazoezi ya muda mrefu yenye kuandamana na hatua mbali mbali za utekelezaji na ufuatiliaji. Kuhusu msisitizo wa udugu wa kiimani katika kujizatiti kuondoa dhulma Qur’an yatueleza: Enyi mlioamini shikeni hadhari zenu, tokeni(kwenda vitani) mmoja mmoja au kwa pamoja. (4:71) Na mna nini hampigani katika njia ya Mwenyezi Mungu na (katika kuwaokoa)
wale walio dhaifu katika wanaume na wanawake na watoto ambao husema Mola
wetu! tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhalimu na utujaalie tuwe
na ulinzi unaotoka kwako na tujaalie tuwe na kutunusuru anaetoka kwako"
(4:7).
|
TAHARIRI HAKI YA KUABUDU MASHULENI: Hoja ya uwingi isizuie haki ya wachache Aliyeandika Yesu si Mungu bado akabiliwa
na kesi
Wazazi walia na Mkuu wa shule
Mkwawa
Serikali iache kudhulumu
Waislamu - Bakwata
KESI YA MIRATHI: Hukumu ya
Jaji Agostino yatupwa
Sumaye sasa atoa ‘waadhi’ Msikitini
Sekondari ya Kiislamu Sumbawanga,
mtihani kwenu – Sheikh Akilimali
37 wasilimu Mwanza
Akamatwa kwa kusoma gazeti la ANNUUR ! MGOGORO WA CHWAKA NA MARUMBI: Serikali
ya Dk. Salmin itafute ufumbuzi
MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA - 4 Kwa nini walengwa wa mabomu wawe ni
Marekani?
Profesa amekosea kusema kwamba...
Ugaidi ni ugaidi, hata wa Marekani
ni ugaidi
UGAIDI: Chanzo si magaidi, ni dhuluma
ya Marekani
Jengeni familia bora
Tuwasaidie Waislamu kielimu
na kiuchumi - Bi Zuhura
Tumieni uhuru wenu vyema
Hoja za kutofautisha Yesu na Issa
ni udhaifu, ni uzushi mtupu! - 4
Mihadhara ya Wakristo yatawala Handeni
Ziara ya Kadinali Pengo Moro
Aonyesha ujuzi wa kutengeneza
Trekta
Waislamu wasizifanye sharia
za dini kuwa nzito – Sheikh Mzonge
Sengerema waomba msaada
Chakula na Lishe
|