AN-NUUR
Na.165 Jamadul Awwal 1419, Septembe 4 - 10, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Hoja za kutofautisha Yesu na Issa ni udhaifu, ni uzushi mtupu! - 4 

Na Muhibu Said 

Kuhusu huyo Roho Mtakatifu aliyetabiriwa na Yesu bado ni Nabii Muhammad (s.a.w) kwa kuwa lipo sharti moja muhimu alilolitaja Bwana Yesu la kuondoka kwanza yeye (Yesu) ndipo huyo msaidizi mwingine aje. Na Mtume Muhammad (s.a.w) alitumwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t) pamoja na mambo mengine alikuja kutangaza kwamba ndiye Nabii aliyebashiriwa kuja kwa Nabii Isa au Yesu (a.s.). Yesu alisema: 

"Lakini mimi nawaambia iliyokweli, yawafaa ninyi mimi niondoke kwa maana mimi nisipoondoka, huyo msaidizi hatakuja kwenu, bali mimi nikienda zangu nitampeleka kwenu". (Yohana 16:7). 

Kauli hiyo ya Yesu inatofautiana wazi na dai hilo la Bw. Augustine hasa tunaporejea katika maandiko mengine mengi ya Biblia yanayoonyesha kwamba Roho Mtakatifu wanayemfikiria Wakristo alikuwepo hata kabla Yesu hajazaliwa (Marko 12:36), kabla Yesu hajaondoka (Yohana 20:22-23), mama yake (Yesu) alichukua mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu (Luka 1:35) n.k. 

Kuhusu kudumu kwa huyo msaidizi kusudio lake siyo lazima Mtume Muhammad (s.a.w) awepo pamoja nasi kimwili. Lakini kudumu kwa usahihi kwa mafundisho yake ni hoja tosha ya kukiri kwamba Mtume Muhammad (s.a.w) yupo pamoja nasi daima. (Qur’an 2:154). 

Hii inafanana na ile kauli ya Yesu alipowaambia wafuasi wake kwamba: "…Natazama, mimi niko pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. (Mathayo 28:20). Hii haina maana kuwa leo Yesu tuko pamoja naye duniani kimwili. 

Lakini watu walio duniani, lakini wakawa hawana faida wala manufaa yoyote kwa mwanadamu, watu kama hao ndio Bwana Yesu aliowaita kwamba ni "wafu" japokuwa wanapumua. (Mathayo 8:21). 

Kwa mantiki hiyo, ni dhahiri kuwa Yesu ndiye Isa aliyemtabiri Nabii Muhammad (s.a.w) kama nilivyoonyesha hapo juu kinyume na anavyopotosha Bw. Augustine. 

Bw. Augustine anaendelea kudai "Qur’an inasema Isa alitoa zaka (19:31). Katika Biblia hakuna sehemu yoyote ya aya inayosema Yesu alitoa zaka. Je, huoni kuwa nayo ni tofauti?" Mwisho wa kunukuu. 

Kama nilivyokwishabainisha hapo juu kwamba, Mwinjilisti Yohana amekwishaeleza kwamba "kuna mambo mengine mengi aliyoyafanya Yesu ambayo hayakuandikwa kwa kuhofia vitabu vingekuwa vingi sana duniani (Yohana 20:25). 

Kwa hiyo, jambo la Bwana Yesu kutoa zaka ni katika orodha ya mambo hayo ambayo hayakuandikwa katika Biblia. Na ndio maana Qur’an Tukufu ikalazimika kukumbusha kwamba "Nabii Isa au Yesu" aliusiwa na Mola wake kutoa zaka. (19:31) 

Haijulikani jambo zito na muhimu kama hilo lisizungumzwe na Biblia hasa ukizingatia kwamba Bwana ndiye mfano mwema kwa wafuasi wake katika kila fundisho la Mwenyezi Mungu! (Yohana 14:6). 

Kwa mantiki hiyo, dai hilo la Bw. Augustine bado halijamtofautisha Yesu na Isa mpaka tuyapate mambo yote aliyoyafanya Yesu. 

Bw. Augustine anaendelea kusema "Biblia inasema Yesu alisulubiwa na kufa msalabani na hatimaye kufufuka" (Mathayo 16:21). Qur’an 4:157 inakataa kusulubiwa, kufa na kufufuka kwa Isa. Je, huoni huyo Isa na Yesu ni wawili tofauti? Mwisho wa kunukuu. 

Aya hiyo (ya Mathayo 16:21) ya Biblia aliyoitaja hapo juu Bw. Augustine inatia shaka kuamini kwamba ni Yesu ndiye aliyetamka maelezo yake, kwani naamini kwamba Yesu kamwee hawezi kutabiri jambo kisha lisitokee. Mwandishi wa aya hiyo Bwana Mathayo Mtakatifu anasema: 

"Tangu wakati huo Yesu alianza kuonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa Makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka" (Mathayo 16:20). 

Pamoja na maelezo hayo, lakini ukisoma Mathayo 27:27 unakuta waliompa mateso, kumsulubu mpaka kufa ni askari wala siyo wazee, wakuu wa makuhani wala waandishi kama ilivyotabiriwa na aya hiyo (ya Mathayo 16:21). 

Kwa utata huo, ndio maana Qur’an Tukufu ikathibitisha kwamba "Hawakumwua wala hawakumsulubu". (4:157-158). Na huu ni ushahidi tosha unaothibitisha kwamba Nabii Isa wa Qur’an ndiye Yesu wa Biblia. 

Isingekuwa hivyo, Qur’an isingejishughulisha kabisa na suala la kukanusha madai ya Wakristo ya kusulubiwa, kufa na kufufuka kwa Nabii Isa au Yesu (a.s.). 

Mwisho, Bw. Augustine anasema "Qur’an (10:94) inawaelekeza Waislamu wenye mashaka kama ndugu yangu Muhibu Said wawaulize watu wa vitabu wa kabla yao (Wakristo). Kwa kutojua maandiko watuulize nasi (Wakristo) tutawafundisha. Elimu ya kiroho wenzetu hawanayo (17:85). Mwisho wa kunukuu. 

Napenda kumuelewesha Bw. Augustine kwamba watu wa vitabu wa kabla yetu tulioagizwa tuwaulize siyo Wakristo na mtu kama Augustine anayezua na kupotosha wazi maandiko na ukweli kwa ujumla. 

Kwanza Wakristo ni watu waliozuka miaka mitatu baada ya Bwana Yesu (Nabii Isa) kuondoka (Matendo 11:25-26). Ni Uislamu na Waislamu wamekuwepo tangu zama za Nabii Adamu (a.s.) (30:30, 2:213). Hivyo, watu waliokuwa kabla yetu siyo Wakristo, bali ni Mayahudi na Manasara waliokuwa wakiijua kweli iliyokuwemo ndani ya Torati, Zaburi, Injili na Nyaraka sahihi za Manabii na kuifuata. Watu hao ni ndugu zetu Waislamu walitutangulia na siyo Wakristo. 

Aidha, elimu ya roho ambayo binadamu wote (na si Waislamu peke yao) ambayo hawakuwepwa isipokuwa kidogo, ni elimu ya kuijua kiundani roho ile inayompa uhai kiumbe, na si elimu ya "kiroho" kwa maana ya "ujuzi wa mambo ya Mwenyezi Mungu" kama anavyopotosha Bw. Augustine hapo juu. (Tafadhali asome tena mara kwa mara aya hiyo). 

Hakuna mtu yeyote anayeweza kuonyesha japo picha ya roho yake ilivyo. Namsihi Bw. Augustine kwamba mara nyingine asipende kuchanganya mambo kwa kuingiza mada isiyohusika katika mjadala husika. 

Kwa upande mwingine, kama alivyozua makusudi katika gazeti la Msemakweli toleo la Juni 28 hadi Julai 4, 1998, kwamba Nabii Isa aliyemwita wa Qur’an alifufua na kisha kuua, nampa Bw. Elia Batendi miaka miwili aonyeshe aya hiyo ndani ya Qur’an Tukufu. Pia kama si uzushi wake, aonyeshe aya katika Qur’an inayosema kwamba Bi. Mariamu alichukua mimba siku ile ile na kumzaa Nabii Isa siku ile ile! 
 

Juu 
 

YALIYOMO
 
 
TAHARIRI 
HAKI YA KUABUDU MASHULENI: Hoja ya uwingi isizuie haki ya wachache 

Aliyeandika Yesu si Mungu bado akabiliwa na kesi 
Na Mwandishi Wetu 

Wazazi walia na Mkuu wa shule Mkwawa 
Na Mwandishi Wetu, Iringa 

Serikali iache kudhulumu  Waislamu - Bakwata  
Na Mwandishi Wetu

KESI YA MIRATHI: Hukumu ya Jaji Agostino yatupwa 
Na Mwandishi Wetu 

Sumaye sasa atoa ‘waadhi’ Msikitini 
Na Mwandishi Wetu, Arusha 

Sekondari ya Kiislamu Sumbawanga, mtihani kwenu – Sheikh Akilimali 
Na Harun Rashid, Sumbawanga 

37 wasilimu  Mwanza 
Na Mwandishi Wetu, Mwanza 

Akamatwa kwa kusoma gazeti la ANNUUR ! 

MGOGORO WA CHWAKA NA MARUMBI: Serikali ya Dk. Salmin itafute ufumbuzi 
Na Mwandishi Wetu, Pemba 

MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA - 4 

Kwa nini walengwa wa mabomu wawe ni Marekani? 
Na Maalim Ali Bassaleh 

Profesa amekosea kusema kwamba... 
Na A.M. Hamza 

Ugaidi ni ugaidi, hata wa Marekani ni ugaidi 
Na Maalim Ali Bassaleh 

Dhana ya Udugu wa kiislamu 

UGAIDI: Chanzo si magaidi, ni dhuluma ya Marekani 
Na HASSAN KIMANGALE 

Jengeni familia bora 
Na Abuu Said, Iringa 

Tuwasaidie Waislamu kielimu na kiuchumi - Bi Zuhura 
Na SAID RAMADHANI KISSIMBA 

Tumieni uhuru wenu vyema 
Na Abuu Zaina, Iringa 

Hoja za kutofautisha Yesu na Issa ni udhaifu,  ni uzushi mtupu! - 4  
Na Muhibu Said 

Mihadhara ya Wakristo yatawala Handeni 
Na Mwandishi Wetu, Handeni 

Ziara ya Kadinali Pengo Moro  
Na Mussa Ally, Morogoro 

Aonyesha ujuzi wa kutengeneza Trekta 
Na Mwandishi Wetu 

Waislamu wasizifanye sharia za dini kuwa nzito – Sheikh Mzonge 
Na Ashraf  Yusuf, Moshi 

Sengerema waomba msaada 
Na Idd Katimba, Mwanza 
 
Mafundisho ya Quran 

Barua za wasomaji 

Mashairi: 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na Lishe 
Matunzo ya mtoto mwenye lishe duni 

Matangazo 
 
 

 

 

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita