|
|
| Sumaye
sasa atoa ‘waadhi’ Msikitini
Na Mwandishi Wetu, Arusha WAZIRI Mkuu Mheshimiwa Frederick Sumaye amekariri msimamo wa serikali kwamba inaheshimu dini zote na kwamba serikali haina ugomvi na watu wa dini ili mradi tu dini isitumike kuleta vurugu nchini. Aidha, Waziri Mkuu alikumbusha na kusisitiza kwamba majengo ya Ibada yawe sehemu muhimu kutoa malezi kwa vijana. Mheshimiwa Waziri Mkuu ameyasema hayo hivi karibuni huko Hanang wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Msikiti Masjid N-nuur. Katika hali isiyo ya kawaida nasaha hizo za Mh. Sumaye zilikuwa zikisindikizwa
kwa makofi yaliyochanganyika na Takbir toka kwa wananchi waliohudhuria
hafla hiyo.
Sekondari ya Kiislamu Sumbawanga, mtihani kwenu – Sheikh Akilimali Na Harun Rashid, Sumbawanga WAISLAMU wa mjini Sumbawanga wamehimizwa kutumia uwezo wao wote kukamilisha ujenzi wa jengo litakalokuwa sekondari ya Kiislamu, ulioanza takriban miaka miwili iliyopita. Maneno hayo yalizungumzwa na Sheikh Rashid Akilimali mara baada ya sala ya Ijumaa Agosti 28, 1998 katika Msikiti Mkuu wa mjini Sumbawanga wa Qiblatain. Sheikh aliyasema hayo kufuatia ujenzi wa jengo hilo kuwa wa "mwendo wa kinyonga". Alisema kuwa idadi kubwa ya wafanyabiashara wakubwa wa mjini Sumbawanga ni Waislamu, hivyo aliwaomba wamkopeshe Mwenyezi Mungu kwa kutoa sadaka zao kuchangia ujenzi wa jengo hilo, kwani Mwenyezi Mungu hamdhulumu mja wake na humlipa kutokana na alichokitanguliza. "Inashangaza kuona wafanyabiashara wengi wako tayari kuchangia katika mambo ya kidunia kama vile mpira, ili wapate kusifika kutokana na uwezo wa kipesa, lakini inapokuja masuala ya kuendeleza Uislamu wanakuwa wazito katika kutoa michango yao", alisema Sheikh huyo. Pia aliwahimiza waumini hao wa mjini Sumbawanga kutokuwa wazito katika kutoa michango ya hali na mali ili kuleta maendeleo katika jamii ya Waislamu. Sheikh Akilimali alisema kuwa ni jambo linalotia uchungu kuona vijana wengi wa Kiislamu hawana elimu inayowafaa katika maisha yao, na kwa kutolelewa katika maadili ya Kiislamu kunachangia kuwafanya wengi wao kuwa vibaka, watumiaji wa madawa ya kulevya na mambo mengi ya kishenzi. Hivyo, aliwahimiza kuwa njia nzuri ya kuwanusuru vijana wa Kiislamu ni kumalizia ujenzi wa jengo hilo, ambapo litakapokamilika kuwa shule itapatikana hapo elimu ya ya Kiislamu na masomo mengine. Kwani alisema Sheikh huyo kuwa, vijana watakaokuwa na pande zote mbili za elimu, ndio watakaonusuru Uislamu na kuondoa kudhalilika kwa Waislamu kutokana na viwango vidogo vya elimu, kwa kuwa wakielimika kwa elimu zote mbili ndio watautetea vizuri Uislamu. Sheikh huyo alimalizia kwa kusema, Uislamu katika mkoa wa Rukwa ni mchanga bado hivyo, shule hiyo itakuwa chachu ya maendeleo ya Kiislamu hapa mkoani. "Waislamu kwa kuamua kujenga shule hiyo tayari tumeishaweka ahadi mbele ya Allah, hivyo tujiandae kwenda kujibu, iwapo tutashindwa kukamilisha ujenzi wa shule hiyo", alisema Sheikh Akilimali. Na aliwasihi waumini hao wa Sumbawanga kuwa kitu kimoja ili kutimiza
ahadi waliyomuahidi Allah.
37 wasilimu
Mwanza
Na Mwandishi Wetu, Mwanza IMEARIFIWA kwamba watu wapatao 37 walisilimu katika Ijitimai iliyomalizika mjini Mwanza hivi karibuni. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Amir Asadullaah waliosilimu ni kutoka madhehebu ya Katoliki, Lutherani na Sabato. Aidha, Amir Asadullah amesema kwamba baadhi ya Waislamu waliohudhuria Ijitimai hiyo walipata nusra ambapo walifungishwa ndoa hapo hapo katika uwanja wa Ijtimai. Awali, wakati wa hutubaa ya ufunguzi wa Ijtimai hiyo, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Alhaj Aboud Jumbe aliwaomba Waislamu kutokuwa wazito kuhudhuria mikusanyiko ya namna hiyo. Alisema kwamba kukutana Waislamu kuna faida nyingi zaidi ya zile za kiroho ambazo ndio lengo kuu. Wakati wa Ijitimai hiyo, mada mbalimbali zilifikishwa na wahadhiri toka humu humu nchini Tanzania, Kenya na Uganda. Mahudhurio yalikuwa ni zaidi ya watu elfu kumi na tano. Sheikh Salum Hassan Ferej Sheikh wa mkoa wa Mwanza alirudia wito alioutoa wiki mbili zilizopita mjini Sengerema wakati wa sherehe za Maulidi kimkoa kuwataka Waislamu kutambua mbinu zinazotumiwa na maadui wa Uislamu. Alisema kila kundi liheshimu juhudi za kundi jingine, kwani makundi yote yana lengo la kuinua Kalima ya Allah (sw) iwe juu na kushinda, aliwataka Waislamu mmoja mmoja na makundi yote kuwa kitu kimoja mara linapotokea jambo linalohusu kama umma mmoja. Akizungumza katika Ijitimai hiyo, Naibu Amir wa Baraza Kuu (M) Ustaadh Omar Mbalamwezi aliwakumbusha Waislamu kuchukua tahadhari ya matangazo mbalimbali ya biashara hasa za ulevi na zinazohimiza kufanya zinaa "salama" alikemea matangazo hasa ya pombe. "Taifa halina cha kuwarithisha ila ulevi, mbona kuna mbuga za wanyama, miti, milima, maziwa na mali nyingi za asili haturidhishwi ila ulevu tu…?" Alishangaa Ustadh Mbalamwezi. Aliwatahadharisha viongozi wakuu wa nchi kwa kufumbia macho mambo yanayochochea zinaa katika jamii. "Hakuna dalili za kupungua kwa maradhi ya ukimwi ila idadi ya waathirika inapanda kwa kasi ya ajabu". Alisema hakuna cha kutarajia zaidi ya wazinifu kuangamia kwa fedheha kubwa na vifo pamoja mabalaa chungu nzima. Katika kuhitimisha Ijitimai hiyo iliyofanyika katika kitongoji cha Igoma nje kidogo ya mji wa Mwanza, maazimio kadhaa ya shughuli za Tabligh yalipitishwa mojawapo ikiwa ni kujenga vituo vya kudumu kila mkoa. Taarifa ya jumla mara baada ya kufungwa kwa Ijitimai hiyo, ilisema kuwa kwa kuanzia tayari mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Kilimanjaro, Arusha na sasa Mwanza viwanja vimepatikana. Shughuli za ujenzi kwa kila mkoa zitakuwa chini ya Maamir wa Mikoa. Akielezea makusudio hasa ya vituo hivyo, Naibu Amir Mkuu Asadullah kupitia kwa Amir Benge’s alisema kuwa kila kituo kitakuwa na makazi ya makundi, shule za awali kwa elimu na vyuo vya ufundi ili kuwaandaa Waislamu mbalimbali kujitegemea kimaisha. Aidha, Ijitimai hiyo iliazimia kuimarisha makundi ya kwenda vijijini kuandaa umma; kuwaandaa Maamir pamoja na makundi yao kuitangaza dini ya Kiislamu kwa juhudi bila woga na kuwa na kamati za ujenzi wa vituo kila mkoa palipopatikana uwanja chini ya Maamir wa mikoa. Azimio lingine ni kuimarisha mawasiliano na makundi ya nje ya nchi kwa
karibu.
Akamatwa kwa kusoma gazeti la ANNUUR ! MZEE Hamis K. Msuya: "Tulikuwa tunasoma gazeti la ANNUUR
na wenzangu Hassan Hole na Idd Mhango, Katibu Tarafa alimpelekea Mkuu wa
Wilaya taarifa hiyo na Mkuu wa Wilaya alipeleka taarifa hiyo kwa Mkuu wa
Polisi wilayani (Singida mjini), naye alituma askari kuja kunikamata usiku
saa mbili Agosti 16, 1998 na kuniweka ndani (mahabusu) mpaka Agosti 19,
1998 kisha nikafikishwa mahakamani na kesi yangu imeahirishwa hadi Septemba
10, 1998".
|
TAHARIRI HAKI YA KUABUDU MASHULENI: Hoja ya uwingi isizuie haki ya wachache Aliyeandika Yesu si Mungu bado akabiliwa
na kesi
Wazazi walia na Mkuu wa shule
Mkwawa
Serikali iache kudhulumu
Waislamu - Bakwata
KESI YA MIRATHI: Hukumu ya
Jaji Agostino yatupwa
Sumaye sasa atoa ‘waadhi’ Msikitini
Sekondari ya Kiislamu Sumbawanga,
mtihani kwenu – Sheikh Akilimali
37 wasilimu Mwanza
Akamatwa kwa kusoma gazeti la ANNUUR ! MGOGORO WA CHWAKA NA MARUMBI: Serikali
ya Dk. Salmin itafute ufumbuzi
MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA - 4 Kwa nini walengwa wa mabomu wawe ni
Marekani?
Profesa amekosea kusema kwamba...
Ugaidi ni ugaidi, hata wa Marekani
ni ugaidi
UGAIDI: Chanzo si magaidi, ni dhuluma
ya Marekani
Jengeni familia bora
Tuwasaidie Waislamu kielimu
na kiuchumi - Bi Zuhura
Tumieni uhuru wenu vyema
Hoja za kutofautisha Yesu na Issa
ni udhaifu, ni uzushi mtupu! - 4
Mihadhara ya Wakristo yatawala Handeni
Ziara ya Kadinali Pengo Moro
Aonyesha ujuzi wa kutengeneza
Trekta
Waislamu wasizifanye sharia
za dini kuwa nzito – Sheikh Mzonge
Sengerema waomba msaada
Chakula na Lishe
|