|
|
| Ziara
ya Kadinali Pengo Moro:
Wazazi washutumu watoto wao kufanyishwa
kazi Kanisani
Baadhi ya wazazi mkoani Morogoro wamesikika wakilalamika kuwa watoto wao wanaosoma shule za msingi wamefanyishwa kazi Kanisani wakati wa maandalizi ya ujio wa Kadinali Pengo mkoani Morogoro. Wazazi hao wamedai kuwa wameshangazwa na hatua hiyo ambayo hata hivyo hawakuweza kueleza iliamriwa na nani, na wamedai kwamba kwa kufanya hivyo kumehujumu masomo ya watoto hao. Haikuweza kufahamika mara moja siku na makanisa ambayo watoto hao wamefanyishwa kazi hizo. Kadinali Policarp yuko katika ziara ya kutembelea mikoa mbalimbali nchini ambayo pamoja na mambo mengine atakayoyafanya ni kuwasalimia waumini wa Kanisa lake (Katoliki) kufuatia kurejea kwake toka Vatican ambako rasmi alivishwa wadhifa alionao sasa. Juhudi za gazeti hili kujua mahali ilipotoka amri wanafunzi hao wakafanya kazi za usafi Kanisani, hazikuweza kufanikiwa. Wakati huo huo, Kadinali Pengo alizuru mkoa wa Morogoro jioni ya Ijumaa Agosti 21, 1998 huku akiongozwa na msafara wa magari na pikipiki za polisi na kwa ving’ora na kupokelewa kwa nyimbo za pambio. Wiki moja kabla, magari ya kutengenezea barabara ambayo huonekana nyakati za uchaguzi, mbio za mwenge au ujio wa Rais Mkapa, yalianza kuvinjari katika barabara alizotarajiwa kupita Kadinali Pengo jambo ambalo limeacha maswali mengi yasiyo na majibu kwa wana Morogoro. Kufanyishwa kazi za Kanisa wanafunzi wa shule za msingi, kumekuja wiki
chache tu tangu pale Afisa Elimu Manispaa alipowataka walimu wakuu wamtayarishie
orodha ya wanafunzi Wakatoliki wa darasa, hii ikiwa umebakia muda mfupi
kabla ya mitihani ya mwisho haijaanza.
Aonyesha ujuzi wa kutengeneza Trekta Na Mwandishi Wetu KIJANA Athumani S. Tumbo wa Shule ya Sekondari ya Tayma iliyoko jijini Dar es Salaam amedai kuwa anao uwezo wa kutengeneza vitu (mashine) mbali mbali akipata mtu wa kumwendeleza. Mwanafunzihuyo ambaye amefika katika ofisi za gazeti hili na mojawapo ya mashine aina ya Tractor maarufu kwa jina la "kijiko" ambalo amelitengeneza mwenyewe kwa kutumia maboksi, betri kubwa tatu na moja ndogo na motor (motor) ya radio. Trekta hilo linapigwa stata kama kawaida ya magari mengine, linatumia rimoti ya kusogeza (kutembea) mbele na nyuma, kuinua mzigo na kumwaga mzigo ambao limebeba. Kijana huyo amesema huko nyuma alikuwa akisoma shule ya msingi Wilayani
Kilosa, aliwahi kutengeneza vitu mbali mbali kama feni ambayo ilikuwa inazunguka
kawaida.
Waislamu wasizifanye sharia za dini kuwa nzito – Sheikh Mzonge Na Ashraf Yusuf, Moshi WAISLAMU mjini Moshi na nchi nzima kwa ujumla wametakiwa kutozifanya sharia za dini kuonekana nzito kinyume na zilivyo. Hayo yalisemwa na Sheikh Ramadhani Hamza Mzonge katika khutba ya sala ya Ijumaa hivi karibuni katika Msikiti wa Al-Haramain mjini Moshi, huku akisikilizwa na mamia ya Waislamu waliohudhuria sala hiyo. Sheikh Ramadhani alisema Uislamu ni mwepesi, lakini umefanywa mzito na Waislamu wenyewe. Akitoa mfano wa wepesi wa sharia za dini ya Kiislamu alisema kuwa Muislamu anaweza kuswali sala yake popote alipo na akatia udhu kwa mchanga tu (akatayamamu) iwapo atakosa maji. Akitoa mfano alisema, msafiri anaweza akaacha kufunga saumu na hana makosa ili mradi aje kulipa. Akinukuu aya za Qur’an na tafsiri zake, Sheikh Ramadhani alisema msafiri wa Kiislamu ameruhusiwa kuchanganya sala mbili, na alasiri na adhuhuri au magharibi na isha zote mbili akazishwali kwa wakati mmoja (ima wakati wa Isha au Magharib) na sala zake zinakubaliwa bila wasiwasi. Akisisitiza juu ya dini ya Uislamu, Sheikh Ramadhani alisema Uislamu ndiyo dini ya Nabii Adam, Nuhu na Ibrahimu na hatimaye Muhammad (saw). Akinukuu aya ya Qur’an na hadithi alisema, "Na yeyote anayefuata dini kinyume na Uislamu, hakika atakuwa kesho ni mwenye hasara kubwa hivyo amepotea". Mwisho aliwahimiza Waislamu kutokuacha sunna za Mtume Muhammad (saw), alilikema kwa kusema hadithi ya Mtume isemayo "Mwenye kuacha suna zangu hatokuwa pamoja nami" alimalizia Sheikh Ramadhani. Sheikh Ramadhani ni Imamu wa Msikiti wa Al-Haramain hapa Moshi mjini
na ni mmoja wa viongozi wa dini maarufu hapa mkoani Kilimanjaro.
Na Idd Katimba, Mwanza Uongozi wa shule ya Sengerema Muslim School umewaomba Waislamu na viongozi mbalimbali kuwatembelea ili kubadilishana nao ujuzi wa kuendesha shule hiyo pekee ya Waislamu mjini Sengerema. Wito huo umetolewa na mmoja wa viongozi waanzilishi wa shule hiyo, Bw. Hamisi Hussein Mwagao. Akizungumza na AN-NUUR mjini Sengerema mbele ya shule hiyo hivi karibuni, alisema kuwa hali ngumu ya maisha imesababisha shule kuwa katika hali mbaya mno kutokana na wazazi wengi kushindwa kulipa ada na kuufanya uongozi wa shule kukabiliwa na gharama kubwa za uendeshaji. Akiungwa mkono na kiongozi mwenzake Ustadh Abdu Khalifa alisema kuwa watashukuru kama watapatikana wafadhili wa kwenda kuwaunga mkono ili kuihudumia vizuri shule kwa gharama mbalimbali. Shule hiyo ambayo iko chini ya bodi ya udhamini wa Sengerema Islamic Centre hadi sasa imefikisha darasa la tatu wakati lengo ni hadi darasa la saba. Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ni mwalimu Mariam Chande na hali kwa ujumla
inahitaji misaada na uangalizi wa karibu mno kwa kila aliyepewa jukumu
la kuongoza shule hiyo na wahusika wote kwa pamoja.
|
TAHARIRI HAKI YA KUABUDU MASHULENI: Hoja ya uwingi isizuie haki ya wachache Aliyeandika Yesu si Mungu bado akabiliwa
na kesi
Wazazi walia na Mkuu wa shule
Mkwawa
Serikali iache kudhulumu
Waislamu - Bakwata
KESI YA MIRATHI: Hukumu ya
Jaji Agostino yatupwa
Sumaye sasa atoa ‘waadhi’ Msikitini
Sekondari ya Kiislamu Sumbawanga,
mtihani kwenu – Sheikh Akilimali
37 wasilimu Mwanza
Akamatwa kwa kusoma gazeti la ANNUUR ! MGOGORO WA CHWAKA NA MARUMBI: Serikali
ya Dk. Salmin itafute ufumbuzi
MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA - 4 Kwa nini walengwa wa mabomu wawe ni
Marekani?
Profesa amekosea kusema kwamba...
Ugaidi ni ugaidi, hata wa Marekani
ni ugaidi
UGAIDI: Chanzo si magaidi, ni dhuluma
ya Marekani
Jengeni familia bora
Tuwasaidie Waislamu kielimu
na kiuchumi - Bi Zuhura
Tumieni uhuru wenu vyema
Hoja za kutofautisha Yesu na Issa
ni udhaifu, ni uzushi mtupu! - 4
Mihadhara ya Wakristo yatawala Handeni
Ziara ya Kadinali Pengo Moro
Aonyesha ujuzi wa kutengeneza
Trekta
Waislamu wasizifanye sharia
za dini kuwa nzito – Sheikh Mzonge
Sengerema waomba msaada
Chakula na Lishe
|