|
Ijue Madrastin-Nuur
Ngaranaro
Na Mwandishi Wetu, Arusha Madrasatin-Nuur iliyopo Ngaranaro Unga Limited ilianza takriban miaka 40 iliyopita; ilianzishwa na Mwalim Sultan kutoka Kondoa kama madrasa ya barazani. Mwalimu Saidi alichukua nafasi baada ya kifo cha Mwalimu sultan mwaka 1960 ikaongozwa na mwalimu Abdallah Saleh akifundisha Qur’an na Fiqh. Sheikh Siraj Salum na Sheikh Mahmoud Salim walijiunga na madrasa hiyo kumpa nguvu Sheikh Abdallah mwaka 1977 wakifundisha tafsiri ya Qur’an, Hadith Sirat na lugha ya Kiarabu. Kwa nguvu hii mpya darasa lilipata watoto wengi zaidi ambapo ilibidi wasome kwa kupokezana –asubuhi, mchana na wale wa jioni. Mwaka 1984 Mwalimu Abdallah alifariki na hivyo nafasi yake kuchukuliwa na Mwalimu Juma Salim Teva. Ongezeko kubwa la wanafunzi lilifanya nafasi kuwa ndogo na hivyo ikawa watoto baadhi wakawa wanasomea nyumbani kwa Sheikh na wengine msikitini. Mwaka 1987 Waislamu waliamua kujenga msikiti mpya mkubwa kwa kujitegemea ujenzi ambao ulikamilika mwaka 1992 kwa gharama isiyopungua milioni 55. Hivi sasa, Waislamu hao wa Ngaranaro – Unga Limied wapo katika ujenziwa jengo la madarasa lenye ghorofa nne (4) kwa gharama inayokisiwa kufikia shilingi milioni tisini (90 m. shs.) Hatua ya awali ya kuweka msingi na kusimamisha nguzo ishakamilika kwa gharama ya shilingi 8,440,000. Hata hivyo, ujenzi umesimama toka Februari 1998 kutokana na ukosefu wa fedha na vifaa ambavyo ni vyuma; simenti na mchanga. Jengo hilo litakapokamilika litakuwa na vyumba vya madarasa vya kutosheleza shule ya awali ya watoto; madrasa (traditional) na shule ya sekondari. Kamati inayosimamia madarasa; msikiti na Ujenzi wa jengo jipya inawaomba Waislamu watoe michango yao kusaidia ujenzi. Michango ya vifaa iwasilishwe msikitini na ile ya fedha itumwe msikiti wa Ijumaa Ngaranaro, A/C No. 6590900131
Miongoni mwa mafanikio makubwa ambayo madrasa hii imepata
ni pamoja na kutoa wanafunzi wengi sasa hivi ni masheikh, maimamu na waalimu
wa madrasa. Miongoni mwao wakiwemo masheikh maarfu kama SheikhYahya Khamis.;
Sheikh Adil, Ustaadh Hamidu Issa na Ustadh Abbas Othman.
|
Maoni yetu: Prof. Juma Kapuya, vipi Muislamu usijue agenda za Waislamu? Hatimaye Mzee Katambo, Chata waachiwa
Sheikh Bafadhil aitaka Bakwata iwe
mtetezi wa Waislamu
Makala: Uinjilisti wa Mbuni haufai
Mussa Katambo: Mzee aliyewekwa rumande kwa kuandaa mihadhara Makala: Elimu ya ngono yapenyezwa
tena Zanzibar
Arusha wasema: Hongera Mhe. KK kwa
kuwa mfano mwema
Wanawake Songea kuandaa maonesho
Kesi ya mgogoro wa Ardhi
AN-NUUR marufuku
gerezani?
Waislamu Karagwe wadai kusalishwa
na imamu asiyejua kutawadha
Ofisi mpya za Rabita
|