|
|
| Mussa Katambo:
Mzee aliyewekwa rumande kwa kuandaa mihadhara
MZEE Mussa Katambo alizaliwa mwaka 1916 katika kijiji cha Tindiga wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro. Alisoma madrasa moja kwa Sheikh Abdulrahmani Swedi, mkoani Morogoro, 1922. Alipigana vita vya pili vya dunia nchini Madagascar 1930, pia alishiriki katika harakati za kudai uhuru wa Tanganyika. Hakufanya kazi serikalini wala katika chama. Alifanya kazi ya udereva Idara ya Forodha hadi 1980. Ndiye muasisi wa Msikiti wa Kibo (Masjid Baytul Muqaddas). Aliuza raslimali zake nyingi na kununua kiwanja na kisha kujenga Msikiti huo, pia ni muasisi wa madrasa huko Kisaki- Morogoro, Gomero – Chalinze na sehemu nyingi nyinginezo. Alikamatwa mara ya kwanza na polisi akiwa jukwaani akifungua mhadhara wa Khidmat ndani ya eneo la Msikiti wa Kibo hapo Februari 9, 1998 na kupelekwa kituo cha polisi cha Oysterbay kwa kuhojiwa na kisha aliruhusiwa kurudi nyumbani. Siku ya pili yake, Februari 10, 1998 alikamatwa nyumbani kwake Ubungo Kibo na kupelekwa moja kwa hadi Kituo Kikuu cha Polisi (Central Police Station) na kuwekwa ndani. Kesho yake, yaani Februari 11, 1998 pamoja na waumini wengine walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakama ya Kisutu na kusomewa shitaka la kufanya mhadhara bila kibali cha polisi, kukashifu Ukristo kwa kusema "Yesu siyo Mtoto wa Mungu na Biblia siyo kitabu cha kweli". Baada ya hapo walipelekwa moja kwa moja katika gereza la Keko. Mara walipoingizwa gerezani hapo, walivuliwa nguo zote na kubaki uchi bila kutenganishwa na watoto wadogo na kuanza kupekuliwa sehemu zote za mwili kutafuta kama wameficha mabomu na silaha nyingine. Aliingizwa gerezani akiwa na afya njema, lakini ametoka na maradhi ya ngozi. Ametokwa na vidonda kwa kujikunakuna sana kutokana na mwasho wa mwili anaoupata. Kutokana na kuathiriwa kisaikolojia, amevurugikwa na akili. Pia ulimi wake umekuwa mzito kutamka mpaka umsikilize kwa makini. Aliwahi kupigwa kofi (kibao) na afisa mmoja wa Magereza wakati akipangwa kuelekea mahakamani. Anasema katika maisha yake yote tangu ujana wake hakuwahi kuwekwa ndani kabla ya tukio hili. Alidai aliambiwa aachiwe kwa masharti kwamba akitoka abomoe Msikiti
na aachane na mihadhara, lakini alikataa na kusema ni heri auliwe au awekwe
ndani maisha kuliko kukubli masharti hayo.
|
Maoni yetu: Prof. Juma Kapuya, vipi Muislamu usijue agenda za Waislamu? Hatimaye Mzee Katambo, Chata waachiwa
Sheikh Bafadhil aitaka Bakwata iwe
mtetezi wa Waislamu
Makala: Uinjilisti wa Mbuni haufai
Mussa Katambo: Mzee aliyewekwa rumande kwa kuandaa mihadhara Makala: Elimu ya ngono yapenyezwa
tena Zanzibar
Arusha wasema: Hongera Mhe. KK kwa
kuwa mfano mwema
Wanawake Songea kuandaa maonesho
Kesi ya mgogoro wa Ardhi
AN-NUUR marufuku
gerezani?
Waislamu Karagwe wadai kusalishwa
na imamu asiyejua kutawadha
Ofisi mpya za Rabita
|