AN-NUUR
Na.157 Rabi' Awal 1419, Julai 10 - 16, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Ukweli usiachwe 

Katika gazeti la AN-NUUR Na. 150, iliandikwa makala yenye kichwa cha habari "Mohammed Saidi acha kuwapotosha wenzako". Napenda kutoa maoni yangu juu ya makala hayo, kama tulivyotakiwa na mhariri wa gazeti hilo. Bi. F.M. Abdulrahman anaelezea kwa undani. 

Ni ukweli usiofichika kwamba, Waislamu Watanzania kwa makusudi kabisa, wamenyimwa elimu kabla ya uhuru na hata baada ya uhuru. Pamoja na ahadi ya Mwalimu Nyerere baada ya uhuru kuwa atasawazisha uwiano mbaya wa elimu kati ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu. Je? Bwana Mtaki hulijui hilo? 

Kunyimwa elimu kwa Waislamu ni mkakati maalum uliopangwa na maadui wa Uislamu. Kama Bwana Mtaki halijui hilo arejee kitabu kilichoandikwa na Dr. Sivalon "Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania. Kwanini watoto wa Kiislamu walikuwa anabatizwa ili wasome? Kwanini Mwalimu Nyerere aliivunja EAMWS? Na kuzuia ujengwaji wa Chuo Kikuu cha Kiislamu Chang’ombe? Naomba Bwana Mtaki atoe majibu na maswali hayo. 

Sambamba na hilo. ni tabia iliyozoeleka kwa Watanzania, kuficha ukweli na anapotokea mtu akaufichua ukweli anaonekana ni mchochezi na mvurugaji wa amani. Hii ina maana kuwa amani ya tanzania haiwezi kuwepo mpaka ukweli wa aina fulani ufichwe, kwa sababu ukweli unapobainishwa, anayedhulumu atajulikana, na anaedhulumiwa atang’amua kuwa anadhulumiwa na hivyo kuanzisha harakati ya kudai haki yake. 

Katika jamii au nchi yoyote ile historia ya nchi haitaweza kufahamika vizuri mpaka iwe imeandikwa au watokee watu wa kuielezea historia hiyo. Ndivyo ilivyo historia ya Tanzania hususan historia ya chama cha TANU. 

Historia ya chama cha TANU haifahamiki vizuri. Hii inathibitishwa na kauli ya Mwalimu Julius K. Nyerere alipotoa maoni yake ju ya kitabu cha "Mwito wa Uhuru" kilichoandikwa na saadani Abdu Kandoro, namnukuu. 

"moja ya upungufu wetu katika TANU ni kwamba hatujaandika historia ya TANU. Kwa kweli hakuna mtu mmoja ambaye aweza kusema kwamba yeye anajua historia yote ya TANU. Kila mmoja wetu anajua sehemu sehemu tu ya mambo yaliyofanyika nakufikisha TANU hapo ilipo. 

Bwana Kandoro, katushinda wote na pia katushinda kwa kuandika yale ambayo yeye anayakumbuka. Wakipatikana wengine kama yeye na kuandika yale ambayo wao wanayakumbuka, tutakuwa tumechukua hatua ya mwanza kukusanya nakuandika historia ya TANU. 

Kwa hiyo, natumaini kuwa kitabu hiki cha Bwana Kandoro kitawatia moyo watu wengine na kufuata mfano wake na kwa hiyo nakitakia heri." 

Mhe. Julius Kambarage Nyerere, 22 Septemba, 1961). 

Kwa bahati mbaya changamoto hii iliyotolewa na Mwalimu Nyerere haikupokewa kwa muda mrefu sana. Hivi karibuni Bwana Mohammed Saidi, ameipokea changamoto hii na kuanza kuandika yale anayoyafahamu katika historia ya TANU. Na kazi anayoifanya Bwana Mohamed Said imeshapata baraka za Mwalimu Nyerere tangu mwaka 1961. Cha muhimu sio kushutumiwa Bwana Mohammed Saidi kwa kile anachokifanya kwa kuambiwa mchochezi na anaetaka kuvuruga amani, kwani anayoyaeleza sio ya uongo kwa kuwa hadi leo hakuna aliyekanusha maenno yake. Kama kuna anayesema kuwa, anayasema ni uongo, uwanja uko wazi, abainishe wapi kwenye uongo huo na sio kutoa shutuma zisizo na msingi wala ukweli wowote. 

Labda linalomkera Bwana Mtaki ni kuona jinsi Waislamu na nchi hii walivyokuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru. Hili kwa kiasi fulani linatokana na ukweli kwamba kumbe hata Nyerere alipokuja Dar es Salaam, na hapa tena alikuta tayari, harakati za kudai uhuru zimeshamiri na kwamba yeye alipewa uongozi tu. Huo ndio ukweli wa harakati za uhuru Tanganyika. Usistaajabu leo kuona Waislamu wanatupwa nyuma. Haya ameyakiri Nyerere mwenyewe katika hotuba zake mbalimbali wewe linakushangaza lipi? 

Mwisho, nawataka Watanzania wengine wote kama kuna wanayoyafahamu (ya kweli) katika historia ya nchi hii, basi wayaandike ili Watanzania wengine wayafahamu na sio wafanye kazi ya kushutumu wenzao tu. Na nampongeza Bwana Mohammed Said kwa kazi kubwa anayoifanya na mnamtakia kila la heri katika kazi yake hiyo, na asikatishwe tamaa na watu kama akina John Mtaki na Mwinjilisti Kusupa 
 

Juu 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI 

Maoni yetu: Prof. Juma Kapuya, vipi Muislamu usijue agenda za Waislamu? 

Hatimaye Mzee Katambo, Chata waachiwa
Na Mwandishi wetu

Polisi Newala wajenga Msikiti 

Sheikh Bafadhil aitaka Bakwata iwe mtetezi wa Waislamu
Na mwandishi wetu

Makala: Uinjilisti wa Mbuni haufai
Na Rajabu Mbambwa, Kigoma

Mussa Katambo: Mzee aliyewekwa rumande kwa kuandaa mihadhara

Ukweli usiachwe 

Makala: Elimu ya ngono yapenyezwa tena Zanzibar 
Na Saidi Mzee 

Arusha wasema: Hongera Mhe. KK kwa kuwa mfano mwema 
Na Hussein M.,  Arusha 

Wanawake Songea kuandaa maonesho 
Na. Jumah Mbwana, Songea 

Kesi ya mgogoro wa Ardhi
Na. Mustafa Adam 

AN-NUUR marufuku gerezani? 
Na Mwandishi Wetu 

Waislamu Karagwe wadai kusalishwa na imamu asiyejua kutawadha 
Na. Abu Abdallah 

Ofisi mpya za Rabita 
Na Mwandishi Wetu

Barua za wasomaji

Habari za Madrasa

Masomo

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita