NASAHA
Na. 062 Jumatano  Agosti 23 - 29, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
HABARI ZA KIMATAIFA 
 
 

Sharia ya Kiislamu yaanza Borno

MAIDUGURI, Nigeria.

WIKI hii Waisamu wa jimbgo la Burno, nchini Nigeria wamefanya sherehe ya kuanza kutumia rasmi Sharia ya Kiislamu.

Gavana wa jimgo hilo Malla Kachalla akitangaza katika mkusanyiko wa Waislamu zaidi ya 100,000 uliofanyika katika mji wa Maiduguri jimboni humo, amesema sharia hizo zitawahusu Waislamu tu. 

Wakristo wa jimgo hilo wameeleza wasiwasi wao kuwa kuanzishwa kwa matumizi ya sharia jimboni humo huenda ukatishia uhuru wao wa kuabudu. 

Jimbo la Borno lililopo kaskazini mwa nchi hiyo ni jimbo la tisa miononi mwa majimbo yanayotumia au yaliyotangaza mpango wa kutumia sharia. 

Majimbo mengine manne yana mpango wa kuanzisha utekelezaji huo hivi karibuni. 

Wapinzani wa sharia ya Kiislamu nchini humo wamesema kuwa wimbi la kuanzisha sharia ya Kiislamu ni tishio kwa umoja wa kitaifa. 

Hapo mwaka jana Rais wa nchi hiyo Bwana Olegusun Obasanjo ambaye ni muumini wa dini ya Kikristo alisema kuwa anavyofikiri yeye ni kwamba wimbi la kuanzisha sharia lingengefifia na ni la muda tu. 

Aliongeza kuwa hadhanii kuanzishwa kwa sharia kutavuruga amani na umoja wa kitaifa. 

Watetezi wa sharia ya Kiislamu nchini humo wameeleza kuwa utekelezaji wa sharia ni sehemu ya maisha yao tangu maelfu ya miaka iliyopita. 

Wamefafanunua kuwa tangu utawala wa Uthman Dan Fodio nchi za Afrika Magharibi zilikuwa na utawala wa Kiislamu. 

Wamedai kuwa ukoloni wa Kiingereza ambao ni waumini wa Kikristo walivuruga utaratibu wao maridhawa ambao ni mfumo wa maisha. 

Ukoloni wa Kiingereza uliingia nchini humo karne iliyopita hadi miaka ya sitini. 

Jimgo la Zamfara ni la kwanza kuanza kutumiasharia toka nchi hiyo irudi katika utawala wa kiraia hapo Mei mwaka jana. 

Katika jimbo hilo hivi sasa uuzaji na matumizi mengine ya ulevi (pombe), hadharani vimepigwa marufuku. 

Pia shule za mchanganyiko zimekuwa ni za jinsia moja na usafiri wa Umma hairuhusiwi mchanganyiko wa wanaume kwa wanawake. 

Tangu kuanzishwa kwa sharia nchini humo zaidi ya watu 2,000 wamepoteza maisha kutokana na mapigano kati ya Waislamu naWakristo. 

Wakristo waishio katika majimbo yanayofuata shari nchini humo, wameanza kufunga na kusali kwa juhudi zote, ikiwa ni harakati za kufanikisha sheria hiyo ifutwe. 

Jaji Mkuu wa Kiislamu 'Ghand Khadi' aliapishwa kushika wadhifa huo, atakuwa na madaraka ya kuendesha kesi pale sheria hiyo itakapovunjwa. 

Sheria hiyo itatumika katika kuhukumu kesi za unywaji pombe. Wizi, uporaji na ukahaba. 


Waislamu Kenya wakutana na Wabunge 

NAIROBI,Kenya.

Zaidi ya wabunge 27 Waislamu kutoka vyama tofauti vya siasa nchini Kenya walifanya kikao cha pamoja na Baraza Kuu la Waislamu wa Kenya (SUPKEM) katika Hoteli ya Nairobi.

Akizungumza na Wabunge hao Mwenyekiti wa SUPKEM, Profesa Abdul Ghafoor El Busaidy amesema umuhimu wa kikao hicho ni kujadili juu ya elimu kwa vijana wa Kiislamu nchini humo. 

Alifafanua kuwa vijana hao wanashindwa kupata elimu kwa sababu ya hali duni ya kiuchumi aidha hawapati nafasi za elimu katika taasisi za serikali. 

Akiainisha zaidi alisema nchini humo kuna vyuo vikuu visivyo vya serikali 12 na kati ya hivyo saba nivya kidini (Kikristo), wakati Waislamu hawana hata chuo chenye dalili za dini hiyo. 

SUPKEM kwakushirikiana na nchi za Kiislamu itatoa nafasi za masomo nje ya nchi kwa ajili ya vijana hao hasa katika taulumu ya utabibu. 

Mwenyekiti huyo alikiambia kikao hicho kuwa vijana wa Kiislamu waliopo katika taasisi za elimu ya juu wapo asilimia mbili miongoni mwa wanaotakiwa kulipiwa ada. 

Mheshimiwa Faim Y.Twaha, Mbunge wa Lamu Magharibi na Naibu Waziri wa Maliasili alitoa mchango wa shilingi milioni moja kusaidia wanafunzi hao. 

Waziri wa mambo ya ndani Mheshimiwa Sharif Nasir alisema ili Waislamu waweze kupiga mbele hatua ya maendeleo suala la kujitegemea lipewe kipaumble. 

Mbunge pekee Muislmau mwanamke Mheshimiwa Marere Wamwachai alisisitiza kuwasaidia wanawake katika matatizo makubwa yanayowakabili ikiwa ni pamojana kujenga shule maalum kwa ajili yao. 

Aliongeza kuwa viongozi washirikiane bega kwa bega na wanawake katika kukabiliana na hali duni ya uchumi, maradhi na ujinga. 

Pia mama huyo alitoa changamoto kwa wanawake kushiriki kikamilifu katika masuala ya siasa, uchumi na uongozi. 

Wabunge Waislamu hao wa Kenya walichaguliwa katika uchaguzi wamara ya pili wa vyama vingi uliomalizika katika wiki ya kwanza ya Januari 1998. 

Juu
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI
Kama hamtaki demokrasia, mnataka nini basi?

Prof. Lipumba ana uwezo wa kuongoza nchi - CCM

Kampeni za uchaguzi 2000, CCM yamalizia muda wake na kusema:
Imefanya kazi ya ‘kuipendeza’ Marekani

Vita dhidi ya rushwa ianzie kwa vigogo -Lipumba

Wakati umefika wanawake kushiriki siasa - Mugissa

TLP yadaiwa kuukejeri Uislamu

CUF Kigamboni kuzindua kampeni leo

USHAURI NASAHA
Nimechoka kuwa mtangazaji wa redio

MAKALA
Mungu na mataifa ya dunia

MAELEZO BINAFSI
Mjue mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Lipumba

MIPASHO NASAHA
Krosi matiplikesheni!

MAKALA
Wananchi kajiandikisheni kupiga kura ili kuleta mabadiliko ya serikali kwa njia ya amani

KALAMU YA MWANDISHI
Mkijirekebisha mtakaribishwa

Habari za Kimataifa

LISHE
Unakula au unaliwa?

MASHAIRI

MICHEZO

  • Yanga, Mtibwa nani bingwa leo?
  • Ugomvi mkubwa baina ya Simba na Yanga waibuka 
  • Arsenal yaitandika Liverpool
  • Ngorongoro Heroes yaenda Msumbiji

  •  


    Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita