NASAHA
Na. 062 Jumatano  Agosti 23 - 29, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
MAELEZO BINAFSI 

Mjue mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Lipumba



MAELEZO BINAFSI 

JINA : Ibrahim Haruna Lipumba 

Mwenyekiti wa Taifa wa Civic United Front (CUF - Chama Cha Wananchi) 
P.O. Box 10979 
Dar es Salaam, Tanzania. 
Tel. 255 (51) 860812, 255 (51) 861009 
Fax 255 (51) 861010 

E-mail: cuf@twiga.com, lipumba@homemail.com
 

MAENEO YA UTAALAM : International Trade and Finance, Macroeconomics, Development Economics and Agricultural Economics. 
 

TAREHE YA KUZALIWA : June 06, 1952 
KIJIJI : Ilolangulu 
WILAYA : Tabora 
MKOA : Tabora 
DINI : Muislam 
NDOA : Nimeoa 
 

ELIMU

Elimu ya Msingi 
1959 - 62 : Swedish Free Mission Primary School, Sikonge 
1962 - 66 : L.A Upper Primary School, Sikonge 
 

Elimu ya Sekondari
1967 - 70 : Tabora Boys Secondary School 
1971 - 72 : Pugu Secondary School 
 

Elimu ya Chuo Kikuu
1973 - 77 : University of Dar es Salaam 
1978 - 83 : Stanford University 
 

SHAHADA

BA (Hon. Economics) University of Dar es Salaam 1976 
MA (Economics) University of Dar es Salaam 1977 
MA (Economics) Stanford University 1979 
Phd (Economics) Stanford University 1983 
 

UZOEFU WA UONGOZI NIKIWA MASOMONI.

Mweka Hazina - Umoja wa Vijana Tabora Boys Secondary School 1969 - 70 
Mjumbe wa kamati ya Umoja wa Vijana - Pugu Secondary School 1970 - 71 
Mwenyekiti - Umoja wa Vijana - Chuo Kikuu 1975 - 76. 
Mwanzilishi na Rais wa Kwanza wa Stanford African Students Association (SASA), Stanford University; Stanford, California USA. 1978 
 

KAZI

1976 - 77 Mkufunzi Msaidizi (T.A) 
1977 - 83 Mhadhiri Msaidizi 
1983 - 86 Mhadhiri 
1986 - 89 Mhadhiri Mwandamizi 
1989 - 93 Profesa Mshiriki 
1991 - 93 Msaidizi wa Rais Mambo ya Uchumi 
1993 - 95 Fulbright Visiting Professor, Williams College, Massachussets, United States of America. 
1996 - 98 Senior Research Fellow, United Nations University, World Institute of Economic Research, Helsinki Finland. 
 

Heshima za Kitaaluma

1993 - 1995, Fulbright Visiting Professorship 
1986-1989, Kellogg International Fellow in Food Systems 
1977-1983, Rockefeller Foundation Fellowship 1976, Zawadi ya Mwanafunzi Bora, Best Student Award, Faculty of Arts and Social Sciences, University of Dar es Sa laam. 

Mshauri wa Uchumi (Consultant to)

The World Bank, UNDP, Global Coalition for Africa, Preferential Trade Area for Eastern and Southern Africa (now COMESA), Swedish International Development Agency (SIDA), NORAD, DANIDA, Ministry of Foreign Affairs Finland, Bank of Tanzania, Macroeconomic and Financial Management Institute of Eastern and Southern Africa (MEFMI), African Capacity Building Foundation. 

SHUGHULI ZA KIMATAIFA

Utafiti kuhusu kushiriki kwa nchi za kusini katika mfumo wa biashara wa kimataifa, Uruguay Round Multilateral trade negotiations - 1986 - 90. 

Utafiti kuhusu sera za kilimo za nchi zinazoendelea. 

Kuwasilisha maelezo (Testmony) kuhusu matatizo ya madeni ya Afrika kwenye kamati ya Bunge la Marekani - House Sub Committee on International Development, Finance, Trade and Monetary Policy - February, 1994. 

Kuwasilisha, maelezo (Testmony) kuhusu shirika la Fedha la Kimataifa (IFM) na uhusiano wake na nchi masikini kwenye kamati ya Bunge la Marekani House - Sub Committee on International Development, Finance, Trade and Monetary Policy - April, 1994 

Kutayarisha "Report of Group of Independent Advisers on Development Cooperation issues between Tanzania and Aid Donors". June , 1995 

Kuteuliwa kuwa mjumbe wa kamati ya Umoja wa Mataifa ya sera ya maendeleo (member of the United Nations Committee for Development Policy (1995 - 99.) 

Kutayarisha vigezo vya kuainisha nchi masikini sana duniani. (The list of Least Developed Countries (1997 na 2000) 

Kutayarisha na kuratibu utafiti na kupendekeza sera za viwango vya kubadilishana sarafu (exchange rate policy) na sera za kulegeza masharti ya mfumo wa fedha (financial liberalization) Kampala, Uganda (1997). 

Kutoa taarifa katika Kamati ya Umoja wa Mataifa ya mambo ya uchumi na maendeleo (ECOSOC) kuhusu mgogoro wa kimataifa wa fedha katika nchi za Asia, NewYork (1998). 

Kutoa ushauri wa namna ya kuimarisha muundo na sera za fedha, Wizara ya Fedha, Windhoek, Namibia (1998). 

Kutoa ushauri wa namna ya kuimarisha muundo na sera za fedha, Wizara ya Fedha, Mbabane, Swaziland (1998). 

Kutathmini maendeleo ya 'The Macroeconomic And Financial Management Institute Of Eastern And Southern Africa', (MEFMI) ili kuwasaidia wahisani kufanya maamuzi juu ya kuendelea kuisaidia taasisi hiyo,1998. 

SHUGHULI ZA KITAIFA

Mjumbe - Kamati ya kurekebisha mashirika ya umma, 1992 - 1993 

Mwenyekiti - Tume ya kuchunguza matatizo ya chama cha ushirika cha mkoa wa Shinyanga (SHIRECU), 1992 

Mwenyekiti - Tume ya Waziri wa Fedha ya kuchunguza matatizo ya Shirika la Bima (NIC) 1993 

BAADHI YA UTAFITI WA UCHUMI NA MAANDISHI MUHIMU

Stabilization Policies in Tanzania, University of Dar es Salaam, 1984. 

African Unity, Some Practical Guidelines, MAWAZO Vol. 1. No. 2, May 1983. Published by Stanford African Students Association. 

Problems and Prospects of African Economic Integration , MAWAZO Vol. 1. No. 1, April 1982. 

The Brandt Commission Report: A General Overview, Journal of Economic Reflections, January 1982. 

Book Review, R. H. Green (et al.) Economic Shocks and National Policy Making. Tanzania in the 1970s. UCHUMI Journal of the Economic Society of Tanzania. 

The Economic Crisis and Basic Needs in Tanzania, ILO Basic Needs and Development in Tanzania 1983 Addis Ababa. 

Basic Needs and Agricultural Development Policy: A Critical Review. ILO Basic Needs and Development in Tanzania. 1983 Addis Ababa. 

"Macroeconomic Management of the Tanzania Economy", International Development Research Centre. The Zambian Economy: Problems and Prospects 1984. 

"Policy Reforms for Economic Development in Tanzania", published in Stephen K. Commins (ed.) Africa Development Challenge and the World Bank. Lynne Rienner Publishers. Boulder/London. 1988. 

"The Global Trading System and Economic Development of Tanzania" in John Whalley (ed.) Dealing with the North. Centre for the Study of International Economic Relations (London, University of Western Ontario) 1987. 

"Domestic Supply Constraints versus Market Access Problem in International Trade and Economic Development of Tanzania" in John Whalley (ed.) The Small Among the Big. Centre for the Study of International Economic Relations (London, University of Western Ontario). 

"A Supply Constrained Macroeconometric Model of Tanzania" Economic Modelling Vol. 5 No. 4. October 1988 with Ndulu, Horton and Plourde. 

"Market Liberalization and Food Security in Tanzania", with Amani, Ndulu and Kapunda. Proceedings of SADCC Food Security Conference Harare 1987. 

"The Arusha Declaration and Economic Development of Tanzania", in Hartmann, J. The Arusha Declaration Twenty Years After (Copenhagen Centre for Development Research) 1990. 

"Reflections on Economic Development in Tanzania", in UCHUMI Journal of Economic Society of Tanzania 1987. 

The Impact of Market Liberalization on Household Food Security, with Amani, Ndulu and Kapunda. SADCC Conference on Food Security Conference Proceedings. 1988. 

Reflections on Long Term Development Strategy in Tanzania, in World Bank Sub-Saharan Africa: From Crisis to Sustainable Growth A Long Term Perspective Study, Vol. I. 1990. 

The Record and Prospects of the Preferential Trade Area of Eastern and Southern African States in Chhibber Ajay and Stanley Fischer Economic Reform in Sub-Saharan Africa World Bank 1991. 

Determinants of Appropriate Exchange Rate, in UNDP Aspects of Exchange Rate Determination United Nations, New York 1991. 

Exchange Rate Policy in Tanzania, UNDP, Stabilization and Adjustment United Nations, New York 1991. 

Tanzania: Medium Term Development Issue and Prospects, African Development Bank, African DevelopmReport 1994. 

Structural Adjustment Policies and the Economic Performance of African Countries. 

United Nations Conference on Trade and Development International Monetary and Financial Issues for the 1990s. Vol. V. 1995. 

African Beyond Adjustment, Policy Essay No. 15 Overseas Development Council Washington, D.C. 1994. 

"Financing Long Term Development in Sub-Sahara Africa" in Culpeper Roy, Caroline Pesteau, IDRC, Development and Global Governance 1995. 

"The Liberalization of Foreign Exchange Markets and Economic Growth in Sub-Sahara Africa" UNU/WIDER Research for Action No. 35, 1997. 

"An evaluation of the institutional set up and technical capacity of the Ministry of Finance - Namibia." A Consultancy Report to The Macroeconomic and Financial Management Institute of Eastern and Southern Africa (MEFMI) 1998 

"An evaluation of the institutional set up and technical capacity of the Ministry of Finance - The Kingdom of Swaziland." A Consultancy Report to The Macroeconomic and Financial Management Institute of Eastern and Southern Africa (MEFMI) 1998 

"The Macroeconomic And Financial Management Institute Of Eastern And Southern Africa, Mefmi - Midterm Review" Consultancy Report to MEFMI Liason Committee. 

"Opportunities and challenges of globalization: Can sub-sahara Africa avoid marginalization?" in UNDP(1999) Back ground papers to the 1999 Human Development Report. 

"Globalization of Finance and Development Prospects in Africa." In UNDP Cooperation South No. 1 1999 

"Debt Relief and Sustainable Development in Sub Sahara Africa." Fifth Expert Group Meeting on Financial Issues of Agenda 21, Nairobi, Kenya, 1-4 December 1999 
 


KWA NINI NIMEAMUA KUWA MGOMBEA URAIS.

Waheshimiwa Wananchi, 

Hii ni mara ya pili kuhiari kusimama kuwa Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vyama vya CUF na CHADEMA kwa pamoja vimenikabidhi jukumu hilo, kwa imani kwamba nina nia, sababu, na uwezo wa kutoa ushawishi kwa watanzania kuchagua serikali itakayorejesha haki, kuondoa umasikini, na kuharakisha maendeleo yao. Pamoja na kwamba mzigo mzito hupewa Mnyamwezi, hii ni heshima kubwa inayoashiria imani ya wanachama wa vyama hivi na mapenzi yao makubwa kwangu. Kwa kweli sina budi kuwashukuru sana kwa heshima hiyo. 

Mwaka 1995 nilikubali kugombea Urais kupitia tiketi ya CUF katika saa za majeruhi kwa sababu mbili kubwa. Mosi, mfumo wa demokrasia ya vyama vingi ulikuwa ndio unaanza kufanya kazi katika nchi yetu. Baada ya miaka karibu 35 ya uhuru wa Tanzania maendeleo yetu yalikuwa madogo. Sera za kuondoa ukiritimba wa dola katika uchumi zilizokuwa zikitekelezwa na Rais Mwinyi hazikuungwa mkono kikamilifu na Chama chake. Baada ya kufanya kazi kama Mshauri wa Uchumi wa Rais Mwinyi, na kushuhudia vizingiti alivyowekewa katika utekelezaji wa sera za kurekebisha uchumi, niliamini kuwa CCM haina uwezo wa kufanya mageuzi ya kimsingi yatakayojenga uchumi imara wenye manufaa kwa wote. 

Nilikubali kugombea Urais kwa tiketi ya CUF ili niitumie nafasi hiyo kuwazindua wananchi waelewe kuwa wakiichagua CCM, hali zao za maisha zitaporomoka. 

Kwa nini CUF? Nilivutiwa na sera za msingi za Chama cha CUF za "HAKI SAWA KWA WANANCHI WOTE" na itikadi ya UTAJIRISHO yenye madhumuni ya kujenga uchumi imara utakaoleta NEEMA KWA WOTE. 

Waheshimiwa wananchi, Je, ni Watanzania wangapi ambao kwa dhati kabisa wanaweza kusema imekuwa ni neema kwao kumchagua Mhe. Mkapa kuwa Rais? Je, hali ya maisha ya wananchi wa kawaida imeboreka au imeporomoka? 

Sababu ya pili ilikuwa kujenga umoja wa kitaifa kwa kukiimarisha chama cha CUF Tanzania Bara. Nilikuwa na uhakika kuwa CUF itashinda Zanzibar. Vile vile niliamini kuwa Chama chetu kisingeweza kushinda Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Niliingia katika kugombea Urais kwa nia ya kukiimarisha Chama chetu Bara ili kulinda Umoja wa Kitaifa na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kama chama chetu kingekuwa imara Zanzibar peke yake na kuwa kibovu Tanzania Bara, umoja wa kitaifa ungeathirika. Chama cha CUF sasa kimeimarika sana Tanzania Bara. Naamini Chama chetu kilishinda uchaguzi mdogo wa Temeke na Ubungo na CCM ikatupokonya kwa mbinu za wizi wa kura. Hivi sasa CUF ni ngangari kweli kweli Bara na Zanzibar. 

Waheshimiwa wananchi, kwa mara ya pili katika uhai wangu nimehiari kujitwika mzigo mzito wa kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano. Sababu kubwa za kuhiari kubeba jukumu hili ni tatu. Mosi, Chama chetu kimeimarika. Sera zake za msingi : Haki sawa kwa wote na ujenzi wa uchumi imara wenye neema kwa wote zinakubaliwa na Watanzania wote. Changamoto wanayoitoa wananchi ni kutafsiri misingi hii kwa vitendo ili kujenga nchi inayoheshimu haki za binadamu, inayoendeshwa kisheria na inayoweka mazingira ya kuboresha hali ya maisha ya wananchi wote mwaka hadi mwaka. 

Sababu ya pili ni kwamba baada ya kutawala kwa muda wa miaka 40, CCM imechoka, inanuka rushwa na haina uwezo wa kusimamia maendeleo ya Tanzania. Uongozi wa CCM wa sasa hauna huruma na hauyajali matatizo yanayomkabili mtu wa kawaida. CCM haina dira. Viongozi wake wanang'ang'ania madaraka kwa manufaa ya watu wachache. Hawana mtazamo wa kujenga demokrasia ya kweli au kutetea maslahi ya wananchi wa kawaida. Viongozi wa CCM hawana haya. Wako tayari kutumia dola na propaganda yeyote ile ili wabaki madarakani. Mbinu hizi zinahatarisha umoja wa kitaifa. 

Waheshimiwa wananchi, sababu yangu ya tatu ni ya binafsi. Toka nikiwa kijana mdogo katika shule ya sekondari ya Tabora nilipendelea sana kusoma uchumi na namna nchi zinavyoendelea kiuchumi. Nilipomaliza kidato cha nne nilikuwa katika mchepuo (sub stream) wa sayansi. Masomo niliyofanya vizuri sana yalikuwa Hisabati, Fizikia na Kemia. Kwa kupenda kuelewa maendeleo ya uchumi niliamua kuomba kuchukua masomo ya Hesabu, Uchumi na Jiografia katika kidato cha tano (5). Kwa muda wa miaka thelathini nimekuwa najifunza na kutafiti sababu zinazofanya nchi ziendelee kiuchumi. Shahada zangu zote nne, mbili za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na mbili za Chuo kikuu cha Stanford Marekani ni za uchumi. Miaka 40 baada ya uhuru Tanzania ni miongoni mwa nchi maskini sana duniani. Nahitaji kutumia ujuzi na uzoefu wangu wa maendeleo ya uchumi kushirikiana na Watanzania wenzangu kujenga uchumi imara wenye neema kwa wananchi wote. 

Waheshimiwa wananchi, ni vyema tuuelewe vizuri umaskini wa Tanzania. Katika kila Watanzania mia moja, hamsini ni maskini wa kutupwa. Wastani wa pato la Mtanzania ni chini ya nusu ya wastani wa pato la watu wa Bara la Afrika. 

Waheshimiwa wananchi, maendeleo hayawezi kupatikana kwenye taifa la wagonjwa. Kwanza kabisa tija ya mtu anayesumbuliwa na maradhi ni ndogo. Pili, fedha nyingi ambazo zingeweza kuelekezwa kwenye maeneo mengine ya huduma za jamii na huduma za kiuchumi itabidi zitumike kugharamia tiba. Katika Tanzania tatizo la afya za wananchi wetu ni kubwa. Huduma za afya ziko katika hali mbaya. Hospitali, vituo vya afya, na zahanati ni chache na zinakabiliwa na matatizo mengi. Msongamano mkubwa wa wagonjwa, uhaba wa madaktari na wauguzi, uhaba wa vitanda, uhaba wa vifaa vya kazi, uchakavu wa majengo, na zaidi ya yote uhaba mkubwa wa madawa ni baadhi tu ya matatizo haya. Wafanyakazi katika sekta ya afya wanafanya kazi katika mazingira ya hatari yanayoweza kuwaletea maambukizi. Mishahara ni midogo ambayo hailingani kabisa na ugumu wa kazi. Wakilalamika wanaitwa 'wabinafsi' wasiojali 'wito' wa kazi yao na kukumbushwa viapo walivyoapa. Matokeo yake madaktari na wauguzi wamekuwa 'ombaomba' na wagonjwa wasio na chochote cha kutoa wamejikuta wakitelekezwa. Nchi jirani zimekuwa ndiyo kimbilio kubwa la madaktari na wauguzi wetu. Utafiti unaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 60 ya watoto wanaokufa chini ya umri wa miaka mitano hufia majumbani bila kufikiswa hospitali au zahanati alau kwa mara moja. Katika kila watoto 100 wenye umri usiozidi miaka mitano, 44 wana utapiamlo, hawana lishe bora. Watoto wanaokosa lishe bora hawajengi kinga ya mwili na ubongo wao haukuwi vizuri. Wastani wa maisha ya Mtanzania umeteremka toka miaka 52 mwaka 1990 mpaka kufikia miaka 48 mwaka 1997. 

Elimu yetu inaendelea kuporomoka. Hivi sasa inakadiriwa kuna watoto 3,000,000 wenye umri wa kuwa shule za msingi ambao hawasomi. Walioko shuleni hawana elimu bora. Mwak1998, katika ya kila wanafunzi 100 waliofanya mtihani wa darasa la saba, 70 hawakupata alama za kufaulu. Tanzania ni nchi ya nyuma kuzidi zote ulimwenguni kwa maendeleo ya elimu ya Sekondari. Katika kila vijana mia moja wenye umri wa kuwa shule za sekondari ni sita tu ndio wanasoma sekondari, ukilinganisha na wastani wa 27 katika nchi za Kiafrika kusini mwa jangwa la Sahara. 

Waheshimiwa Wananchi, Watanzania ni fukara, lakini Tanzania sio maskini wa mali ya asili. Tuna ardhi ya kutosha, mito mingi na maziwa makubwa. Jiografia ya Tanzania inafanya nchi yetu iwe na majimbo yenye hali ya hewa tofauti. Mazao mbali mbali ya chakula na biashara yanastawi katika ardhi ya Tanzania. Mahindi, mtama, mpunga, ngano, jamii ya kunde, ndizi, mihogo, viazi, karanga, matunda na mbogamboga, hata uyoga vinastawi vizuri katika maeneo mbali mbali. Mazao ya biashara kama kahawa, pamba, chai, katani, korosho, tumbaku, alizeti, ufuta, pareto, minazi, chikichi, na hata maua yanastawi vizuri nchini mwetu. Tanzania ina uwezo mkubwa wa kuzalisha mazao ya chakula na biashara lakini miaka 40 baada ya uhuru Tanzania haijitoshelezi kwa chakula. Uzalishaji wa mazao ya kilimo tunayouza nchi za nje ulipungua kwa kasi kubwa miaka ya 1972 - 85. Ongezeko la mazao hayo katika miaka ya 1986 - 96 haukuwa wa kutosha kuweza kufidia kuanguka kwa uzalishaji miaka ya nyuma. Kilimo cha Tanzania kinategemea jembe la mkono na hakitumii sayansi na teknolojia ya kisasa. 

Hakuna kabisa ubunifu wa kuangalia ni mazao gani mapya ya kibiashara yanaweza yakakuzwa. Mathalani, michikichi ni zao ambalo lingeweza likakuzwa kwa mafanikio makubwa katika ukanda wote wa pwani na mkoa wa Kigoma. Mawese yatokanayo na chikichi ndio malighafi kubwa ya takriban mafuta yote ya kula yanayouzwa madukani. Hali kadhalika mawese ni malighafi kubwa kabisa katika utengenezaji wa sabuni za aina zote. Viwanda vya mafuta ya kula na sabuni nchini na katika nchi jirani vinategemea malighafi ya mawese kutoka Malaysia na Indonesia. Zao kama muarobaini linastawi katika ukanda wote wa pwani na katika baadhi ya maeneo mengine ya nchi yetu. Mbegu za muarobaini ni zao kubwa la kibiashara kwani ni malighafi muhimu ya kutengenezea baadhi ya madawa ya kufukuzia baadhi ya wadudu waharibifu mashambani. Kwa kifupi ni kwamba uwezekano wa Tanzania kukuza kilimo chake ni mkubwa sana. 

Kwa bahati mbaya sana sera za kilimo za serikali ya CCM tangu uhuru zimekuwa ni za kauli za kisiasa kuliko kuzingatia utafiti, kutoa motisha, ushauri na utaalamu kwa wakulima, na kuwepo kwa mikopo ya zana za kilimo na pembejeo. Wote tutakumbuka matangazo ya 'kilimo cha kufa na kupona' kwenye miaka ya sabini. Wananchi wakahimizwa 'kila mtu alime na alime popote'. Matokeo yake mahindi yakapandwa mpaka katikati ya miji na mapori yanayohifadhi vyanzo vya maji yakafyekwa ili watu wapande viazi! Haikusaidia kitu, zaidi ya uharibifu wa mazingira. Vyanzo vingi vya maji vilikauka na mazalio ya mbu mijini yakaongezeka. Sera zisizotabirika ikiwa ni pamoja na kuvunja vyama vya ushirika vya wakulima wenyewe, operesheni vijiji, operesheni maduka, na mashamba ya mfumaki zimeacha madonda sugu kwa wakulima na sekta ya kilimo kwa ujumla. Nchi yetu haina huduma bora za kilimo cha kisasa. Matumizi ya utafiti na mafunzo kwa wakulima kuongeza tija yametoweka. Barabara na mawasiliano vijijini ni mabaya sana. 

Sote tutakumbuka jinsi serikali ya CCM ya awamu ya tatu ilivyoyaanza madaraka kwa pupa. Waziri mkuu, alitoa tishio kwa wakuu wa wilaya kuwa 'Mkuu wa wilaya yoyote ambaye wilaya yake itakumbwa na uhaba wa chakula atakuwa amejifukuzisha kazi mwenyewe!' Lakini, Serikali haikuweka mazingira ya kuendeleza kilimo. Zana za kilimo na pembejeo haziwafikii wakulima kabisa na zinapowafikia siyo kwa wakati. Katika miaka mitano ya utawala wa Rais Mkapa, matumizi ya mbolea yamepungua mwaka hadi mwaka. Sababu kubwa ni kupanda kwa bei yake na kutoweka mikopo kwa wakulima. Hata mikopo ya kununulia mazao imekauka kabisa na kusababisha kuanguka kwa bei wanayolipwa wakulima. Tanzania haina dira na sera za kuendeleza kilimo. Miaka arobaini baada ya uhuru wastani wa uzalishaji hapa nchini kwa eka moja ni mdogo kuliko nchi nyingine zote za Kiafrika. 

Bahari ya Hindi, visiwa vya Zanzibar na Mafia, delta ya mto Rufiji, mbuga za wanyama za Serengeti, Ngorongoro, Lake Manyara, na Selous, Milima Kilimanjaro na Meru na ukarimu wa wananchi wetu na tamaduni zao, unaifanya Tanzania kuwa nchi ya pekee kwa mapumziko murua kwa wageni watokao nchi za Ulaya, Marekani na Asia. Gazeti la Financial Times la Uingereza limeelezea kuwa Tanzania "offers one of the world's most complete holiday destination." (Ni moja ya nchi inayotoa mapumziko murua yaliyokamilika.). Hata hivyo hatujatumia urithi wetu wa asili kuinua hali ya maisha ya Watanzania. 

Tanzania ina vyanzo vikubwa vya nguvu za umeme wa maji lakini gharama zake za umeme ni kubwa kuliko nchi za jirani na ukatikataji wa umeme ni jambo la kawaida. Hili ni jambo la kushangaza kabisa ikizingatiwa kuwa serikali imekuwa ikipata dola za kimarekani siyo chini ya milioni 10 kwa mwaka kutokana na ushuru wa petroli kuchangia mfuko wa nishati. Nchi yetu ina madini mengi ikiwa ni pamoja na dhahabu, almasi, bati, Chuma., Uraninium, phosphate, makaa ya mawe, vito, nickel, chokaa, jasi, chumvi, mfinyanzi na gesi. Madini haya hayajatumiwa kukuza uchumi wa nchi na kuboresha hali ya maisha ya wananchi. 

Maendeleo ya viwanda ni madogo sana nchini. Pamoja na madeni makubwa tuliyolimbikiza katika uwekezaji wa rasilimali katika viwanda, uzalishaji wa bidhaa za viwanda haukuongezeka kwa kasi iliyotarajiwa. Ajira viwandani ni ndogo sana. Katika nguvu kazi ya Watanzania milioni 17, walioajiriwa viwandani ni 145,000 tu. Hii ni chini ya asilimia moja ya nguvukazi yote. Watanzania laki nane tu ndio wenye ajira rasmi katika sekta zote. 

Kuongezeka kwa ajira rasmi ni kigezo muhimu cha uchumi unaokua na kupunguza umaskini. Hii ni kutokana na ukweli kwamba shughuli nyingine zote za kujiajiri zinategemea matumizi ya vipato vya wale wenye ajira rasmi. Mkulima, seremala, fundi cherehani, kinyozi, muuza duka, n.k., wote wanategemea mzunguko wa fedha ambao chanzo chake ni yule mwenye ajira rasmi. Mathalani, kikijengwa kiwanda mahali kinachoajiri wafanyakazi 1000 ambao kwa wastani kila mmoja wao analipwa shilingi 50,000/- kwa mwezi. Kila mwisho wa mwezi kutakuwa na jumla ya shilingi milioni 50 kwenye mikono ya wafanyakazi hao ambazo ziko tayari kutumiwa. Wako wanaohitaji vitanda watakwenda kwa fundi seremala. Wako watakaohitaji suruali au magauni watakwenda kwa fundi cherehani. Wako watakaohitaji mchele, maharage, unga, mchicha, n.k., watakwenda sokoni. Fundi seremala naye ili aweze kuchonga vitanda vya watu atahitaji kununua na kuchaniwa mbao. Fundi cherehani atahitaji kununua vitambaa. Mchuuzi wa sokoni atahitaji mkulima amuuzie, nk., alimradi ajira rasmi alfu moja zinaweza zikatengeneza mlolongo wa ajira tegemezi zinazoweza kuajiri watu wengine hata alfu tano. 

Waheshimiwa wananchi, pengine hakuna kitu kinachochangia kuongezeka kwa haraka kwa maendeleo katika nchi kama mtandao mzuri wa mawasiliano. Barabara na reli, usafiri wa majini pale unapohitajika, usafiri wa anga, simu, fax, na hivi sasa Internet. Kuwapo kwa njia za uhakika za usafiri ndani ya nchi kunarahisisha sana usafirishaji wa idadi kubwa ya watu na kiasi kikubwa cha bidhaa toka pande moja ya nchi hadi nyingine. Hili mbali ya kuokoa muda, lina mchango mkubwa katika kushusha gharama za kibiashara na hatimaye bei ya bidhaa. Hali kadhalika linasaidia sana kukuza maingiliano ya watu kwenye jamii na hivyo kufanya watu wa upande mmoja kujifunza kutoka watu wa upande mwingine. 

Kwa mujibu wa utafiti wa shirika la mawasiliano la umoja wa mataifa (ITU), mapato ya nchi masikini yanaweza yakaongezeka kwa wastani wa dola za kimarekani 4,000.00 kwa mwaka kwa kila simu moja mpya inayoongezeka ambayo itagharimu wastani wa dola za kimarekani 1,000.00 tu kuiweka. Nchini Tanzania hivi sasa kuna wastani wa laini za simu sita (6) kwa kila watu 1,000. Hali kadhalika kuna wastani wa masanduku ya barua matano (5) kwa kila watu 1000. Huu ni uwiano mbaya sana unaoashiria kuwa wananchi wetu hawatumii tekinolojia kufanya mawasiliano. Watanzania walwanatumia muda mwingi kutafuta taarifa na kuingia gharama kubwa za usafiri kwa sababu tu ya kukosa mawasiliano mazuri ya simu. 

Tanzania kuna tatizo kubwa la mawasiliano. Barabara ziko katika hali mbaya kabisa. Baada ya miaka 40 ya uhuru mtu anayetaka kwenda mikoa ya kanda ya ziwa kwa usafiri wa basi kutokea Dar es salaam, inakuwa ni nafuu kwake kupitia nchi jirani za Kenya na Uganda! Wakati wa masika safari ya kwenda Lindi na Mtwara inaweza ikachukua wiki tatu katika mazingira ya barabara iliyoko hivi sasa badala ya masaa manane. Kielelezo cha ubovu wa barabara zetu si kigeni kabisa kwa wakazi wa miji yetu. Barabara takriban zote alizoziacha mkoloni zikiwa na lami hivi sasa ni vumbi na makorongo matupu. Serikali ya CCM inawajibika kubeba lawama zote. Kila mwaka serikali hii inakusanya kiasi cha wastani wa dola za kimarekani 48 milioni kama ushuru wa barabara unaotozwa kwenye kila lita moja ya petroli na dizeli inayouzwa nchini. Fedha hizi kwa gharama za leo hii zinatosha kujenga umbali wa wastani wa kilometa 320 za barabara imara na ya kisasa. Lazima tujiulize hizi fedha zimekuwa zikifanyia nini iwapo hali ya barabara zetu ndiyo hii tunayoiona. 

Waheshimiwa wananchi, Ilani yetu ya Uchaguzi inafafanua kwa undani zaidi azma yetu na mikakati tutakayoitumia kujenga uchumi imara wenye manufaa kwa wote. Hapa nitazungumzia mambo machache ambayo nikiwa Rais nitayasimamia kwa karibu. 

1. Kujenga uchumi imara unao ongeza ajira.

Iwapo nitachaguliwa kuwa Rais lengo kuu la sera litakuwa kujenga uchumi unaokua kwa kasi kubwa na kuongeza ajira. Haiwezekani watanzania kuondokana na umaskini bila kukuza uchumi unaoongeza ajira. Katika suala la kukuza uchumi hakuna miujiza. Uchumi unakua kwa kuongeza elimu, ujuzi na utaalamu wa wafanyakazi, ongezeko la raslimali na vitendea kazi, na kuongezeka kwa ufanisi na tija katika uzalishaji na utoaji huduma. Dira ya maendeleo na sera za kutekeleza dira hiyo ni jambo la msingi katika kuleta maendeleo ya muda mrefu. Sera za ukiritimba wa dola katika mambo ya uchumi na kuwabana wananchi, kuwanyang'anya motisha wa kujiendeleza, na kufumbia macho rushwa ya hali ya juu inayoendelea nchini zimeporomosha uchumi wetu. Kwa muda mrefu uchumi wetu umetumikia siasa, badala ya siasa kuweka mazingira mazuri ya kukuza uchumi. Dira yetu ya maendeleo itakuwa ni kujenga uchumi wa soko wenye ushindani halali na unaowashirikisha na kuleta maendeleo kwa wananchi wote. Majukumu makubwa ya dola chini yetu yatakuwa ni:- 

Kuasisi utawala unaolinda kikamilifu haki za wananchi, unaozingatia kanuni na kufuata sheria. 

Kujenga mazingira yatakayotuhakikishia ongezeko kubwa la ajira mwaka hadi mwaka. 

Kuweka mazingira yanayolinda ushindani halali wa biashara, kuepuka mfumuko mkubwa wa bei, na kulinda ushindani wa bidhaa zetu katika soko la dunia. 

Kuboresha huduma za msingi za jamii na hasa elimu na afya. 

Kujenga au kusimamia ujenzi wa miundombinu mizuri kama vile barabara, reli, nguvu za umeme, simu na maji. 

Kulinda na kuhifadhi mazingira. 

2. Kilimo.

Ili Tanzania ijinasue katika dimbwi la umaskini ni lazima pawepo na mapinduzi ya Kilimo. Kuendeleza kilimo tunahitaji:- 

Kuongeza motisha kwa wakulima wapate bei nzuri ya mazao yao. Hatua za makusudi zahitajika kuboresha huduma za kilimo na kuweka usimamizi wa kuwalinda wakulima wasinyonywe na wafanyabiashara wanaoshirikiana kupunguza ushindani katika soko huria na kwa lengo la kuangusha bei za mazao. 

Mfumo wa kodi na ushuru wa mazao ya kilimo kurahisishwa na viwango vya kodi ya mazao kupunguzwa ili kuongeza motisha kwa wakulima kuwekeza katika sekta ya kilimo. Vizuizi vya biashara ya mazao yote ndani ya nchi vitaondolewa. 

Mapinduzi ya kilimo kuasisiwa kwa kusisitiza matumizi ya zana na pembejeo bora. Serikali itashirikiana na benki na taasisi nyingine za fedha kuwasaidia wakulima kujiingiza kwenye kilimo cha kibiashara kinachotumia zana na pembejeo za kisasa. 

Serikali kushirikiana kwa karibu na taasisi za kimataifa kuboresha utafiti wa kilimo na mafunzo na ushauri kwa wakulima. Serikali itatenga alau asilimia 5 ya bajeti yake kuimarisha utafiti wa kilimo, ushauri na huduma nyingine kwa wakulima. 

Kila wilaya kuhamasishwa kutayarisha na kuutekeleza mpango wa muda mrefu wa kujenga na kukarabati barabara ziendazo vijijini. Asilimia 50 ya fedha za ushuru wa barabara unaotozwa mafuta ya magari utatumiwa kuimarisha barabara za vijijini. 

3. Barabara.

Mawasiliano mabovu ya barabara ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya uchumi na hivyo ni kizingiti katika vita yetu dhidi ya umaskini. Ni wazi kabisa kuwa utaratibu wa makusudi unapaswa kuwekwa na kusimamiwa kwa karibu kuhusiana na ujenzi na ukarabati wa barabara zetu kuu na za vijijini. Rushwa imekithiri katika Wizara ya Ujenzi na inachangia kwa kiasi kikubwa ukarabati hafifu wa barabara zetu. 

Waheshimiwa wananchi, kuweka utaratibu ulio wazi wa kutoa zabuni na kuwajibika kwa watendaji wa serikali na makampuni ya ujenzi kutasaidia sana kupunguza rushwa na kuimarisha matengenezo ya barabara. 

Iwapo nitachaguliwa kuwa Rais, serikali itatayarisha mpango kabambe wa miaka kumi wa kujenga barabara muhimu za kitaifa zitakazounganisha mikoa yote ya nchi yetu. Katika mpango huu tutaazimia kujenga kilomita 300 za barabara safi kila mwaka. Ni wazi kabisa kuwa ili mali asili na nguvu kazi iliyoko mikoa ya kanda ya ziwa na mikoa ya kusini itumike kikamilifu kuinua maisha ya wananchi wa mikoa hii na Watanzania kwa ujumla, barabara kuu ya Mwanza mpaka Dar es Salaam na Barabara ya kusini inayounganisha Mikoa ya Lindi na Mtwara na Dar es Salaam ni lazima zijengwe haraka iwezekanavyo. 

5. Elimu 

Kukua kwa uchumi wa kisasa wenye uwezo wa kuboresha maisha ya wananchi kunategemea sana wafanyakazi wenye ujuzi na maarifa. Kwa hakika utafiti unaonyesha kuwa kukua kwa uchumi wa taifa lolote kunashabihiana kwa karibu na kiwango cha kuwekeza katika sekta ya elimu. Hivi sasa Dunia inashuhudia mapinduzi ya teknologia ya mawasiliano ya habari (Communication and Information technology) ambayo yanaleta mageuzi makubwa ya uchumi na biashara ya kimataifa. Uchumi wa kisasa unatumia kompyuta na mtandao (internet). Kwa hakika mtandao umeondokea kuwa ni kisima kilichojaa kila aina ya habari, taarifa, na data ambazo kila mmoja wetu anaweza kujichotea kwa matumizi yake kwa gharama nafuu kabisa. Ili Tanzania ishiriki kikamilifu na ifaidike na uchumi wa ulimwengu inatulazimu kuweka mkakati wa kuboresha na kupanua elimu toka elimu ya msingi mpaka vyuo vikuu. Pamoja na mambo mengine, iwapo nitachaguliwa kuwa Rais serikali itachukua hatua za makusudi ikishirikiana na taasisi za kimataifa kusambaza matumizi ya kompyuta na mtandao (internet) katika mashule yetu. 

Elimu bora ya msingi ni haki ya kila mtoto. Nikichaguliwa kuwa Rais, itakuwa marufuku kumfukuza mwanafunzi kwa kisingizio cha kukosa ada. Serikali itachukua hatua zote zinazowezekana ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wazazi, mashirika ya dini, taasisi zisizokuwa za kiserikali na wahisani wa nje na ndani kuhakikisha kuwa kila mtoto wa Tanzania anapata fursa ya elimu ya msingi iliyo bora. 

Aidha, Serikali itashiriki kwa nguvu zote katika kuongeza na kuboresha shule za sekondari, vyuo vya kawaida na vyuo vikuu. Mafanikio ya hatua hii yatategemea juhudi za serikali katika kuongeza ufanisi na kubana matumizi yasiyo ya lazima ili sehemu kubwa ya matumizi yalenge katika kutoa elimu. Nikiwa Rais nitafanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa ufanisi unaongezeka na kuondoa kabisa matumizi yasiyo ya lazima katika serikali. 

Waheshimiwa wananchi, huwezi ukazungumzia uboreshaji wa elimu bila kumzungumzia mwalimu. Katika makuzi ya mtoto, umuhimu wa mwalimu huenda ukauzidi hata ule wa mzazi. Waalimu ndio wanaowaandaa vijana kuchukua majukumu yao. Kwa bahati mbaya kabisa serikali ya CCM imekataa kabisa kuuthamini mchango wa waalimu kwenye jamii. Hali za waalimu wetu zimezidi kuwa mbaya siku hadi siku na malalamiko yao yote yamekuwa yakipuuzwa, kukabiliwa na vitisho, na kusimangwa kwa kisingizio kuwa eti ualimu ni 'kazi ya wito' hivyo hawapaswi kulalamika. Kutokana na hali hii utafiti uliofanywa mwanzoni mwa miaka ya tisini ulibaini kuwa kiasi cha waalimu waliokuwa wanaamua kuacha kazi hiyo nchini kilikuwa ni wastani wa 25 kwa mwezi. Kwa kweli mahala kijana anayesomea ualimu kujisikia mnyonge pale anapokutana na vijana wenzake wanaosomea fani nyingine. Nikiwa Rais suala la kuboresha ajira ya ualimu litapewa umuhimu mkubwa. Serikali itafanya juhudi zote kuhakikisha kuwa hadhi na heshima ya kazi ya ualimu inarejeshwa. 

Waheshimiwa wananchi, elimu na teknolojia inaongezeka kila wakati. Ili tusiachwe nyuma inatubidi tujenge mazingira yatakayowezesha kushamiri utamaduni wa kujiendeleza kielimu katika maisha yetu. Hivi sasa wananchi wengi hawajisomei. Ni lazima maktaba zifufuliwe na zilizopo kuimarishwa. Wachapa vitabu na majarida ambao karibu wote hivi sasa wamefirisika kutokana na gharama kubwa za uendeshaji zinazosababisha bidhaa zao zishindikane kuuza, wapewe msukumo kufufua shughuli zao. Viwango vya kodi inayotozwa kwa wachapishaji na bidhaa za kielimu kwa ujumla, vifanyiwe marekebisho makubwa ili kushusha gharama na hatimaye bidhaa hizo ziwafikie wananchi kwa bei ambayo wataimudu. 

Waheshimiwa wananchi, ili kuhakikisha kuwa fedha si kisingizio katika kuipa sekta ya elimu msukumo unaohitajika, nikichaguliwa kuwa Rais tutalenga kutumia asilimia 25 ya matumizi yote ya Serikali katika kuimarisha sekta hii. 

6. Afya.

Kusambaratika kwa sekta ya afya nchini siyo kitu cha bahati mbaya, ni matokeo ya sera. Bajeti ya serikali ya awamu ya tatu katika sekta ya afya imepunguzwa sana. Matumizi ya kawaida ya serikali ya kununulia madawa yalipunguzwa toka shilingi 27.8 bilioni mwaka wa mwisho wa Rais Mwinyi mpaka kufikia shilingi 4.8 bilioni mwaka wa pili wa Rais Mkapa. Vigogo serikalini hawaoni sababu yoyote ya kuipa sekta hii msukumo kwa sababu wao na familia zao wanapimwa afya zao na kutibiwa nje ya nchi, kwa fedha za walipa kodi. 

Waheshimiwa wananchi, kuna haja kubwa kuhakikisha kuwa suala la afya linapewa umuhimu unaostahili. Ni lazima tujenge mazingira yatakayo uhakikishia umma kuwa kuna nia ya dhati kabisa ya kuifufua na kuiboresha sekta hii. Waandaliwe madaktari na wauguzi kwa wingi zaidi na wapewe motisha wa kutosha ili wasilazimike kutukimbia. Hospitali, vituo vya afya, na zahanati mpya zijengwe na zilizopo zipanuliwe na kuimarishwa. Madawa ya tiba ya msingi yawepo na yawe ya gharama nafuu. Katika zahanati na hospitali za serikali wananchi wasinyimwe tiba kwa kukosa fedha za kuilipia. Uandaliwe utaratibu utakaotuhakikishia kwamba Mtanzania yoyote hatakosa kupata matibabu kwa sababu tu ameshindwa kumudu gharama. Lakini lililo la msingi kabisa ni kufufua na kuimarisha huduma ya afya ya kinga. Uboreshaji wa mazingira ni sehemu muhimu kabisa katika utoaji wa huduma ya afya ya kinga. Ni lazima taka zizolewe na tuharibu vyanzo vya maradhi. Hatuna budi kurejesha utaratibu uliochwa siku nyingi zilizopita wa kudhibiti wadudu wanaobeba vimelea vya maradhi, hususan mbu. Pamoja na haya yote ni lazima tuhakikishe kuwa suala la uhaba wa maji salama kwa matumizi ya majumbani linapatiwa ufumbuzi wa haraka kabisa. 

Waheshimiwa wananchi, nikiwa Rais serikali yangu itapitisha sheria inayowazuia viongozi wa serikali na familia zao kuchota fedha za umma kwa ajili ya kupimia afya na kupatiwa matibabu nje ya nchi. Hii itakuwa kwa lengo la kuelekeza fedha zitakazookolewa kwenye kuboresha huduma katika mahospitali ya ndani ya nchi. Viongozi wote watalazimika kupata huduma za matibabu kwenye hospitali za nchini na yule atakayeona kwamba anahitaji huduma nje ya nchi atalazimika kutumia fedha zake au kuomba michango kama wanavyofanya Watanzania wengine wenye haja hiyo. 

6.1. Kupambana na Ukimwi.

Ukimwi hivi sasa ni tishio kubwa linaloashiria maangamizi si kwa taifa letu tu, bali pia katika nyingi ya nchi zinazoendelea hususan katika bara letu la Afrika. Inakadiriwa kuwa nchini mwetu katika kila watu mia moja waishio mjini, 25 wana virusi vya ukimwi. Hata huko Vijijini hali si shwari. Inakadiriwa kuwa vijijini kuna wananchi 10 wenye virusi vya ukimwi katika 

kila wanakijiji 100. Tukiendelea kuuonea haya ukimwi utatumaliza. 

Waheshimiwa wananchi, wanawake wanaathirika vibaya zaidi na ukimwi. Kimaumbile ni rahisi zaidi kwa wanawake kuambukizwa virusi vya ukimwi kuliko wanaume. Katika kila watanzania watano wenye virusi vya ukimwi, watatu ni wanawake na wawili ni wanaume. Naomba tuelewe vizuri kuwa wanawake wengi wanaoambukizwa ukimwi sio kwa sababu za uasharati bali ni kutokana unyonge na umasikini wao. Uhuru wa ukombozi wa wanawake na kuongezeka kwa uwezo wao wa kupata ajira na kujiendesha kimaisha utasaidia sana kupunguza ongezeko la ugonjwa huu kwa wanawake. 

Utafiti katika nchi nyingi umeonyesha wazi kuwa vijana wanaofahamu vizuri athari na jinsi ukimwi unavyoenea, wanajikinga na hawaambukizwi virusi vya ukimwi ukilinganisha na wale ambao hawana elimu ya ugonjwa huu. Kuwapa elimu vijana wetu kuhusu ugonjwa huu ni kuwapa kinga ya radhi hili hatari. Kuanzia mwaka 1985 hatua na mikakati kadhaa imechukuliwa yote ikilenga katika kuelimisha na kuhamasisha jamii juu ya athari za maambukizo ya ukimwi na njia za kudhibiti kuenea kwa maambuki mapya. Hata hivyo pamoja na kampeni hizi, maambukizi ya ukimwi bado yameshika kasi na wanaougua maradhi haya wanazidi kujitokeza. Ni dhahiri kabisa kuwa hatua za ziada zinahitajika. 

Waheshimiwa wananchi, nikichaguliwa kuwa Rais tutaweka mkakati wa kitaifa utakaolenga kupunguza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa mtu ambaye hivi sasa hana virusi vya ukimwi, kuambukizwa ugonjwa huu. Pamoja na mambo mengine mkakati huu utalenga katika kuishirikisha jamii katika mjadala wa kutunga sera mahsusi ya nchi itakayosimamia mapambano dhidi ya ukimwi kwa nia ya kufanikisha malengo yafuatayo: 

( Kuondoa utaratibu wa sasa unaofanya taarifa za maambukizi ya ukimwi kuwa ni siri na badala yake taarifa hizi ziwe za wazi kama ilivyo kwa magonjwa mengine. 

( Kufikia makubaliano ya kitaifa ni nini kifanyike ili kudhibiti kwa kiwango cha juu kabisa uwezekano wa maambukizi kwa wananchi wetu ambao bado kuambukizwa. 

( Kuweka taratibu na mikakati rasmi ya kukinga maambukizi mapya katika sehemu za kazi, mashule, vyuo vya elimu, majeshi, na taasisi nyingine. 

( Kuweka taratibu na mikakati rasmi ya kukinga maambukizi mapya kutokana na tendo la ndoa. 

( Kuweka taratibu za kuwahudumia walioambukizwa virusi vya ukimwi katika hospitali na vituo vya afya vilivyopo nchini. 

( Kuanzisha utaratibu wa makusudi wa kuziunga mkono na kutoa kila aina ya msaada unaowezekana, juhudi za watafiti wa kizalendo ikiwa ni pamoja na waganga wa jadi katika kutafuta tiba au kinga dhidi ya maambukizo ya virusi vya ukimwi. 

Waheshimiwa wananchi, pamoja na sera tunayokusudia kuiunda, nikichaguliwa kuwa Rais serikali itaanzisha uhusiano wa karibu na taasisi za kimataifa, na shirika la Afya ulimwenguni WHO utakaolenga katika kufungua vituo maalum vya kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu na kutoa tiba inayopunguza athari na kuongeza muda wa kuishi kwa wale wenye virusi. 

7. Katiba Mpya 

Demokrasia ya kweli na ushindani wa kisiasa unaotoa haki sawa kwa washiriki wote, uhuru wa kusema na uhuru wa vyombo vya habari, ni msingi wa utawala bora. Demokrasia ni lengo la maendeleo ya kisiasa lakini pia ni nyenzo ya kujenga uchumi kwani inasaidia sana kuzuia kuenea kwa sarakani ya rushwa. Demokrasi ya kweli inawafanya viongozi wawajibike kwa wananchi. 

Kujenga misingi imara ya demokrasia ya kudumu tunahitaji Katiba nzuri inayowapa uhuru wa kweli watanzania wa kuchagua na kuchaguliwa. Muungano wetu utaimarika ikiwa Watanganyika na Wazanzibari watahisi wana haki sawa katika Muungano huo. Katiba ya sasa haikidhi maendeleo ya demokrasia nchini mwetu. Nimemteua mgombea mwenza ambaye ni Mwanasheria Maarufu Zanzibar na pia ni mwenyekiti wa Zanzibar Law Society. Yeye ni mwanaharakati wa Haki za Binadamu na mjenzi wa demokrasia ya kweli. Wakili Nassor Khamis atanisaidia sana katika kusimamia uundaji wa Katiba mpya ya Watanzania wenyewe itakayoweka misingi ya utawala bora. 

8. Utawala Bora

Maendeleo ya Uchumi yatakayoinua hali ya maisha ya wananchi kwa muda mrefu yanahitaji utawala bora wenye sera zilizo wazi na zinazotabirika. Kila mwananchi awe na uhuru wa kumiliki mali aliyoipata kwa njia za halali. Ni wajibu wa serikali kujenga mazingira yatakayomwondolea mwananchi hofu kuwa mali yake aliyoichuma kihalali haitapokonywa na serikali au majambazi kwa kisingchochote kile. Sera na utendaji wa serikali uweke mazingira ambayo yatatoa motisha kwa wananchi kufanya kazi kwa bidii na kwa ufanisi ili kujiendeleza kiuchumi na kibiashara. 

Nikichaguliwa kuwa Rais, tutashirikiana na wananchi kujenga mfumo wa uwajibikaji. Watendaji wa serikali ikiwa ni pamoja na viongozi wa juu watawajibika mara moja pindi itakapodhihiri kuwa majukumu waliyokabidhiwa yamewashinda. 

Rushwa siyo tu kuwa ni adui wa haki, lakini pia ni adui mkubwa wa maendeleo. Rushwa ni sarakani (cancer) inayoua uchumi na kuwanyima wananchi haki ya maisha na maendeleo. Rushwa katika Tanzania imekithiri. Taasisi ya kimataifa inayochunguza ukuaji wa rushwa imeorodhesha nchi mbalimbali ulimwenguni kwa umahiri wa rushwa. Tanzania ni ya saba katika ulimwengu mzima, na ni ya tatu katika nchi za Kiafrika. Serikali inapoteza mabilioni ya kodi ambazo hazilipwi na waagizaji wa bidhaa. Matengenezo ya barabara ni hafifu japokuwa gharama inayotajwa ni kubwa. Madawa yaliyomaliza muda wake wa kutumika yanaingizwa nchini. Mitihani inavuja na kwa hivyo haipimi uwezo wa wanafunzi wetu. Mabilioni ya fedha za walipa kodi yanafujwa kila mwaka kwa matumizi ya ajabu ajabu. 

Chanzo kikubwa cha rushwa ni ukiritimba wa madaraka, mishahara midogo ya watendaji serikalini, maamuzi yasiyofuata taratibu zinazoeleweka na kutowajibishwa kwa wanaoshiriki katika vitendo vya rushwa. Vita dhidi ya rushwa itafanikiwa ikiwa ukiritimba wa madaraka utaondolewa, maamuzi ya kiserikali yatafuata taratibu zilizo wazi na zinazoeleweka na kuwaadabisha wanaoshiriki katika rushwa. Ni lazima tujenge mazingira ambayo yatatuhakikishia kuwa "SAMAKI WAKUBWA" wanaoshiriki katika rushwa wanashughulikiwa kwanza kabla ya kuwashughulikia 'dagaa'. Nikiwa Rais vita dhidi ya rushwa itachukua sura mpya kabisa. Hakutakuwa na kuoneana haya wala kujuana. Kwa kweli kila aliyepata kuwa mwanasiasa kwenye nchi hii na wale waliopata kuteuliwa na wanasiasa kusimamia majukumu mbalimbali ya umma itabidi watuthibitishie kuwa mali walizonazo hazikuchangiwa na rushwa. Tutakuwa ngangari kuhakikisha kuwa VIGOGO wa rushwa bila kujali kuwa ni walaji au watoaji wanafikishwa mahakamani na kuhukumiwa ili wawe mfano kwa wengine. Tutasaidiana na timu ya wataalamu wachunguzi kuweka mikakati ya kuwanasa " MAGWIJI WA RUSHWA " na kujenga mazingira yatakayowafunza watendaji serikalini kuogopa kupokea rushwa. 

FEDHA ZA KUGHARAMIA MIPANGO YA MAENDELEO ZITAPATIKANA WAPI?

Waheshimiwa wananchi, bila shaka mtajiuliza: Mambo yote haya yanahitaji fedha; Je, fedha zitapatikana wapi kuinua viwango vyetu vya elimu, kuongeza huduma za kilimo, kuimarisha huduma za afya na kupambana na ukimwi, kujenga barabara, na kuweka mazingira bora kwa wawekezaji wa ndani na nje ili kuanzisha shughuli za kiuchumi zitakazoongeza ajira? 

Kwanza kabisa inatupasa tuelewe kuwa pamoja na majigambo ya serikali ya awamu ya tatu kuwa imeongeza ukusanyaji wa kodi, mfumo wetu wa kodi bado ni mbaya, ambao unawabana wafanyabiashara wadogo na wale wa kati kulipa kodi na wakati huo huo kusamehe makampuni makubwa kwa kisingizio kuwa wao ni wawekezaji. Sehemu ya pato la Taifa linalokusanywa kama kodi limepungua toka asilimia 13.4 mwaka 1996 mpaka kufikia asilimia 11.2 mwaka 1999. Tanzania inakusanya sehemu ndogo ya pato la taifa kama kodi ukilinganisha na wastani wa asilimia 15 wa nchi nyingine za Kiafrika. Kwa kuongeza uwajibikaji wa mamlaka ya kodi, kuondoa misamaha ya kodi isiyo ya lazima, kupunguza viwango vya kodi na kuongeza adhabu ya kukwepa kodi, Tanzania pia inaweza kukusanya alau asilimia 15 ya pato la taifa kama kodi. 

Pili, serikali inawajibika kubana matumizi kwa kuondoa matumizi yote ambayo siyo ya lazima, ikiwa ni pamoja na kupunguza ukubwa wa serikali yenyewe. Tutapunguza safari za nje za viongozi. Serikali yetu itakuwa na wizara chache zisizozidi kumi na tano. Misaada yote toka nje kusaidia elimu, afya, ujenzi wa barabara na mawasiliano haitanyofolewa na kutumiwa kwa matumizi ambayo hayakukusudiwa. Tatu, tunatarajia vita yetu dhidi ya rushwa iwe na msukumo mkubwa katika kupunguza matumizi hewa ya serikali, kuongeza ukusanyaji kodi na kupata malipo ya haki kwa mali ya umma inayobinafsishwa. Nne, tutaweka mazingira mazuri sana kwa wawekezaji kutoka nje na ndani kuweza kuwekeza mitaji yao kwenye huduma za maji, barabara, reli, na mawasiliano. 

Pamoja na haya yote, nikichaguliwa kuwa Rais, Serikali itaacha kutumia utaratibu wa sasa wa cash budget. Kwa miaka mitano iliyopita bajeti inayoidhinishwa na Bunge na matumizi halisi katika wizara na sekta mbali mbali ni vitu viwili tofauti kabisa. Bajeti ya serikali yetu siyo tu kwamba itazingatia gharama halisi, bali pia itazingatia makadirio ya mapato yaliyo sahihi. Mapengo ya muda mfupi kati ya matumizi na mapato yatazibwa na mikopo toka Benki Kuu ya Tanzania. 

9. Kufuta Kodi Zinazonyanyasa Wananchi.

Waheshimiwa wananchi, kodi ya maendeleo imekuwa ni kero kubwa kwa wananchi. Kwa kweli kuiendeleza kodi hii ni kutozingatia hali halisi ya nchi yetu. Wananchi walio wengi hawana uahakika wa chumo. Kutokana na hali hii msimu wa kulipa kodi ya maendeleo unapofika wananchi wengi wamekuwa wakikosa haki za kimsingi za binadamu ikiwa ni pamoja na haki ya maisha. Kuna taarifa kuwa wananchi kadhaa katika baadhi ya maeneo ya nchi yetu tayari wamekwisha poteza maisha kutokana na vipigo na mateso mengine waliyopata kutokana na kushindwa kuilipa kodi hii. Pili, matumizi ya kodi hii yamekuwa hayaeleweki, na wananchi wanapoomba wapewe taarifa wamekuwa wakijipalia mkaa. Hapa kuna wasiwasi mkubwa kuwa kodi hii imekuwa ikitumiwa kinyume na makusudio yake na ndio maana taarifa za matumizi yake zimekuwa ngumu kutolewa hata pale wananchi wanapozidai. Tatu, kodi hii imekuwa ni mzigo mzito kwa wafanyakazi. Jijini Dar es salaam kila mfanyakazi aliyeajiriwa kwenye sekta rasmi amekuwa akikatwa asilimia moja ya mshahara wake kila mwezi kama kodi ya maendeleo. Hata hivyo sababu hasa za makato haya hazieleweki ikizingatiwa kuwa wakaazi wa jiji wanajigharamia kwa takriban kila kitu ikiwa ni pamoja na huduma za maji, elimu, afya, usombaji taka na maji machafu. 

Waheshimiwa wananchi, iwapo nitachaguliwa kuwa Rais kodi ya maendeleo nitaifuta. Hii ni kodi ya kikoloni inayonyanyasa watu walio wanyonge. Aidha nitahakikisha kuwa suala la wale wanaodaiwa kuwa wamepoteza maisha kutokana na kadhia ya kodi hii linafanyiwa uchunguzi wa kina ili ukweli uingizwe kwenye kumbukumbu na haki kutendeka. 

Waheshimiwa wananchi, hakuna takwimu za kitaifa za wananchi waliolipa kodi ya maendeleo. Wanaume wenye umri wa miaka 18 au zaidi hawazidi milioni 7. Tunakisia kuwa wanaolipa kodi ya maendeleo hawazidi milioni 5. Ikiwa kila mtu analipa shilingi 5000/-, kodi inayokusanywa haizidi shilingi bilioni 25. Hata kama wote milioni 7 wanalipa kodi, mapato hayazidi bilioni 35 ambayo ni chini ya asilimia 5 ya kodi inayokusanywa na serikali kuu. Shirika la fedha la kimataifa IMF, linakisia kuwa serikali inapoteza shilingi bilioni 45 kila mwaka kutokana na ukwepaji wa kodi ya mafuta.Uimarishaji wa ukusanyaji wa kodi za serikali kuu utatosheleza kabisa kufidia pengo litakalotokana na kufutwa kodi ya maendeleo. Aidha, serikali za mitaa zitahamasishwa kutafuta vianzio vingine vya kodi inayowiana na uwezo wa wananchi kulipa kodi bila kuathiri motisha wa uzalishaji bidhaa na utoaji huduma. 

10.Umoja Wa Kitaifa.

Waheshimiwa Wananchi, ili tuweze kujenga nchi yenye haki sawa kwa wote na tujenge uchumi imara utakaoleta neema kwa wote ni lazima tuing'oe CCM. Watanzania wamechoka na CCM na wanahitaji uongozi mpya. Napenda kuwahakikishia kuwa Tanzania ni nchi yenye kila sababu ya kuweza kufikia maendeleo makubwa na ya haraka. Hata hivyo katika mazingira ya sasa hilo ni muhali. Mazingira tuliyonayo hivi sasa yameshamiri ufisadi, rushwa, na visingizio. Ni mazingira ambayo haki haipatikani ila kwa kuangalia sura, nasaba, uwezo wa kiuchumi, itikadi za kisiasa, dini ya mtu, na pengine hata jinsia. Ni mazingira ambayo mbegu za mfarakano zinapandikizwa kwa makusudi kabisa bila ya kujali athari zake kwa siku zijazo. 

Waheshimiwa wananchi, moja ya kero kubwa sana zinazowakabili wananchi leo hii ni kutosikilizwa. Milango ya majadiliano kwa lengo la kutatua migogoro imefungwa. Mahakama zetu siyokinga tena. Wote tunashuhudia jinsi amri za muda za mahakama zinazoizuia serikali kufanya jambo fulani zinavyopuuzwa. 

Haki ya watu kujiunga na kujumika katika vyama vyao vya hiari iko chini ya huruma ya serikali. Baraza la Wanawake Tanzania (BAWATA), Muungano wa Wamiliki wa Daladala (MUWADA), na Umoja Wa Vijana Tanzania (Tanzania Youth Forum) ni miongoni mwa jumuia za wananchi ambazo zimezuiliwa kufanya shughuli zake bila sababu za msingi. Lakini, haki iko njiani. Sera ya Chama Cha Wananchi - CUF ya HAKI SAWA KWA WOTE inatoa matumaini ya kuwajengea Watanzania maisha mapya. Hili CCM wanalijua na linawauma. 

Waheshimiwa wananchi, CCM, serikali yake, vyombo vyake vya habari, na wapambe wake wengine wana kazi kubwa hivi sasa ya kujaribu kuwazuia wananchi wasikiunge mkono chama chao, yaani CUF. Kila siku maneno yanabadilika. Mara CUF ni chama cha Wapemba, mara CUF ni chama cha Waarabu, na sasa CUF ni chama cha waislamu. Kama CUF ni chama cha kipemba kwa sababu katibu wangu mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad ni Mpemba, basi CCM inastahili hukumu hiyohiyo kwa kuwa makamu wa Rais wa serikali yake naye ni Mpemba. Kama CUF ni chama cha Waarabu kwa sababu baadhi ya wanachama wetu ni Watanzania wenye asili ya kiarabu, je, CCM iko tayari kutangaza hadharani kwamba kwa kuwa chama hicho ni cha 'Watanzania weusi' basi inawafukuza kwenye chama hicho wanachama wake wote wenye asili ya Kiarabu na Kihindi ambao baadhi yao hivi sasa ni makada wa kutegemewa wa chama hicho? Kama CUF ni chama cha waislamu kwa sababu kina wanachama wengi waislamu, je, CCM iko tayari kusimama hadharani na kuwaambia wanachama wake walio waislamu waondoke kwenda kwenye 'chama chao' cha CUF, kwa kuwa huko waliko ni kwa wale wasio waislamu tu? 

Waheshimiwa wananchi, CCM iko tayari kueneza fitna, uhasama na ufisadi wenye lengo la kuwagawa wananchi alimradi tu hali hiyo itawabakiza kwenye madaraka. Hawa si watu wa kuwasikiliza hata kidogo. Wameifanya Tanzania iwe nambari one kwa umaskini na sasa wanaeneza propaganda yakuathiri mshikamano wetu wa kitaifa. 

Waheshimiwa wananchi, nikichaguliwa kuwa Rais pamoja na majukumu mengi yatakayonikabili, sintasau kamwe umuhimu wa kujenga mazingira ambayo haki itashamiri. Pamoja na mambo mengine, tume huru ya haki za binadamu itaundwa ambayo pamoja na mambo mengine itapokea malalamiko ya wananchi, kuyafanyia uchunguzi wa dhati, na kuwafikisha wakiukaji wa haki mahakamani. Chini ya serikali ya CUF, mahakama itapatiwa uhuru wake na vitendea kazi ili kiwe ndio chombo cha juu kabisa kwenye utatuzi wa migogoro. 

Waheshimiwa wananchi, nafarijika sana kuwa wengi mmeonyesha imani ya dhati juu yangu kama mgombea. Naomba tusaidiane zaidi kuwahamasisha wananchi wote wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na kuendelea wajiandikishe na kupiga kura, na baada ya hapo wawe ngangari kusimamia ulinzi wa kura zao. 

Waheshimiwa wananchi, CCM wanatamba. Wanadhani kuwa japokuwa ni kweli hawana cha kuwaeleza wananchi, lakini fedha itamaliza udhia wote. Wanaamini Watanzania bei yao ni ndogo. Wamejiandaa kutumia dola na fedha kunyakua ushindi. Tumeona rushwa ilivyokithiri kwenye kura zao za maoni za kuteua wagombea udiwani na ubunge. Wanatumia Radio Tanzania kueneza propaganda ya CCM. Polisi wametumiwa kuzuia baadhi ya mikutano yetu. Lakini sisi tunawaambia: Pamoja na mabilioni yao na utumiaji wa vyombo vya dola, CCM haiwezi kushinda nguvu za wananchi. Kama wazee wetu kwa kuchangia thumni thumni zao waliweza kumng'oa mkoloni, sisi watoto na wajukuu zao kwa shilingi ishirini ishirini zetu, hamsini hamsini zetu, na mia mia zetu hatutashindwa kuing'oa CCM. Ni lazima tuionyeshe CCM kuwa safari hii lugha pekee tunayoielewa ni kuwa ngangari katika kulinda haki na maendeleo yetu. 

Waheshimiwa wananchi, pamoja na mambo mengine, 'niliyoyaelezea ndiyo mkataba baina yetu. Iwapo mtanichagua kuwa Rais sitakuwa na cha kuwalipa zaidi ya HAKI NA MAENDELEO.

HAKI SAWA KWA WOTE 

Juu
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI
Kama hamtaki demokrasia, mnataka nini basi?

Prof. Lipumba ana uwezo wa kuongoza nchi - CCM

Kampeni za uchaguzi 2000, CCM yamalizia muda wake na kusema:
Imefanya kazi ya ‘kuipendeza’ Marekani

Vita dhidi ya rushwa ianzie kwa vigogo -Lipumba

Wakati umefika wanawake kushiriki siasa - Mugissa

TLP yadaiwa kuukejeri Uislamu

CUF Kigamboni kuzindua kampeni leo

USHAURI NASAHA
Nimechoka kuwa mtangazaji wa redio

MAKALA
Mungu na mataifa ya dunia

MAELEZO BINAFSI
Mjue mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Lipumba

MIPASHO NASAHA
Krosi matiplikesheni!

MAKALA
Wananchi kajiandikisheni kupiga kura ili kuleta mabadiliko ya serikali kwa njia ya amani

KALAMU YA MWANDISHI
Mkijirekebisha mtakaribishwa

Habari za Kimataifa

LISHE
Unakula au unaliwa?

MASHAIRI

MICHEZO

  • Yanga, Mtibwa nani bingwa leo?
  • Ugomvi mkubwa baina ya Simba na Yanga waibuka 
  • Arsenal yaitandika Liverpool
  • Ngorongoro Heroes yaenda Msumbiji

  •  


    Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita