AN-NUUR 
Na.183 Ramadhan 1419, Januari 8 - 14, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Historia: Form IV 

Upinzani dhidi ya Serikali ya Kiislamu wakati wa Khalifa wa Pili Umar Bin Khatab 
 

Umar aliukagua mji wa Jerusalem. Muda wa swala ulipofika Bishop aliwaruhusu waswali kanisani, lakini Umar aliogopa kuswali humo kusije kuwa hoja ya kuchukua kanisa hilo, hivyo aliswalia nje kwenye ngazi. Hata hapo aliacha maandishi yanayokataza kuchukua sehemu hiyo. 

Umar akiwa Jerusalem aliweka jiwe la msingi la msikiti unaojulikana kwa jina la msikiti wa Umar wa Jerusalem. Inasadikiwa kuwa msikiti huu umejengwa kwenye uwanja ambao Mtume Yakub alipewa Wahy na lilipojengwa hekalu la Solomon.75 

Pamoja na kutekwa Jerusalem Warumi walijaribu kuirejesha Syria katika Himaya yao. Watu wa Jazirah kwa sasa ni sehemu ya magharibi ya iraq walikula njama ya kuwaondoa Waislamu Syria. hericlus alipeleka jeshi lake na wakavamia Hims. Hata hivyo walishindwa na Jazirah ikatekwa chini ya ukamanda wa Ayad bin Ghanam. 

Kutekwa kwa Misri 

Misri ilikuwa jimbo la Dola ya Warumi. Warumi waliofukuzwa Palestina Syria walikimbilia Misri, hali hii ilihatarisha usalama wa Dola ya Kiislamu hasa kwa vile Misri iko karibu na miji hiyo. Isitoshe Misri iko karibu na Makka jambo ambalo pia lilihatarisha usalama wa Waislamu. Si hivyo tu bali Alexandria kilikuwa kituo kikubwa cha jeshi la maji la Warumi. Hali kadhalika Misri ilikuwa lango kubwa kati ya Arabuni na Afrika ya kaskazini. Isitoshe Warumi walikuwa wanajitahidi kufanya njama ili wakomboe sehemu zilizotekwa. Sababu hizi zilipelekea kuwavamia Misri mnamo mwaka 18 A.H. sawa na 639 A.D. Waislamu waliiteka ngome ya Warumi ya Fusta. Warumi walipostuka na kupeleka jeshi kubwa kamanda wa jeshi la Kiislamu Amr bin al-As alipata askari wengine kutoka kwa Khalifa na walielekea alexandria. Mji huu ulizingirwa kwa miezi sita hatimae ukatekwa na Waislamu mwaka 642 A.C. na baadhi ya wanahistoria wanasema ulitekwa 640 A.D. sawa na 20 A.H. Baada ya ushindi huu Misri ikawa chini ya Himaya ya Kiislamu. 

Hivi ndivyo vitimvi vya Warumi na Wapeshia wakati wa Ukhalifa wa Umar. Umar alifariki 23 A.H. sawa na (643 A.C.) akiwa na umri wa miaka 61 (sitini na moja). 

Palikuwa na mtumwa wa Kiajemi aliyemlalamikia tajiri yake kwa Khalifa kuwa anamfanyisha kazi ngumu. Madai haya yalikuwa uongo na Khalifa Umar aliyadharau. Mtumwa huy anaeitwa Lu-Lu-Firoze alijificha katika pembe moja ya msikiti. Na Khalifa alipokuwa anakwenda kuswali alfajir alivamiwa na kupigwa majambia mara sita na mtumwa huyu. Ingawa watu walimkamata lakini alijiua na jambia lile lile. Asubuhi yake al-Faruq Umar Kamanda wa waumini alifariki. 

Upinzani dhidi ya Serikali ya Kiislam wakati wa Khalifa wa tatu, Uthman bin Affan 

Wakati wa ukhalifa wa Uthman upinzani ulitokea kutoka kwa Warumi, Wapeshia na kutoka Waislamu wenyewe. 

Kama ilivyokwisha elezwa uthman alianza ukhalifa tangu mwaka 24 A.H. na akauliwa mnamo mwaka 36 A.H. sawa na (644-656 A.D.). Hali kadhalika tumeshaeleza alivyo chaguliwa na kuwa Khalifa. 

Upinzani toka kwa Waajemi na Warum

Maadui wa nje Warumi na Wapeshia hawakuwa na sababu mpya za kuendeleza upinzani ila kwa sasa waliendeleza upinzani ili kukomboa sehemu zao zilizotekwa. Tangu wakati wa mtume (s.a.w.) hadi wakati wa umar, Warumi waliipoteza Syria, na Alexandria na Misri. Warumi waliiangalia Syria na Alexandria kwa jicho la wivu na wasingevumilia kuziachia hivi hivi. Hivyo mnamo mwaka 25 A.H. sawa 645 A.C. kulikuwa na maasi makubwa katika mji wa Alexandria yalichochochewa na Warumi, na katika mwaka 26 A.H. Warumi wakavamia alezandria na kuurudisha mikononi mwao. Kahlifa Uthman alipopata taarifa hii alimuamuru kamanda Amr bin al-As kuzima uasi na kuyafukuza majeshi ya Warumi. Kamanda amr aliwashambulia Warumi na kuwafukuza nje ya Alexandria na kwa mara nyingine Alexandria ikawa chini ya Dola ya Kiislamu. Hata hivyo Warumi hawakukata tamaa walivamia tena mji wa Alexandria na jeshi la wanamaji lenye meli 500 mnamo mwaka wa 31 A.H. sawa na 651 A.C. Waislamu hao walijiandaa Muawiya gavana wa jimbo la Syria tayari nae alikuwa na jeshi la wanamaji. Hivyo alituma jeshi lake la wanamaji chini ya ukamanda wa Abdullah bin Sarah na wakapambana baharini. Vita hivi vya wanamaji ndivyo vilikuwa vya kwanza katika historia ya Uislamu. Ingawa Waislamu walikuwa wageni kwenye vita vya majini, haikuwawia vigumu kuwadhinda adui ambao walikimbilia kisiwa cha Cicily. 

Kwa kuimarisha usalama wa jimbo la Misri na Dola ya Kiislamu kwa ujumla, ilikuwa lazima kwa Waislamu kuiteka ngome kubwa ya Warumi iliyokuwa Tripoli (kwa sasa Libya). Kwa sababu hii Abdullah bin Sarah alipoteuliwa kuwa gavana wa jimbo la Misri, aliomba ruhusa kwa Khalifa Uthman aitwae ngome ya Warumi iliyoko Tripoli. Baada ya mapigano na wakazi wa Tripoli walikubali suluhu kulipa Jizya ya Dirham milioni mbili na nusu kwa mwaka. Mapigano baina ya jeshi la Warumi na Waislamu yalifanyika mahali paitwapo Yaquba. Lakini kamanda wa upande wa adui akauawa na majeshi ya Warumi yakashindwa. kwa ushindi huu Waislamu waliteka sehemu za tunisia, Morocco na sehemu ya Algeria. 

Uasi wa Azerbaijan na Armenia 

Mnamo mwaka wa 26 A.H. kulitokea maasi katika jimbola Azerbaijan dhidi ya serikali ya Kiislamu, jimbo hili lilikuwa chini ya Himaya ya Kiislamu tangu wakati wa Umar. Khalifa Uthman alimuamuru Walid bin Uqba gavana wa kufa kuzima uasi wa Azerbaijan. 

Katika mwaka huo huo watu wa Armenia waliokuwa chini ya Dola ya Kiislamu tangu wakati wa Umar waliasi. Amir Muawiya Gavana wa Syria alipeleka jeshi Armenia kukutana na Warumi. Mfalme wa Warumi Constantine II alituma jeshi la watu 80,000. Kuona hali hii Muawiya aliomba msaada wa Askari kutoka kwa Khalifa uthman. Jeshi likatumwa chini ya ukamanda wa Habib bin Muslimah, katika mapigano haya Warumi walishindwa na Armenia ikatekwa. Baada ya ushindi huu Waislamu waliteka karibu Asia Minor yote pamoja na Aran na Garjastan. 
 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
Tahariri 
Onyesheni ushujaa wa Badri 

Daniel kuwatimua waumini Msikitini 

Waislamu Moshi: Wadai kulishwa nguruwe, vibudu 

Dondoo za Kisakolojia 
Na. Abu Halima Sachangwa 

Kona ya WachaMungu  

Jicho la Uzalendo 

Maulana Sayyid Jamal-Din Afghan 1214 - 1254 (1838-1897) - 2 

Vipi umoja wetu uwe hatari ? 

MASHAMBULIZI YA MAREKANI NCHINI IRAQ  

Marekani si rafiki mwema  

Tunahitaji UN ya Waislamu - 2  

Njia bora zitakazotusaidia kuwalea watoto 
Na Ust. Hashim Rusaganya, Mombasa 

Ijue Madrasatul-Qaadiriya Sokoni I Arusha. 
Na Habiba Swedi, Arusha 

Tutafute kwanza ufalme wa Allah (s.w.) 
Na Mwapwani Mohammed 

Sheikh Kisiwa atunuku zawadi 

Chuo cha Kilimo Ukiriguru kupata Msikiti mpya  
Na Mwandishi Wetu, Mwanza  

Huduma za maji Kondoa haziridhishi 
Na Abu Zuberi, Kondoa  

Mnyororo wa imani 
Na Sheikh Bernard P. Nyangasa 

Je, Yesu alibatizwa? 
Na Muhibu Said  

Kufuatia Waislamu kuritadishwa Merela Morogoro: Masheikh wa mjini watupiwa lawama  

Abiria walaani kumwagiwa pombe Kondoa 

Sheikh Bafadhil ateuliwa kudhamini waandishi wa habari Morogoro 
Na Mussa Ally, Morogoro 

Sayansi na Teknolojia 
[Tatizo la mwaka 2000] 

Masomo ya Dini ya Kiislamu 

Barua za Wasomaji 

Chakula na lishe 
[Mlo wa siku ya Idd] 


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita