|
|
| Waislamu
Moshi:
Wadai kulishwa nguruwe,
vibudu
Wamedai kwamba umekuwepo utaratibu wa mganga mmoja wa nyama kupima nyama ya ng’ombe, mbuzi na nguruwe kwa wakati mmoja na bila kubadili vifaa. Kwa utaratibu huo wamedai kwamba muhuri unaotumika kuwekea alama nyama ya nguruwe ndio huo huo hutumika kwa nyama ya ng’ombe na mbuzi. Kutokana na madai hayo, Katibu wa Bakwata Wilaya ya Moshi Mjini Sheikh Mnyone amekuwa akizungukia Misikiti yote mjini Moshi kuwaeleza Waislamu juu ya hali hiyo na kutafakari pamoja nini cha kufanya. ANNUUR ilipowasiliana na ofisi husika; madai hayo yalikanushwa na kutolewa maelezo kwamba kuna waganga wawili na mihuri tofauti kwa nyama ya nguruwe. Hata hivyo madai hayo yalipingwa na Bw. Mnyone akisisitiza kwamba muhuri ni mmoja labda wabadili sasa baada ya malalamiko haya. Kwa mujibu wa maelezo ya Sheikh Mnyone, madai mengine ya Waislamu ni kuwa machinjio ya nguruwe yapo karibu na makaburi ya Waislamu ambapo uchafu wa wanyama hao hutupwa makaburini hapo. Aidha, nguruwe hao wanapoletwa kuuliwa huachwa wavinjari katika makaburi ya Waislamu. Jambo jingine lililotajwa kama kero ni uchomaji wa mishikaki ya nguruwe karibu na Msikiti wa Suni na hoteli nyingine za kawaida. Vile vile imeelezwa kwamba kufunguliwa kwa mabucha ya nyama ya nguruwe karibu kabisa na kituo cha mabasi cha Kiboriloni ni kero nyingine. Walalamikaji wanadai ama kituo cha basi kihame eneo hilo au mabucha. Kufuatia kero hizo, Katibu wa Bakwata Wilaya amekuwa akiwasilana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkoa ili kutafuta ufumbuzi. Uchunguzi wa gazeti hili umegundua kuwa Mkurugenzi huyo alishapelekewa barua tatu toka mwezi Agosti, 1998 kuhusu suala hili. Kutokana na Ofisi ya Mkurugenzi kutokuchukua hatua yoyote; Katibu wa Bakwata Desemba 21, 1998 alimwandikia barua Mkuu wa Mkoa Mh. Philemon Sarungi akimwomba aingilie kati suala hili. Katika ziara zake Misikitini, Katibu wa Bakwata Sheikh Mnyone amekuwa akikabiliwa na wakati mgumu ambapo Waislamu wamekuwa wakidai ni kwanini halijafanyika jambo la kutoa fundisho kwa Mkurugenzi na wenye machinjio ya nguruwe. Hata hivyo, Sheikh Mnyone amekuwa akiwapoza Waislamu na kuwataka wasubiri majibu ya Mkuu wa Mkoa. Katika maelezo mengine imedaiwa kwamba upo wasiwasi wa watu kulishwa vibudu kwani Halmashauri imekuwa ikiteua wachinjaji bila kuwashirikisha viongozi wa dini. Wasiwasi uliopo ni juu ya umakini na uadilifu wa watu wanaoteuliwa na
Halmashauri kuchinja kama hawawezi kutumika "kuhalalisha" kilichokufa bila
kuchinjwa. Ombi la Bakwata ni kwamba ishirikishwe kuwateua wachinjaji ili
kuondoa wasiwasi wa kulishwa vibudu.
|
YALIYOMO
Tahariri Onyesheni ushujaa wa Badri Daniel kuwatimua waumini Msikitini Waislamu Moshi: Wadai kulishwa nguruwe, vibudu Dondoo za Kisakolojia
Maulana Sayyid Jamal-Din Afghan 1214 - 1254 (1838-1897) - 2 MASHAMBULIZI YA MAREKANI NCHINI IRAQ Njia bora zitakazotusaidia kuwalea
watoto
Ijue Madrasatul-Qaadiriya Sokoni
I Arusha.
Tutafute kwanza ufalme wa Allah (s.w.)
Chuo cha Kilimo Ukiriguru kupata
Msikiti mpya
Huduma za maji Kondoa haziridhishi
Mnyororo wa imani
Je, Yesu alibatizwa?
Kufuatia Waislamu kuritadishwa Merela Morogoro: Masheikh wa mjini watupiwa lawama Abiria walaani kumwagiwa pombe Kondoa Sheikh Bafadhil ateuliwa
kudhamini waandishi wa habari Morogoro
Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|