AN-NUUR 
Na.183 Ramadhan 1419, Januari 8 - 14, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Mlo wa siku ya Idd 

Na Mujahid Mwinyimvua 

IDD - el - Fitr ni sikukuu inayoanza baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Katika makala zetu maalum za chakula na lishe za mwezi huu wa Ramadhani, tulijifunza mlo wa futari na mlo wa daku. Ni vyema pia wiki hii tukajifunza mlo wa siku ya Idd el Fitr. 

Kwa kawaida mwili wa mwanaadamu huweka akiba ya chakula. Chakula hicho hutumika wakati wa mazingira fulani kama vile pale ambapo mwili wa mwanadamu unapokosa chakula (kipya) yaani mtu akikaa masaa kadhaa bila kula. Funga ya Ramadhani ni mfano wa hali ya mwili kukaa masaa fulani bila ya chakula. 

Kwa maneno mengine tunaweza kusema kwamba ibada ya funga ya Ramadhani inausaidia mwili kutumia chakula chake cha akiba. Chakula hicho cha akiba kikikaa kwa siku nyingi mwilini bila ya kutumika kinaweza kuleta magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na ulaji (vyakula). 

Mtu anapomaliza mfungo wa mwezi wa Ramadhani sehemu fulani ya chakula chake cha akiba huwa kimeshatumika, ndiyo maana wengi waliofunga hupungua miili yao. Idi inapoanza mwili wa mtu nao unaanza zoezi jipya la kuweka akiba mpya. Kwa hiyo elimu juu ya mlo gani wa siku ya Idi na siku nyingine zinazofuata ni jambo la msingi. 

Kwa vile kipindi chote cha Ramadhani mwili umezoea kula usiku tu, ni vyema siku ya Idi iwe na mlo maalum, yaani ule mlo utakaofurahiwa na kila mtu katika familia. Vile vile mlo wa siku ya Id na siku zinazofuata lazima uwe mlo kamili (Balance diet) ili mwili uweze kujijenga upya. Hata hivyo, tusisahau kanuni za lishe kuwa: 

Kula sana ni chanzo kikubwa cha maradhi mbalimbali kwa binadamu. Inawezekana katika jamii fulani baadhi ya watu wakakosa uwezo wa kupata/kununua chakula kwa ajili ya siku ya Idi. Wasiwasi huo ni mkubwa zaidi tunapoitazama nchi ya Tanzania ambayo karibu nusu yake ina njaa kali. 

Dini ya Kiislamu imeweka sheria (ibada) kwa kila Muislamu mwenye uwezo japo wa kawaida atoe zaka maalum ya funga ya Ramadhani (Zakatul Fitr) na kuwapa wale wasiokuwa na kitu. Kama ibada hiyo itatekelezwa ipasavyo inawezekana hasa siku ya Idi kila mtu (hasa muumini) atakuwa na chakula kizuri na chakutosha na pia ataweza kukidhi mahitaji yake mengine. 

Tunamalizia makala hii, tukizingatia umuhimu wa lishe bora kwa kuwakumbusha na kuwaomba Waislamu wenye uwezo (japo akiba ya shilingi mia tano) watowe zakatul Fitr. 
 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
Tahariri 
Onyesheni ushujaa wa Badri 

Daniel kuwatimua waumini Msikitini 

Waislamu Moshi: Wadai kulishwa nguruwe, vibudu 

Dondoo za Kisakolojia 
Na. Abu Halima Sachangwa 

Kona ya WachaMungu  

Jicho la Uzalendo 

Maulana Sayyid Jamal-Din Afghan 1214 - 1254 (1838-1897) - 2 

Vipi umoja wetu uwe hatari ? 

MASHAMBULIZI YA MAREKANI NCHINI IRAQ  

Marekani si rafiki mwema  

Tunahitaji UN ya Waislamu - 2  

Njia bora zitakazotusaidia kuwalea watoto 
Na Ust. Hashim Rusaganya, Mombasa 

Ijue Madrasatul-Qaadiriya Sokoni I Arusha. 
Na Habiba Swedi, Arusha 

Tutafute kwanza ufalme wa Allah (s.w.) 
Na Mwapwani Mohammed 

Sheikh Kisiwa atunuku zawadi 

Chuo cha Kilimo Ukiriguru kupata Msikiti mpya  
Na Mwandishi Wetu, Mwanza  

Huduma za maji Kondoa haziridhishi 
Na Abu Zuberi, Kondoa  

Mnyororo wa imani 
Na Sheikh Bernard P. Nyangasa 

Je, Yesu alibatizwa? 
Na Muhibu Said  

Kufuatia Waislamu kuritadishwa Merela Morogoro: Masheikh wa mjini watupiwa lawama  

Abiria walaani kumwagiwa pombe Kondoa 

Sheikh Bafadhil ateuliwa kudhamini waandishi wa habari Morogoro 
Na Mussa Ally, Morogoro 

Sayansi na Teknolojia 
[Tatizo la mwaka 2000] 

Masomo ya Dini ya Kiislamu 

Barua za Wasomaji 

Chakula na lishe 
[Mlo wa siku ya Idd] 
 


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita