|
|
| Tunahitaji
UN ya Waislamu - 2
Na Tahir Rashid New York: Mji maarufu kuliko yote leo duniani, ni mji huu wa New York.Hapo ndipo ambapo Baraza Kuu la Ulimwengu liliposimikwa, nalo ni Baraza la Umoja wa Mataifa. Baraza hili liko katika nyumba ya Umoja wa Mataifa badala ya kuwa katika nyumba isiyo na kushirikisha (22:26). Na haya sio kwa kubahatisha. La. Bali ni mpango maalumu ili watu wageuzwe bila wao kujua. Na imekuwa hivyo. Siri hii New York maana yake ni "Kiini Kipya". Sasa hicho kiini cha kale ni kipi? (22:29) Hivi kusema New York kwa maana ya kiini kipya, Waingereza wenyewe wangaliita New Center. Sasa la kujiuliza ni kwamba ni ipi iliyokuwa Old Center? Zingatia uone kwamba katika huo mji uitwao New Center ipo nyumba inayoeleweka na walimwengu wote kwa maongozi na baraka (ruzuku). Kwa hiyo, tukisema ipi hiyo Old Center la kuangalia hapa ni kutafuta kuijua nyumba ya kwanza iliyowekwa kwa ajili ya ulimwengu wote (Umoja wa Mataifa wa kweli) yenye maongozi na baraka (3:96). Na jambo hili la uongozi limefichwa. (2:159, 2:146). Uongozi wa walimwengu wote ndio Uongozi (2:120) Nyumba hii ya Umoja wa Mataifa bandia iliyoko kiini kipya ndiyo ambayo Mola wetu anaiita "nyumba ya maangamizo". (14:28). Hutuamrisha kuua watoto (6:1379) (Uzazi wa mpango) kwa hiyo utaratibu wa maisha unavurugwa. Lengo la maisha ya watu limekuwa ni kuboresha mazingira yao binafsi bila kujali litakalo tokea. Kwa maana hii ituyakinie kwamba hivi leo duniani upande (kibla) watu wanapoelekea sio kiini cha kale (Makkah). Bali ni kiini kipya (New York). Jambo ambalo Mola wetu ametuasa kuwa tusifuate upande (kibla) wa wale waliopewa Kitabu (2:145) kwani tukifanya hivyo, tutakuwa "madhalimu". Kwa kuelekea leo kibla cha New York hakuna maana nyingine bali sisi tulioko Makanisani na Misikitini tumekuwa madhalimu bila kujua. Wito wa Allah (s.w.): Na Mwenyezi Mungu anatuita katika nyumba ya amani (The Old Center) (10:25) (kwani) amani itakuwa juu ya wale wanaofuata uongozi (Wake) (20:47). Hapo ndipo ilitakiwa liwepo baraza la (Usalama 2:124). Jambo ambalo wale waliopewa Kitabu wanalijua kama wanavyo wajua watoto wao (2:146). Lakini kwa dhulma yao (4:160) (huzua kwao kibla kingine 2:145) watu walioko Makanisani na Misikitini, tunafuata kibla hiki, kwa hiyo nasi sote tumekuwa madhalimu. (Ole wetu) siku ambayo itatufikia adhabu aseme wale waliodhulumu. "Mola wetu tuakhirishe muda kidogo, tutaitikia wito wako na tutawafuata Mitume ..." (14:44). Kwani huku kumfuata Mtume ni nini? Tujiulize kwanza, hivi leo anayefuatwa ni nani? Mtume leo hayupo, lakini kile alichokuja nacho kipo. Na ni agizo kwetu kuwa tuwaite watu kwa Mola wetu na mtu yeyote asikuzuie kufuata aya za Mwenyezi Mungu (28:87). Na ni nani dhalimu kuliko yule anayekumbushwa aya za Mola wake akawa anazipuuza, na akayasahau yaliyotangulizwa na mikono yake. (18:57) Watu badala ya kukampeni jina kwa ajili ya Allah (s.w.) wao hukampeni kwa ajili ya majina yasiyokuwa jina Hili. Basi wasituzuie (kukampeni kwa ajili ya Rais wetu Allah) wale wasioamini na wafuatao matamanio yao. (20:16). Kwa kufuata matamanio yao (kibla chao 2:145) tumekuwa madhalimu pasipo kujua (30:26). Kumfuata Mtume! Mwenyezi Mungu aliwatuma Mitume wawili na akawazidishia nguvu kwa Mtume wa tatu; lakini watu waliwakadhibisha (36:14) kwa kuendelea kufuata mila za wakuu wao (7:88-89). Basi akaja mtu akisema "enyi watu wangu wafuateni mitume hawa" (36:20). Kwa sababu kwa kuwafuata Mitume ndio kumuabudu Muumba (36:22). Usipowafuata Mitume utashika Miungu mingine badala Yake (26:23) na huo ndio kuwa katika upotofu uliodhahiri (36:24). Udhalimu maana yake (31:11). Tusijesema "Wallahi", kwa yakini tulikuwa katika upotofu ulio dhahiri, tulipokuwa tukikufanyeni sawa na Allah. Na si wengine hawa wanaofanywa sawa na Allah ila ni (watu) waovu (26:97-99). Nao ni wakuu wa miji (6:123). Kwa kuwafuata wakuu wetu wa miji, ndio upotofu uliodhihiri. Kwani wao ofisi zao huelekea Ikulu iliyoko mji mkuu. Na Ikulu hiyo iliyopo mji mkuu imeelekea Ikulu ya dunia iliyoko Kiini Kipya. Hivyo, kwa ulaini maongozi ya Allah yametiwa kapuni. Ni kwa kuelekea Ikulu ya dunia iliyoko Makkah ndio Kumfuata Mtume (2:44) ili tuongoke (2:150). Said Rajab. Nyanyua mikono tuombe, kwani si mwingine bali ni wewe uloleta hoja hii adhimu. "Mola wetu tumesikia na tutatii tunakuomba msamaha. Na marejeo ni kwako. (2:285). Mola wetu usizipotoe nyoyo zetu baada ya kutuongoza na utupe rehema itakayo kwako. (Wallah jambo hili la mji mkuu wa dunia (Makkah) limefichwa) hakika Wewe ndiye Mpaji Mkuu (3:8). Mola wetu usiendelee kututesa kwa kusahau kwetu (tukakosea na kufuata maongozi ya New York). Hivyo, usitubebeshe mgizo kama ulivyowabebesha wale waliokuwa kabla yetu. Usitutwike tusiyoyaweza, na utusamehe, na utughufirie, na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tusaidie juu ya makafiri. (2:286). Hali yetu ni mbaya. Tuko Misikitini na Makanisani na tunafanywa kugombana, kumbe kikulacho kiko nguoni mwako. AMIN Inaendelea toleo lijalo
|
YALIYOMO
Tahariri Onyesheni ushujaa wa Badri Daniel kuwatimua waumini Msikitini Waislamu Moshi: Wadai kulishwa nguruwe, vibudu Dondoo za Kisakolojia
Maulana Sayyid Jamal-Din Afghan 1214 - 1254 (1838-1897) - 2 MASHAMBULIZI YA MAREKANI NCHINI IRAQ Njia bora zitakazotusaidia kuwalea
watoto
Ijue Madrasatul-Qaadiriya Sokoni
I Arusha.
Tutafute kwanza ufalme wa Allah (s.w.)
Chuo cha Kilimo Ukiriguru kupata
Msikiti mpya
Huduma za maji Kondoa haziridhishi
Mnyororo wa imani
Je, Yesu alibatizwa?
Kufuatia Waislamu kuritadishwa Merela Morogoro: Masheikh wa mjini watupiwa lawama Abiria walaani kumwagiwa pombe Kondoa Sheikh Bafadhil ateuliwa
kudhamini waandishi wa habari Morogoro
Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|