|
|
| Kugeuzwa
nyumba za Wakfu Baa, sasa...
Daniel kuwatimua
waumini Msikitini
Masjid Mwinyi umejengwa katika kiwanja ilipokuwa moja ya nyumba za marehemu Hajat Aziza Omar - Kiwanja Na. 23 kitalu K. No. 66 mtaa wa Moshi. Kutokana na usimamizi aliopewa na Hakimu Natalia Kimaro juu ya nyumba hizo za Wakfu Bw. Daniel anadai kwamba hata Masjid Mwinyi ni mali yake kwa hiyo kama waumini wanataka kuendelea kuswali hapo walipe kodi. Akipigania kupata kodi yake kupitia mahakama ya Kisutu hivi karibuni; Bw. Daniel aliiambia mahakama kupitia maandishi: "Naiomba Mahakama itoe Eviction Order ya kusimamisha ibada katika kiwanja Na. 23 Kitalu K. No. 66 Moshi Street Ilala." Akielezea sababu ya kuomba mahakama iwatimue waumini Msikitini hapo alisema kwamba waumini hao "gharama wanazozitumia hawazilipii (ikiwa ni) jengo lenyewe, kiwanja, maji na umeme". Akaongeza "maswala hayo yanafanya nisimamishe shughuli za Ibada". Kabla ya hatua hii ya kuitaka mahakama iwatimue waumini; Julai 2, 1998 Bw. Daniel aliiomba Ofisi ya Ardhi Kanda ya Ilala imkabidhi nakala ya barua ya toleo (offer) ya kiwanja hicho cha Msikiti ambayo ilitolewa kwa jina la Aziza Omar. Suala hilo lilikuwa gumu kwa Afisa Ardhi Bw. J.M. Mahela kwa hiyo akamshauri Bw. Daniel Zakaria amuombe Kamishna wa Ardhi atengue barua ya toleo kwa jina la marehemu Aziza Omar. Kwa mujibu wa maelezo ya Bw. Ardhi huyo kama yalivyo kwenye barua No. ILA/3632/14 ya Julai 28, 1998, barua mpya ya toleo (offer) yaweza kutolewa kwa jina la Bw. Daniel baada ya Kamishna kutengua ile ya awali. Ukiacha Msikiti, Bw. Daniel alishachukua nyumba nyingine mbili za Wakfu ambazo zipo Mtaa wa Somali No. 58 Gerezani na Mchikichi No. 59 Kariakoo. Nyumba hizo ziliwekwa Wakfu na Hajat Aziza Omar kwa hati ya kiapo MCA/284 2/84 Mahakama ya Mwanzo ya Kariakoo Oktoba 11, 1990. Kwa kauli ya maandishi Hajat Aziza alisema "Natoa wosia nikifa nyumba hizo ziwe WAKFU kwa ajili ya MASJID MWINYI uliopo No. 66 MOSHI STR ILALA D’SALAAM". Pamekuwa na wasiwasi miongoni mwa waumini juu ya ushirikiano uliopo baina ya Bw. Daniel Zakaria na baadhi ya wasimamizi wa nyumba za Wakfu za Hajat Aziza. Wasiwasi huo umekuja kwa kuona kwamba pamekuwa na uzito wa kuchukua hatua stahiki hadi Bw. Daniel anathubutu kuweka Baa kwenye nyumba ya Wakfu. Waumini mbalimbali ambao waliongea na gazeti hili walisema kwamba hawaelewi ni kwanini Masheikh hao wasimamizi wa Wakfu hawajafungua kesi kupinga hukumu ya Hakimu Natalia Kimaro kumpa Bw. Daniel usimamizi wa nyumba za Wakfu. Wala hawaelewi ni kwanini kama wameshindwa kukabiliana na Bw. Daniel kwa sababu yoyote iwayo hawajawaita Waislamu wa Dar es Salaam wakawakabidhi jukumu hilo. Hata hivyo wamesema kwamba iwe vyovyote iwavyo maadhali wana uhakika kuwa hizo ni nyumba za Wakfu hatakaa Daniel wala atakayeuziwa nyumba hizo na Danie Magereza yashukuru misaada ya Jumuiya ya Kiislamu JESHI la Magereza mkoani Morogoro limeishukuru Jumuiya ya Islamic Foundation ya mjini hapa kutokana na misaada mbalimbali iliyoitoa kwa wafungwa wa magereza kadhaa ya mji huu. Katika barua zao kwa Mudir wa Islamic Foundation, Sheikh Suleiman Kiriri zilizoandikwa kwa nyakati tofauti, viongozi wa Magereza hayo pamoja na kuipongeza jumuiya hiyo, waliiomba iendelee kuwasaidia wafungwa na kuwaomba Waislamu popote pale walipo kuiga mfano huo. Misaada iliyotolewa na jumuiya hiyo ni pamoja na Hijab kwa wafungwa wote Waislamu wa gereza la wanawake Kingorwila, madawa yenye thamani ya shilingi 150,000 kwa wafungwa waliopata tohara katika gereza la Mtego wa Simba na msaada wa futari na daku kwa magereza saba yenye jumla ya wafungwa 206 waliofunga. Magereza hayo ni Mtego wa Simba, Mkono wa Mara, wanawake Kingoruwila, mahabusu Morogoro mjini, Mbigiri, Wamikuu na Wami Vijana. Misaada mingine iliyotolewa na Islamic Foundation ni ujenzi wa Msikiti na nyumba ya mwalimu katika gereza la Mtego wa Simba. Katika barua yake ya Desemba 27, 1998 yenye kumbukumbu nambari 166/Moro/3/84 kwa Islamic Foundation, Mkuu wa Gereza la wanawake ASP Angela ameomba ushirikiano wa gereza lake na jumuiya hiyo ya Kiislamu usiishie tu katika mwezi huu wa Ramadhani bali wakati wowote nafasi itakaporuhusu. Naye Mwenyekiti wa Msikiti wa Magereza Mtego wa Simba Bw. Juma Lipalala katika barua yake yenye Kumbukumbu nambari 166/Moro/1/379 kupitia kwa Mkuu wa gereza hilo Bw. Ruvugo aliiomba Islamic Foundation pamoja na Waislamu wengine kuendelea kuwasaidia wafungwa magerezani, hali ambayo si tu itawafariji bali pia itasaidia kubadili tabia zao. |
YALIYOMO
Tahariri Onyesheni ushujaa wa Badri Daniel kuwatimua waumini Msikitini Waislamu Moshi: Wadai kulishwa nguruwe, vibudu Dondoo za Kisakolojia
Maulana Sayyid Jamal-Din Afghan 1214 - 1254 (1838-1897) - 2 MASHAMBULIZI YA MAREKANI NCHINI IRAQ Njia bora zitakazotusaidia kuwalea
watoto
Ijue Madrasatul-Qaadiriya Sokoni
I Arusha.
Tutafute kwanza ufalme wa Allah (s.w.)
Chuo cha Kilimo Ukiriguru kupata
Msikiti mpya
Huduma za maji Kondoa haziridhishi
Mnyororo wa imani
Je, Yesu alibatizwa?
Kufuatia Waislamu kuritadishwa Merela Morogoro: Masheikh wa mjini watupiwa lawama Abiria walaani kumwagiwa pombe Kondoa Sheikh Bafadhil ateuliwa
kudhamini waandishi wa habari Morogoro
Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|