|
|
|
ASKARI wa Tume ya Jiji la Dar es Salaam wamelalamikiwa kwa kuchukua mkaa wa mfanyabiashara hiyo katika eneo la Msasani Mikoroshoni Jijini hivi karibuni. Akiongea na mwandishi wa habari hizi, Bw. Ally Kasinge ambaye ndiye mmiliki wa biashara hiyo ameeleza kuwa Februari 4 mwaka huu askari hao wa Tume ya Jiji walivamia eneo lake la biashara na kupora magunia 46 ya mkaa kwa madai kuwa hakuwa na leseni ya kufanya biashara katika eneo hilo. Bw. Ally amesema kuwa wakati hayo yanafanyika yeye alikuwa amekwenda kunywa chai na kuwaachia vijana wawili kumtizamia biashara yake, vijana hao aliwataja kuwa ni Bw. Salum Athumani na Yahya Mohamed walipelekwa katika mahakama ya Tume ya Jiji na kila mmoja kuandikiwa kuwa amekutwa na gunia mbili za mkaa na hivyo kutozwa faini ya shilingi 10,000 kila mmoja. Bw. Ally ameendelea kueleza kuwa baada ya kulipa faini hizo bado hakurudishiwa mkaa wake na alipojaribu kufuatilia kwa Mkuu wa Mkoa alitakiwa kwanza apitie ofisi za Mkuu wa wilaya. Amesema aliporudi wilayani kuelezea kile alichotendewa na askari wa Tume ya Jiji aliambiwa kama haridhiki afuatilie ngazi nyingine. Bw. Ally amesema kuwa anaona haki yake inapotea na hivyo anaomba vyombo vinavyohusika kumsaidia ili aweze kupata haki yake kwani anachosema ni kwamba wafanya biashara wote wa mkaa katika eneo la Msasani Mkoroshoni hawana leseni lakini yeye peke yake ndiyo aliyekamatwa. Suala la askari wa Jiji kuwavamia wafanyabiashara ndogondogo hapa jijini limekuwa likishamiri kwa kasi kubwa katika siku za karibuni. Jitihada za kumpata Mwenyekiti wa Tume ya Jiji kuhusiana na suala hili
hazikufanikiwa hadi gazeti hili linakwenda mitamboni wiki hii.
|
YALIYOMO
Tahari
Mwaka mmoja wa mauaji ya Mwembechai:
Waliouawa ni wanne
Waasisi wa TAA waibuka kupigania haki zilizoporwa Kuhujumiwa Waislamu kielimu: Mzazi adai mwanafunzi Adam Rashid kafelishwa Maoni yetu: Tuondoleeni wenye mikono ya damu MARADHI YA KISAIKOLOJIA: MULTIPARAPHILIASIS Askari wa Tume ya Jiji wapora mkaa Kuchangia Radio Kheri Broadcasting Station Yesu Kristo na Yohana Mbatizaji
Wakereketwa CCM wawakosha
wauaji wa Mwembechai
Ufugaji holela wa nguruwe
waikumba Dodoma
Watembelea na kusaidia wagonjwa Arusha Mkuu wa wilaya awatimua Masheikh
ofisini kwake
Sayansi na Teknolojia
Chakula na Lishe
Kumbukumbu ya mauaji Mwembechai
|