|
|
|
KATIKA miaka ya awali ya maisha ya Utume ya Mtume (s.a.w.) Waislamu walipata mateso makubwa sana. Zaidi mateso hayo yaliongozwa na waliokuwa wakuu wa koo za Kiquraysh na wale wa dini za kishirikina. Abujahal aliyekuwa mmoja wa makamanda wa kikosi cha kuwatesa Waislamu aliongoza mashambulizi dhidi ya Waislamu dhaifu ambao hawakuwa na silaha. Hamza ambaye alikuwa miongoni mwa viongozi walioheshimiwa sana na ambaye alikuwa pia hajasilimu alipofika kwenye tukio hilo hakuweza kuhimili kuona watu wasio na silaha wakiteswa. Alimnasa kibao kamanda Abujahal na ‘askari’ wale watesaji kila mmoja akasambaa katika njia tofauti. Hizo zilikuwa zama zilizoitwa za ujahili ambapo sifa ya kabila au taifa ilitegemea uwezo wake wa kupigana, kuua na kupora mali toka kabila jingine. Zilikuwa zama za kuzika watoto wa kike wakiwa hai. Karne kumi na tano baadae Waislamu wasio na silaha wameuliwa na polisi kwa amri ya Kamanda wao. Kama walivyokuwa dhaifu Waislamu wale wa wakati wa Kamanda Abujahal Waislamu hawa wa Tanzania huru kwa udhaifu wao wanalinganishwa na watoto ambao "bado wananyonya". Lakini hata hivyo wanapigwa risasi na kuuliwa. Miaka 1500 iliyopita alipatikana Hamza aliyewatetea na kumtia adabu Kamanda anayeua watu wasio na silaha. Leo Makamanda wanapongezwa na wakuu wa nchi! Zile zilikuwa zama za kiza. Leo ni zama za kupigania haki za binadamu, zama za demokrasia, zama za serikali zinazowekwa na watu kwa ajili ya watu! Lakini leo wauaji wanapongezwa wakati zama za kiza walilaaniwa na kutiwa adabu. Wahshiy alikuwa mtumwa wa Hind bint Utbah mke wa Abu Sufyani. Katika vita vya Uhud Wahshiy alipewa amri amsake Hamza mpaka amuue. Na kweli akamuua. Baadaye Wahshiy alisilimu, hata hivyo ikawa kila Waislamu wakikutana naye humkumkumbuka Hamza na kupata majonzi. Mtume (s.a.w.) akamwamuru ahamie mji mwingine wa mbali. Leo sisi tuna akina Wahshiy ambao hawakuamrishwa kitumwa wala hawakuwa vitani; bado tupo nao. Baya zaidi wanazidi kutukejeli kwa kutuhubiria upendo, amani na usalama. Ni vyema serikali angalau ikajali hisia zetu ikatuondolea Wahshiyi hawa machoni petu. Kila tusikiapo sauti zao na kuwatia machoni kwenye majukwaa ya kisiasa au maofisini mwao wanatuletea majonzi kwa wenzetu waliouliwa Mwembechai. |
YALIYOMO
Tahari
Mwaka mmoja wa mauaji ya Mwembechai:
Waliouawa ni wanne
Waasisi wa TAA waibuka kupigania haki zilizoporwa Kuhujumiwa Waislamu kielimu: Mzazi adai mwanafunzi Adam Rashid kafelishwa Maoni yetu: Tuondoleeni wenye mikono ya damu MARADHI YA KISAIKOLOJIA: MULTIPARAPHILIASIS Askari wa Tume ya Jiji wapora mkaa Kuchangia Radio Kheri Broadcasting Station Yesu Kristo na Yohana Mbatizaji
Wakereketwa CCM wawakosha
wauaji wa Mwembechai
Ufugaji holela wa nguruwe
waikumba Dodoma
Watembelea na kusaidia wagonjwa Arusha Mkuu wa wilaya awatimua Masheikh
ofisini kwake
Sayansi na Teknolojia
Chakula na Lishe
Kumbukumbu ya mauaji Mwembechai
|