|
|
| Home |
Sheikh wa Wilaya Same ahimiza Waislamu kushiriki tamashaNa Mwandishi WetuSHEIKH wa Wilaya ya Same Sheikh Mohamed Mustafa amewahimiza Waislamu wa Wilaya ya Same kushiriki tamasha la ujenzi wa Chuo cha Kiislamu huko Kirinjiko, Mwembe. Tamasha hilo ambalo litawahusisha Waislamu wa nchi nzima litaanza June 26, hadi Julai 3, 1998. Akizungumza katika swala ya Ijumaa Juni 12 mjini Same Sheikh Mohamed Mustafa alisema kwamba chuo hicho ni kwa manufaa ya Waislamu wote. Katika kutoa nasaha zake Sheikh Mustafa amesema kwamba kitu chochote kizuri ni kigumu upatikanaji wake. Ni cha kuhangaikia. Akasema hata Mtume (s.a.w.) alipata taabu katika kuueneza Uislamu kwahiyo akawasihi Waislamu wa Same wasikate tamaa kutokana na ugumu unaoambatana na ujenzi wa Kirinjiko Aliwaambia kwamba wanachotakiwa wao ni kufanya juhudi na kutoa michango
yao na hata kama umri wao utakwisha kabla ya chuo kukamilika jaza yao wataipata
kwa Mola wao na wengine wataendeleza kazi hiyo.
Sheikh awataka wanawake wajistiriNa Badru KimwagaIMAMU Mkuu Msaidizi wa Msikiti wa Manyema, uliopo Kariakoo, jijini, Sheikh Abdulrahman , amewataka Waislamu nchini kuwakemea mabinti na wake zao, kutembea bila kuzingatia sheria na maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki, alipokuwa akihutubia waumini wa Msikiti wa Mwinyimkuu, uliopo Magomeni Mapipa, jijini Dar es Salaam kwa kusema kuwa wazazi wa Kiislamu, hasa wanaume wanatakiwa kuwaasa wake na mabinti zao, kujistiri miili yao ili kuweza kuepusha vishawishi vinavyopeleka wanaume kuwatamani na hatimaye kuwabaka. Sheikh Abdulrahman aliongeza kwa kusema kuwa, ni jambo la kawaida kwa siku za hivi karibuni, wake na mabinti wa waumini wa Kiislamu kutembea nusu uchi, huku wazazi wakiona jambo hilo ni sawa na la kawaida bila kujua wanamkosea Mwenyezi Mungu. "Mabinti zetu na wake zetu, siku hizi wanatembea uchi uchi... uchi... kabisa na sisi tunaona sawa ... mwanamke anavaa nguo nyepesi na kuonyesha ramani ya mwili wake.... hapo akibakwa atalaumu nani na hali mwenyewe anajitangaza kubakwa... tena ni mabinti na wake za waumini ambao safu ya kwanza ya swala hawakosi... tukemee na tukosane nao", alisema Sheikh huyo. Na kuongeza kuwa, hata ndani ya Qur'an, Mtume Muhammad (saw) aliambiwa na Mwenyezi Mungu (sw) kuwa awaambie wake zake na mabinti zake kujistiri na wake wa waumini, ili kuwafanya wasipate kero kutoka kwa wanaume, kuwataka, kwani wajitambulisha kuwa wacha Mungu. Aidha, Sheikh alilaumu chama cha waandishi wa habari wanawake nchini (TAMWA), kutokana na hoja waliyopeleka bungeni ambayo imepitishwa kuwa muswada tayari kuwa sheria juu ya kujamiiana bila kupeleka na hoja ya kukemea na kukataza uvaaji nguo fupi kwa wanawake. Alisema kuwa ni wanawake wenyewe wanaojirahisisha kwa kutojisitiri miili yao. "Iweje iwepo sheria ya kuwalaumu wabakaji, huku hakuna sheria kwa wenye kushawishi, ni uongo na utafutaji sifa kwa viongozi wa TAMWA, kwani nao pia huvaa nguo fupi maofisini mwa", alidai Sheikh Abdulrahman. Hivi karibuni TAMWA ilipeleka hoja bungeni kuhusiana na masuala ya kujamiiana na kuzuia kubaka. Sheria hiyo baada ya kupitishwa na Bunge inategemewa kuanza kutumika
mwakani, iwapo itatiwa saini na Rais Benjamin Mkapa, kuidhinisha kuwa sheria.
SHEIKH Mohamed Mustafa.Madrasat Al-Hujuun washerehekea mwaka mpyaNa Mwandishi Wetu AKINA mama wa Madrasat Al-Hujuun Kitangiri, Mwanza walifanya hafla ya kusherehekea mwaka mpya wa Kiislamu hivi karibuni. Katika sherehe hiyo iliyotanguliwa na usomaji wa Qur'an, ulifuatiwa na risala ya akina mama kwa wageni waliohudhuria sherehe hiyo. Risala ya akina mama hao pamoja na mengine, kubwa mno lilikuwa kulaani mauaji ya Waislamu wa Mwembechai na kudhalilishwa kwa akina mama wa Kislamu. Aidha, risala hiyo ilikiita kitendo hicho ni cha ukiukwaji wa haki za binadamu na kitendo cha kinyama. Risala hiyo iliyosomwa na Mwenyekiti wa Madrasa hiyo, Bibi Ziyada Ramadhani uliilaumu serikali kwa kile walichokiita ubaguzi. Walisema serikali ya Tanzania inajidai kila siku kuwa haina dini, lakini kwa kitendo hicho imedhihirisha inayo dini yake. Akina mama hao waliendelea kueleza katika risala yao kuwa, akinamama wa Kiislamu na Waislamu wote katika nchi hii wanaonekana siyo binadamu wanaostahili kupewa haki kama akina mama wengine na raia wengine. Na hii ni kwa sababu ya dini yao ya Kiislamu. Kinachoshangaza walisema ni kuona serikali inapiga kelele kuhusu hazi za akina mama wa Kitanzania na kupambana na wale wanaowadhalilisha, lakini udhalilishaji unapofikia kwa akina mama wa Kiislamu inaonekana si tatizo. Wakati huo huo, Madrasa Sharifatur-Rahman iliyopo Tandale, Mtogole ilifanya hafla ya kuukaribisha mwaka mpya wa 1419 madrasani hapo hivi karibuni. Katika hafla hiyo, mgeni rasmi Alhaj Yusuf Zakaria alisisitiza umuhimu wa kuwaelimisha watoto na akina mama ili kujenga jamii yenye maadili mema. Alihimiza Waislamu wajenge na kuendesha vituo cha kulelea watoto, shule za awali za watoto (Nursery School) n.k. Awali Maalim Kitwana alitoa ufafanuzi juu ya dhana potofu iliyojengeka juu ya kutenganisha elimu - elimu ya dini na dunia. Alisema elimu zote ni lazima zisomwe na zote ni muhimu. Ili kuisaidia Madrasa hiyo, uliendeshwa mnada na michango ambapo fedha taslimu na ahadi zilitolewa. |
Maoni yetu:
Unafiki si suala la wakati fulani
Historia ya harakati za ukombozi wa Kashmir Sheikh wa Wilaya Same ahimiza Waislamu kushiriki tamasha Sheikh awataka wanawake wajistiri Madrasat Al-Hujuun washerehekea
mwaka mpya
Uislamu ni mfumo wa maisha - Mbukuzi Pole ya Mwinjilisti Kusupa ni kejeli
|
| An-nuur Home | Links | Islam Tanzania | Matoleo yaliyopita |