AN-NUUR
Na.154 Safar 1419, Juni 19-25, 1998
 
Home 

Links 

Islam Tanzania 

Matoleo ya nyuma 
 
 

Unafiki si suala la wakati fulani 

Matukio ya kihistoria yaliyotajwa katika Qur'an, yakibainisha njia ya Madhalimu, makafirina wale wanaoamini visivyo sawa, yana madhumuni ya kutoa maonyo kwa wanadamu na kuwaongoza kwenye njia Sahihi ya kuishi, yenye msingi wake katika Ufalme wa Allah, Ukhalifa wa Mwanadamu na kuwa kwake Muulizwa (Mas-ul) mbele ya Allah (katika Siku ya Hukumu) juu ya mambo yaliyomhusu. 

"Je imekufikia hadithi ya Musa? Hapo Mola Wake alipomwita akiwa katika bonde takatifu la Tuwa. (Na Akamwamuru), nenda kwa Firauni, kwani kwa hakika yeye amechupa kabisa mipaka yote. Na umwambie hivi: `Je unapenda kutakaswa (kutokana na matendo yako maovu) na kwamba mimi nikuongoze kwa Mola wako nawe umche?' Halafu, Musa kamwonyesha ishara kubwa (za ukweli wake). 

Lakini yeye alizikanusha na akaasi. Halafu, juu ya hayo, akageuza mgongo wake akifanya jitihada dhidi ya Allah, na akawakusanya pamoja watu wake na kuwatangazia akisema, `mimi ndiye Mola wenu niliyejuu kabisa.' Lakini Mwenyezi Mungu Akamwadhibu, na Akamfanya awe mfano kwa maisha ya ulimwangu ujao na vile vile kwa ulimwengu huu. 

Kwa hakika, katika hayo (yaliyotokea kwa Firauni) kuna onyo kubwa kwa mtu anayeogopa." (79:15-25). 

Ingekuwa kama aina ya watu wenye mwelekeo wa fikara kama zile za Firauni au za Nimrud, au kama zile za watu wa Taifa la Add au Thamud zisiweze kuweko tena katika nyakati za mbele baada ya kuwa wale waliokuwa na fikra hizo hapo zamani wameshaangamizwa basi kutolewa kwa mifano yao (katika Qur'an) kama maonyo kwa watu wa siku za mbele kusingeleta maana yoyote ile. 

Ni nani, kwa kutumia akili yake anayeweza kukana kuweko kwa Firauni au Nimrud miongoni mwa watu siku ya leo? Je, hawako wale ambao ni lazima waukweze Ufalme wao juu ya watu wengine utadhani labda hao ndio walio juu yao kabisa? Ni kwa sababu ipi iliyo nzuri basi, hata mtu atadai kwamba hapawezi kuweko mnafiki, hawezi kuweko Ibn Ubayyi au Abu `Amar miongoni mwetu leo? Je, hakusema Mtume (SAW). 

ALAMA ZA WANAFIKI 

"Ziko alama tatu za unafiki. (Imam Muslim kaongeza)hata kama anafunga, anasali na anang'ang'ania kwamba yeye ni Muislamu. (Baada ya hapo, wote wawili, (Bukhari na Muslim wakasema) anaposema kuwa huwa anadanganya, anapoweka ahadi, huivunja, na anapoaminiwa, anaisaliti amana hiyo." 

"Abdallah bin Amr alihadithia kwamba Mtume (SAW) alisema: `Mambo manne yanamfanya mtu mwenye kuwa nayo awe ni mnafiki mtupu na yeyote mwenye kuwa nalo moja kati ya hayo, anayo sifa mojawapo ya unafiki mpaka awe ameachana nalo. Anapoaminiwa, huvunja uaminifu, anaposema _ hudanganya, anapotoa ahadi (aina ya mkataba) haitimizi,na anapogombana huenda mbali na haki." (Mishkat akirejeza kutoka kwa Bukhari na Muslim). 

Ibn Umar alihadithia kwamba Mtume (SAW) alisema: "Mnafiki ni kama kondoo jike anayeyumba yumba kati ya makundi mawili ya kondoo, wakati mmoja anageuka kwenye kundi hili na katika wakati mwingine anageukia kwenye jingine." (Mishkat anarejeza Hadithi hii kutoka kwa Muslim). 

Ni kweli na wala hapana shaka yoyote, kwamba Hadithi za Mtume zilizotajwa hapo juu na wala siyo nyingine zozote, zinazungumzia juu ya kuweko kwa unafiki na wanafiki kama ulivyokuwa katika wakati wake mwenyewe. 
 
 

 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI  

Maoni yetu: 
Kama hodari wa kuhoji Tuhoji pia Tume ya Majeshi ya Vita 

Waraka wa Abu Aziz  

Unafiki si suala la wakati fulani  
  
Wakatoliki wawili wasilimu 

Ashitakiwa baada kusilimu 

Historia ya harakati za ukombozi wa Kashmir 

Sheikh wa Wilaya Same ahimiza Waislamu kushiriki tamasha 

Sheikh awataka wanawake wajistiri 

Madrasat Al-Hujuun washerehekea mwaka mpya 
 
Kutoa talaka ovyo ovyo ni kuchupa mipaka ya Allah - Ust. Khamis Salim 

Uislamu ni mfumo wa maisha - Mbukuzi 

Pole ya Mwinjilisti Kusupa ni kejeli 
 
 

 
 Maoni yoyote kuhusu ukarasa huu yapelekwe kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
An-nuur Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita