|
|
| Home |
Wakatoliki wawili wasilimuNa Mwandishi Wetu, MtwaraWAKATOLIKI wawili Bw. Thomus Matei na Bi. Reinata George wamesilimu Juni 13, mjini Mtwara na kufunga ndoa katika Msikiti wa Ijumaa Chikongola. Waislamu hao wapya walisilimishwa na Sheikh Khamis Mchewa. Bw. Thomus Matei hivi sasa anaitwa Bw. Suleiman wakati Bi. Reinata amechukua jina la Zamda. Baada ya kusilimu, Waislamu hao wapya waliomba wafungiwe ndoa, Bibie Zamda alidai mahari ya shilingi 6,000, Waislamu walimchangia Bw. Suleiman zaidi ya shilingi 8000 na ndoa kufungwa hapo hapo na Sheikh Jamaldeen Salim. Katika nasaha zake kwa Waislamu, Sheikh Jamaldeen aliwahimiza Waislamu kuitangaza dini ya Allah bila ya kuogopa vitisho vya maadui. Alisema kwamba kuutangaza Uislamu na kufanya majadiliano juu ya Mungu Mmoja wa Kweli ni amri ya Allah (sw). |
Maoni yetu:
Unafiki si suala la wakati fulani
Historia ya harakati za ukombozi wa Kashmir Sheikh wa Wilaya Same ahimiza Waislamu kushiriki tamasha Sheikh awataka wanawake wajistiri Madrasat Al-Hujuun washerehekea
mwaka mpya
|
| An-nuur Home | Links | Islam Tanzania | Matoleo yaliyopita |